DPP wa Tanzania amepora uhuru wa mahakama, Mahakama nayo imeridhia

DPP wa Tanzania amepora uhuru wa mahakama, Mahakama nayo imeridhia

Yajayo yanatamausha!

DPP,TRA, WANACHUKUA kwa watuhumiwa na wafanyabiashara, WANAWEKA Hazina, WAAH Kwenye miradi mikubwa.
 
Mimi ningekuwa hakimu au jaji sikopeshi

Ukileta kesi isiyo na ushahidi kamili nakupangia tarehe ukija second time. Bila ushahidi naidismis kesi fasta

Ujinga ujinga
 
Kwa jinsi jiwe alivyoupata uraisi wa nchi hii,mtu yeyote anaweza kupata,Bashite,Ndugai,polepole,Kangi lugora,
Wote Hawa wanaweza kupata uraisi,maana tuna mfumo mbaya sana,jiwe hakutegemea kupata uraisi,Kikwete alivyoona,janja yake ya kumkata Lowasa,inaenda vibaya,akaona atafute jitu linalofahamika kidogo,jiwe akapatikana.
Nyerere ndie aliyeweka misingi mibovu Sana ya katiba hii aliyokopi toka kwa makomunist.
 
DPP ndio amekuwa mahakama, na
Mahakama inamsikiliza DPP , Leo viongozi wa uwamsho miaka 6 uchunguzi bado haujakamilika, hao
Mashahidi si washakufa??
 
DPP wa Tanzania amepora uhuru wa mahakama, mahakama nayo imeridhia.

Ni jambo la aibu kuwa DPP anamkamata mtu anamfungulia mashtaka yasiyo na dhamana kisha kila mshtakiwa akipelekwa mahakamani DPP anaiambia mahakama kuwa upelelezi haujakamilika. Aibu yako kubwa wewe DPP usiye hata na chembe ya utu.

Binadamu wa kitanzania anaona ameshateseka vya kutosha kutokana na nguvu uliyonayo juu yake anaamua kukubali yaishe. DPP kuna kupanda na kushuka. Ole wako! Unamkamataje mtu unamfungulia mashtaka hayo yasiyo na dhamana kisha kila uchwao unasema upelelezi bado? Iko wapi nguvu ya mahakama kutetea uhuru wake?

Mahakama ya Tanzania imegeuka kuwa msikilizaji wa anayosema na kuamua DPP, kama nchi tuna tatizo kubwa la udikteta. Narudia kusema tena na tena, huu utawala kuna watu wataandikwa kwenye vitabu maalum ili waje walipie wanayoyafanya kwa sasa! Nasema ole!

Kwa haya yanayoendelea ni bora Tundu Lissu asirudi kwa sasa. Haki ya wakosoaji nchi hii ipo katika mashaka makubwa.
Hivi Mganga yeye hawezi kushitakiwa kwa jambo lolote?
 
Siku hizi Mahakama ndo inaonekana kama ni kitengo tu cha serikali na DPP ndo mhimili wa dola. Yaaani mahakama inachezewa na kudharauliwa Kama mtoto mdogo.

Inasikitisha sana. Mahakama yenye majaji ambao walikuwa na uwezo wa kumgomea hadi Nyerere sasaivi inaendeshwa na mtu mmoja DPP
 
Mimi ningekuwa hakimu au jaji sikopeshi

Ukileta kesi isiyo na ushahidi kamili nakupangia tarehe ukija second time. Bila ushahidi naidismis kesi fasta

Ujinga ujinga
Ndivyo inatakiwa mkuu.

Tatizo weledi umekuwa adimu sanaa, na siasa imejikita huko kinyume na matakwa ya Katiba
 
Back
Top Bottom