Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema hakukuwa na nia kwa Wakili kufungua kesi ya jinai labda kuna sababu nyingine amba
yo haijafahamika na alichokifanya kuingilia kesi hii ni kutimiza majukumu yake kisheria kwa sababu leo ni kwa huyu (Mhe. Pauline Gekul) lakini kesho inaweza kuwa kwa mtu mwingine yoyote.
Amesema aliyefungua keshi ya Gekul alipeleka chini ya Kifungu cha 128 (2) (4) na ile sio Private Prosecution. Na sheria imetoa mwanya pale mambo mtu aridhiki kwa namna DPP anaendesha mashtaka anaweza kuomba kuendesha mashtaka yeye.
Anasema kilichotokea kwa Pauline Gekul ni kwamba Polisi walikuwa wanaendelea na Uchaguzi, mara DPP anaona kesi imesajiliwa Mahakama. Ambapo alifutilia kuangalia kama utaratibu wa kifungu cha namba 128 umefuatwa maana yeye kama DPP hakuwa anajua.
Anasema Polisi walikuwa hawajafika mwisho na uchunguzi na walikuwa wanachunguza vitu viwili kwa sababu Gekul alienda Polisi kushtaki na aliyeshtakiwa na Gekul naye alienda kushtaki Polisi. Na hivyo aliamua kuondoa kesi hiyo mahakamani kwa mujibu wa sheria
Amesema majarada ya Pauline Gekul yamefika ofisini kwakwe na wanafanyia kazi na pengine wikii hii ama watashtaki au hawatashtaki na kuna jarada ambalo Gekul analalamika na ambalo analalamikiwa.
View attachment 2862327