DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mahakama ya Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza, Machi 6, 2026 imewaachia huru watuhumiwa saba waliokuwa wakikabiliwa na shitaka la uchomaji Moto, Shauri la Jinai Namba 2037 la Mwaka 2026 baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo pasi kuacha shaka.
Taarifa ya LHRC imeeleza kuwa, Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Mashitaka amewafutia vijana hao shitaka la Uhaini lililokuwa likiwakabiri mahakamani hapo kwa mamlaka aliyonayo kwa mjibu wa kifungu cha 92 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya jinai.
Washtakiwa walioachiwa huru ni Peter Jackson Masulya (33) mkazi wa Buzuruga ambaye ni mwalimu, Sebastian Luchagula (47) mkazi wa Bujora, Zacharia Jumanne (20) mkazi wa Kanyama, Amos Mwita (29) mkazi wa Kisesa, Emmanuel Malagila (34) mkazi wa Nyankumbu, Delphine Muganyizi mkazi wa Mwahuli A, pamoja na Fred Ndege (29), mkazi wa Isangijo.
Soma Pia: Wakili Kisabo: DPP amewafutia mashtaka wengine walioshtakiwa Kisutu kwa uhaini
Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo, mmoja wa mawakili wa utetezi, Erick Mutta, amesema mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa upande wa Jamhuri haukuweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao saba.
Amesema katika shauri hilo upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi 14 kwa lengo la kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikiwakabili washtakiwa, huku washtakiwa wakijitetea wenyewe mahakamani.