DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

Waulize Djibouti
 
Du! Hawa majizi wametupiga pakubwa sana aisee!
 
Kama wewe una muda wa kwenda kuomba radhi ni wewe; Nenda kawaombe; ila kama tutakuwa tume-break terms sidhani kama radhi zako wanazitaka haya mambo yakienda mrama ni Pesa ndio zitaongea sio porojo...; Na bahati mbaya kama kutakuwa kuna malipo / fidia za kulipa basi ni watanzania ndio watagharamika....
 
watu kama wewe kuna siku Mungu akiisafisha hii nchi, mtabaki kama mapopo na makunguru kama walivyo sabaya na bashite sasaivi. kwasababu mmejaa unafiki na mnajali tu matumbo yenu hata kwenye vitu vya msingi wa nchi.
 
Iundwe tume ya wajumbe 50 iende Makao Makuu ya DP world kuomba radhi rasmi
 
Siyo vizuri kuleta taarifa za kupotosha. Lawama zinawahusu hao DP World (Waarabu wa Dubai), pamoja na Wazanzibari wawili walioamua kuuza bandari za Tanganyika, huku wakiacha zile za kwao.
 
Siyo vizuri kuleta taarifa za kupotosha. Lawama zinawahusu hao DP World, pamoja na Wazanzibari wawili walioamua kuuza bandari za Tanganyika, huku wakiacha zile za kwao.
DP wanahusikaje na mkataba mmesaini tayari bila kushurutishwa? vigezo na Masharti vilikuwemo ndani ya mkataba, nyie mkakimbilia kuweka saini tu bila kusoma. Kosa la nani? Next time (mikataba mipya/mwingine) kuweni makini kabla ya kusaini
**Kuna mengi ya kujifunza katika hili, tuache kushupaza makomwe kwenye kichaka cha 'uzalendo'
 
Kabla hatujawaomba radhi waulize kwanza mwenzie na H.E Ahmed Mahboob Musabih ni nani na cheo chake, maana kuna saini tu hakuna jina wala cheo., huoni kama hata wao wanatakiwa watuombe radhi kwa kumuweka asiyejulikana.
 
Kabla hatujawaomba radhi waulize kwanza mwenzie na H.E Ahmed Mahboob Musabih ni nani na cheo chake, maana kuna saini tu hakuna jina wala cheo., huoni kama hata wao wanatakiwa watuombe radhi kwa kumuweka asiyejulikana.
Soma Tena Mkataba mjomba. Mlisaini mkidhani mtaleta janja janja? Mkataba ufuatwe kama unavyotaka
 
Naskia wabongo waliwavamia kwenye page yao hadi wakafunga comments
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…