DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Nuru Mruma ametoa wito kwa Serikali kupokea maoni ya wananchi kuhusu sakata la Bandari, huku akiitaka ifafanue maeneo yote yanayotiliwa shaka.

Hayo ameyasema leo Alhamis Juni 29, 2023 akihutubia Baraza la Eid El-Adh'haa lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco jijini hapa.
"Pia Serikali inapaswa kutoa elimu kwa wananchi ili waendelee kuuelewa mradi huu (uwekezaji bandari)," amesema.

Mruma amesema kubainika kwa mradi huo kuliibua mjadala na taharuki kwa wananchi ambao hawakuwahi kuwa na taarifa sahihi kuhusu mradi huo.
Mruma ameitaka Serikali kupokea maoni ya wananchi na kutoa ufafanuzi kwenye maeneo yote yanayotiliwa mashaka.
Hiyo ni kauli ya kwanza kutoka Bakwata tangu uanze mjadala baada ya Serikali kusaini mkataba wa awali wa ushirikiano wa uwekezaji na uboreshaji bandari na Serikali ya Dubai kupitia kampuni ya Dubai Port World.

Sikukuu ya Eid El Adh'haa hufanyika kila mwaka na waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimisha Nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ismail kwa amri ya Mwenyezi Mungu, lakini badala yake akaletewa Kondoo. Kuchinjwa kwa Kondoo huyo na Nabii Ibrahim ndiko kulikofanya hadi sasa sikukuu hiyo iitwe kuwa ya kuchinja.

Chanzo: Mwananchi
 
MKATABA WA BANDARI NI WA KIUHAINI,UMEVUNJA KATIBA YA NCHI NA UTAKWENDA KUVUNJA SHERIA ZA NCHI -MWANASHERIA DR NSHALA RUGEMELEZA.

"Mkataba uliosainiwa ni "Binding Agreement" hakuna namna ya kujitoa,kuna propaganda zinasema eti tungoje HGA,this is nonsense,itategemea vipi HGA wakati IGA unasema hauna namna ya kujitoa na ukitaka kujitoa uende katika mahakamani za kimataifa,angalia ibara ya 10,18 na 27 ya mkataba huo ndio utagundua waliosaini mkataba huo walikuwa na dhamira ya kuuza nchi" Mwanasheria Rugemeleza.

Yote yanayofanywa sasa na Serikali ni propaganda kiwaaminisha watu walichofanya ni sahihi,na kilikuwa na nia njema,sasa hatuwezi kuruhusu nia njema kuuza rasilimali zetu-Mwanasheria Rugemeleza.

"Namshukuru Daktari Slaa kwa kulisemea hili,nawashukuru wote waliosimama kuhesabiwa kulisemea jambo hili la kuuzwa kwa rasilimali zetu,nilitegemea Bunge lingeweza kumuwajibisha Rais,kwa maana hakuna aliye juu ya sheria,lakini haikuwa hivyo" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mtu mwenye hulka ya wizi lazima atatuibia,mtu mwenye uwezo mdogo wa akili haiwezekani leo ageuke mwenye busara" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa kwa kuuangalia tu kama hauna majeraha ya akili na akili yako iko sawasawa utagundua ule ni mkataba batili,ule ni mkataba haramu,ule ni mkataba usio weza kutetewa na mkataba wenyewe umejivika madaraka kuwa juu ya sheria ya nchi katika ibara ya 27" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa kwa kuuangalia tu kama hauna majeraha ya akili na akili yako iko sawasawa utagundua ule ni mkataba batili,ule ni mkataba haramu,ule ni mkataba usio weza kutetewa ni mkataba unaovunja katiba yetu ya nchi moja kwa moja na mkataba wenyewe umejivika madaraka kuwa juu ya sheria ya nchi katika ibara ya 27" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa unajiweka juu ya sheria ya nchi, mkataba unajiweka juu ya katiba ya nchi,unagandisha sheria za kodi,halafu niliwasikia watu kama kina Tulia wakifokea fokea watu,mtoto mdogo unafokea fokea watu,nilichogundua hajui sheria za mikataba ya kimataifa" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba utaisha siku shughuli za bandari zitakapokwisha, mkataba hausemi manufaa ya uwekezaji huo,ni lipi andiko limeandika manufaa ya uwekezaji huo na kusema tunamuhitaji mwekezaji huyu, mkataba utatumia sheria za kodi za siku iliyosainiwa,hautalipa tozo,halafu Mbarawa anatueleza mkataba huu una manufaa,ni yapi hayo manufaa ikiwa mkataba utakuwa juu ya sheria zote za nchi yetu?" Mwanasheria Rugemeleza.

"Viongozi matumbo wamefanya maamuzi ya vizazi vijavyo bila kuzingatia usawa,Wajukuu wetu watakuwa wanaiangalia bandari kama wanavyomuangalia Mama Mkwe na wasifanye lolote, Mkataba wa Rio unasema kufanya maamuzi juu ya vizazi vijavyo kwa kuzingatia usawa, Mkataba unasema utaisha siku,Mwenyezi Mungu akisema Dunia imefika mwisho,tutatawaliwa na Dubai hadi siku Dunia ikifika mwisho"Mwanasheria Rugemeleza.

"Viongozi awa ndio tunawapisha barabarani kwenye misafara yao,Rais aliapa kuilinda na kuitetea katiba,je alichofanya ndicho!!?? sicho,amepoteza uhalali wa kuwa Kiongozi wetu" Mwanasheria Rugemeleza

"Kitendo cha bunge kupitisha mkataba ule ni aibu,ni dharau kwa nchi,awa watu wameisaliti nchi yetu,wote waliosaini na kupitisha ule mkataba majina yao yaandikwe msaliti,mhaini,tuwakemee watu awa kwa hasira maana wameisaliti nchi yetu" Mwanasheria Rugemeleza.

"Na kuhusu suala la Katiba Mpya,nashauri tukae tuchague watu wa kwenda kutuandikia katiba yetu lakini sio awa waliopo" Mwanasheria Rugemeleza

"Ibara ya 14 kuhusu fidia (Prompty and adequate compassition) utalipa fidia ya hasara ya Sasa na ya mbeleni iliyopotea inapingana na ibara ya 24(2) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema alipwe fidia inayostahili,inapingana na ibara ya 4 na ibara ya 2 la Umoja wa mataifa ya International investment law inayosemwa alipwe fidia inayostahili,Mimi PhD yangu ni ya International investment law na nimesomea Havard,na Mimi sio Mwanasheria uchwara,huu mkataba umeiuza nchi na kukiuka katiba ya nchi yetu" Mwanasheria Rugemeleza

"Mkataba uliosainiwa ni "Binding Agreement" hakuna namna ya kujitoa,kuna propaganda zinasema eti tungoje HGA,this is nonsense,itategemea vipi HGA wakati IGA unasema hauna namna ya kujitoa na ukitaka kujitoa uende katika mahakamani za kimataifa,angalia ibara ya 10,18 na 30 ya mkataba huo ndio utagundua waliosaini mkataba huo walikuwa na dhamira ya kuuza nchi" Mwanasheria Rugemeleza.

"Spika alikuwa anakuja kwetu kama mwanafunzi wa kujifunza intern kuulizia haya mambo ya International investment law,Leo anajifanya yeye anajua sana,hii ni kejeli,dharau na jeuri,hii inatuonesha sisi Watanzania hatujawafundisha viongozi wetu kutuheshimu,zile kanuni za Tanu wao hawajazisoma,kwa hiyo sisi wanatufanya watwana wao,ndio maana licha ya ibara 27 kusema Tanzania itawajibika kwa Dubai,wao wanakata mayenu wanasema mkataba huu uko sawa sawa"Mwanasheria Rugemeleza.

"Ukiangalia ibara ya 28 uhaini mkubwa umefanyika dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mkataba huu wa bandari na hili nalisema bila kumung'unya maneno haya yamefanywa na Kiongozi namba moja,bunge na wote waliosaini" Mwanasheria Rugemeleza

"Viongozi wetu hawana uhalali wa kuendelea kukaa madarakani,wenzetu waislamu kama umemtendea baya lazima akuoneshe alivyochukia, Watanzania lazima tuoneshe tulivyochukia,hapa lazima tuvue gloves,kama kupigwa basi zipigwe kavu kavu kuonyesha jinsi tulivyochukia" Mwanasheria Rugemeleza.
"Mimi sio mtoto mdogo tena,nimepata miaka yangu yote ya kuishi na nimepata akili nyingi juu ya sheria za nchi na kimataifa,namshukuru Mungu,Sasa siwezi kuruhusu mtoto wangu au mjukuu wangu aishi katika ujinga namna hii,huu ni mkataba haramu,danyanyifu,mkataba wa kuuza nchi, mkataba uliovunja katiba"Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba huu umevuja kwa namna ya ajabu sana,je mikataba mingapi haijavuja na kuna madudu kama,uliposainiwa mkataba huu ilisainiwa mikataba mingine mingi hapo Dubai,kwa hili lililotokea tutawaamini vipi awa viongozi wetu,wamepoteza uhalali wa kuaminiwa na Wananchi"Mwanasheria Rugemeleza.
 
WASOMI WAKISHAANZA KUKOSOA UTAWALA NI HATARI KUBWA:-

Na Thadei Ole Mushi

Wasomi Nguli nchini wameendelea kuongea, wameendelea kukosoa Mkataba wa Bandari, Ukiona wasomi kaliba ya kina Shivji wameanza kutoka Vyumbani mwao na kuja kufanya Press fahamu kuwa wakati umefika wa aidha ukubali kubadilika au ubadilishwe kwa Nguvu.

Ipo hivi

Serikalibyoyote dalili zake za kuobdoka madarakani kwa kutokuchaguliwa kwa Kura au kwa kupinduliwa hupitia vipindi viwili muhimu:-

Normal- Ni hatua ya kwanza ni kuona mambo yapo sawa wakati hayapo sawa. Pamoja na Kelele za wananchi watawala hujiona wapo tu sawa. Mfalme Luise wa XVI na mkewe Marine Antoniete pamoja na kelele za Wafaransa kulalamika maisha magumu na kupinga hali ya matabaka (Nobles na Clerks) ambao walikuwa wakila na kisaza na mfalme, Louise aliwapuuza.

Criticism- Hii ni hatua ya pili ambayo huusisha intelectuals kama hawa kina Shivji na wengineo kuanza kupinga aidha kwa kuandika au kwa kusema waziwazi. Kipindi hiki wasomi huamua kuanika uovu na uchafu wa watawala aidha husaidia sana kuwafungua macho na akili tabaka la wasiosoma ambao ni wengi kwa kila jamii Duniani.

Wakati wa mapinduzi ya mara kwa mara kule ulaya miaka ya 1750's na kuendelea ndicho kipindi walichokibatiza kuwa ni kipindi cha enlightenment. Walijitokeza wasomi waliokuwa wanazungumza waziwazi uovu wa viongozi.

Ukiona kwenye utawala wako hizi hatua zote zinakwenda kwa pamoja jua kuna ualakini mbele. Mapinduzi yote duniani huanza na hizi hatua Mbili muhimu sana.

Kosa kubwa la watawala katika kipindi hiki ni kutumia nguvu kunyamazisha wanaopiga kelele. Matumizi makubwa ya askari hutokea kipindi hiki.

Askari katika kipindi hiki huwa watiifu kweli kwa anayewaagiza ila mbele kidogo hugeuka. Tuliona Tunisia wakigeuka na kuungana na wananchi, tuliona Zimbabwe wakati Mugabe akifurushwa askari wakigeuka na kuungana na wananchi huku wakipiga Selfie pamoja na wananchi, tuliona Misri Mubarak akifukuzwa na wananchi huku askari wakiwa pamoja na wananchi kwenye vifaru vya jeshi nk.

Nini Maoni yangu…..

Ni wakati sasa wa kuachana na Chawa kama hawa kina Kitenge, Zembwela, na wengineo kuisemea Serikali kwenye mambo ya Msingi kama haya ya Bandari. Tanzania imeshabadilika mno na kwa sasa kila mtu anaelewa….

Tanzania kwa Sasa Wasomi ni wengi sana, wapo huko mtaani wengine wanauza Juice, Wengine wanaendesha Boda Boda nk. Katika kipindi taifa linapofikia Level ya kuwa na wasomi wengi kiasi hicho viongozi wanapaswa kusoma mchezo na kuwa wajanja haswa katika kauli zao wanazozitoa, hotuba zao, taarifa zao na namna wanavyoishi nao, nk.

Nafikiri umekuwa ukiona siku za karibuni kuanzia miaka ya 2000 criticism kwa viongozi wetu zikiongezeka, Kiongozi anatoa kauli hazitapita Dk tano Atajibiwa kwa ufasaha na utaalamu uliosheheni na kauli yake inakosa maana kabisa. Hiki ni kipindi kigumu sana kwao haya ndio matokeo na Kiashiria cha kuwa na wasomi wengi nchini.

Niliwahi kusema watanzania aliongoza Nyerere sio alioongoza Mwinyi na alioongoza Mwinyi sio alioongoza Mkapa na watanzania alioongoza Mkapa sio alioongoza Jk na Wa Jk sio wale wa JPM na wa JPM sio hawa wa SSH. Kila mtu anaongoza watu tofauti na mazingira tofauti.

Kipindi Cha Nyerere kulikuwa hakuna matumizi haya ya internet leo ukisema kitu utakumbushwa Kesho kwa vielelezo.

Tanzania imeshaingia age of Enlightenment, age of reasoning ni vizuri viongozi wetu wakalifahamu hilo. Ni kazi kubwa sana kuongoza watu wa aina hiyo inahitaji uwe unaongeza maarifa kila Siku, uwe na uhusiano nao mzuri, uwasikilize na Uwe umezungukwa na watu wenye akili ndio maana huwa nasema Akili kubwa ni Mali ya Rais anapaswa kuzitumia. Badala yake tumeruhusu Rais kuzungukwa na Hizi Chawa lengo lake sijajua ni nn au ndio kumhujumu Mkuu wa Nchi.

UKOMO WA CCM

Ukomo wa Chama changu siuoni mbali, upo karibu sana kwa aina ya vijana tunaowa recruit na kuwaingiza kwenye Chama. Kama kwa Sasa tuna wananchi wanaoweza kufikiri hivi itakuwaje miaka 10 ijayo? Tumewaandaje UVCCM kuja kuchukua kijiti?

Biblia Takatifu inasema katika Mithali 18:12

“Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima.”

Morning naenda kupata Supu ya Masingiri Mahali 😀😀😀

Ole Mushi
0712702602
 
Kwa kuwa zimwi la kampuni ya DPW ni la kudumu kama mkataba waliongia na serikali, nimeona ni busara tukawa na munakasha maalumu kuhusu kampuni hii tata iliyoingia mkataba wa kilaghai na serikali ya CCM kununua bandari zote kwenye bahari na maziwa makuu, anga la nchi, special economic zones, na njia zote za usafiri kwa mkataba wa milele.

View attachment 2672918
Katika munakasha huu, wanaJF wakiwa kama wananchi wenye maslahi na rasilimali za nchi hii, watakuwa wakipeana updates kuhusu kila jambo linaloendelea kuhsu DPW. Hapa ndipo wale wanaopinga mkataba na wale wanaoukubali watakuwa wanakutana na kutoa hoja zao bila wasiwasi. Wapingaji watatakiwa kuleta data zinazoonyesha ubaya wa mkataba na hasara za kuuza nchi. Na wanaoukubali mkataba watakuwa wakisema uzuri wa mkataba na manufaa ambayo nchi itapata kwa kuingia mkataba huu. Hatimaye tutafikia muafaka wa suala hili ijapokuwa tayari mkataba umeishasainiwa na serikali ya CCM.

Kupitia majadiliano haya, wapingaji na wanaokubali mkataba watafikia hatua ya kuelewana bila matusi wala kukaripiana. Ikiwa wanaopinga watakuwa na hoja nzuri zaidi yafaa wanaoukubali mkataba wawasikilize na ikiwa hawakueleweka watatakiwa kuweka data na facts zaidi ili waeleweke. Hali kadhalika, wanaoukubali mkataba watatakiwa kuja na hoja kuntu zitakazowashawishi wapingaji kuelewa. Sio mtu unakuja hapa unasema eti mkataba una manufaa kabla ya kuweka bayana vifungu vyenye manufaa na kuweka wazi manufaa hayo. Na pia wapingaji watatakiwa kusema vifungu vyenye utata na jinsi vitakavyoleta hasara na athari mbaya kwenye nchi.

Nisiwachoshe na maneno mengi. Nimeishaweka wazi dhima ya munakasha huu. Nawaomba moderators muugandishe munakasaha huu ili wachangiaji waweze kuufikia kwa urahisi. Kuwa na munakasha maalumu kutawezesha taarifa zote zinazohusu DPW kuwekwa pamoja ili wananchi, wanasiasa, watafiti na watu wengine wenye nia njema na nchi hii wapate taarifa kwa wakati na kwa haraka zaidi.

Nawasilisha.
Ikae Juu. Asante kwa Ubunifu.
 
"DP WORLD wakipata faida huwezi kuwatoza kodi lakini pia hakuna kifungu chochote (katika mkataba wa bandari) kinachozungumzia revenue sharing (mgawanyo wa mapato), kama nchi itafaidika vipi?" Prof. Shivji

"Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD" Profesa Issa Shivji

"Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji" Prof. IssaShivji

"Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika" Prof. Issa Shivji

"Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa" Prof. Issa Shivji

"Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)" Prof. Issa Shivji

"Imezungumzwa sana kwamba watu wetu wataendelea na ajira zao, wafanyakazi Watanzania watashiriki vipi katika management (usimamizi)?, wafanyakazi wa kawaida (makuli) na HR (Afisa Rasilimali Watu) hawa watakuwa Watanzania lakini wengine wote katika management watatoka Dubai (DP World)" Prof. Issa Shivji

"Mikataba ya miradi (project agreement) na nchi mwenyeji (host government) mikataba hii haitapelekwa bungeni wala haitawekwa hadharani kwa sababu ni siri. Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari ) ulipelekwa bungeni kwasababu ni mkataba wa kimataifa lakini project agreement ni ya kibiashara hivyo ni confidential (siri). Watanzania hawatajua wameingia katika mkataba gani na kuna nini ndani ya mkataba na mkataba umesema nini" Prof. Issa Shivji

"Shughuli zilizotajwa katika awamu ya kwanza (ya mkataba wa bandari) sio za bandari pekee, kuna Special Economic Zone (maeneo mahususi ya kiuchumi), trade corridor, free zone" Prof. Issa Shivji

"Eneo ambalo sio la DP WORLD lakini ni karibu na eneo la DP WORLD, mtu akitaka kujenga barabara au flyover ambayo interfere (itaingilia) shughuli za DP WORLD hairuhusiwi kwa mujibu wa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari). Serikali itahakikisha kwamba shughuli hizo hazitokuwepo kando kando na eneo la DP WORLD" Prof. Issa Shivji

"Kwa mfano serikali ina dhamira au haina dhamira ya kudevelop (kuendeleza) bandari ya Tanga au Mwanza kwa mujibu wa mkataba , DP WORLD wana haki ya kupewa taarifa hizo kabla ya yote ili wakitaka waweze ku-express interest (kuonesha nia)" Prof. Issa Shivji

"Kuna sekta nyeti katika uchumi na huwezi kuweka katika makampuni ya watu binafsi na bandari ni sekta nyeti mojawapo, ni roho na mishipa ya uchumi hivyo huwezi kuweka katika mikono ya watu binafsi kwa sababu mbalimbali" Prof. Issa Shivji

"Mali zetu ikiwemo madini tunazo-export (tunazozisafirisha nje) ma mali tunazozileta zinapitia bandari na mali nyingine ni very sensitive (nyeti sana), huwezi kuweka hiyo mikono mwa kampuni mbinafsi bila wewe kuwa na mamlaka" Prof. Issa Shivji
 
Nisiwachoshe na maneno mengi. Nimeishaweka wazi dhima ya munakasha huu. Nawaomba moderators muugandishe munakasaha huu ili wachangiaji waweze kuufikia kwa urahisi. Kuwa na munakasha maalumu kutawezesha taarifa zote zinazohusu DPW kuwekwa pamoja ili wananchi, wanasiasa, watafiti na watu wengine wenye nia njema na nchi hii wapate taarifa kwa wakati na kwa haraka zaidi.
Ninakupongeza kwa wazo hili zuri, na ni matumaini yangu wahusika huku JF wataweka ushirikiano kwa wazo lako hili zuri

Nami ningependekeza kwamba, 'format' ya mada hii ihusishe uwepo wa nyaraka husika inayozungumzia "Makubaliano" kati ya Tanzania na Dubai; ikiwezekana ziwepo hiyo ya lugha ya kigeni na tafsiri katika lugha yetu.
Chini ya hiyo nyaraka, tunaweza pia kuwa na mtiririko (historia) ya jambo hili lilivyoanza, wahusika na hadi kuyafikisha makubaliano hayo hapa yalipofikia hadi sasa.

Chini ya hilo, pawepo taarifa za serikali ya Tanzania katika kuutetea mkataba huo kati ya Tanzania na Dubaya. Wote waliouuza mkataba huo kwetu; kwa mfano Makame Mbarawa, akina Shomari na wengi wengine serikalini waliokwishauzungumzia mkataba khusu uhitaji wake na faida zake.

Hapo hapo, tusisahau waliyoyafanya wabunge, katika kuupitisha na njia zilizotumika kuupitisha Bungeni

Hatuwezi kutowahusisha wataalam wetu, wanasheria nguli, akina Profesa Shivji, akina Lissu; Dr Ruge, yule wa Havard; Dr Mhogo, na wengi wengine waliowasilisha mawazo yao (nisiwasahau TLS), waliyoyasema kuhusu mkataba huu.

Najua hii inaweza kuwa kazi kidogo kwa wataalam wa JF, lakini ni kazi inayowezekana sana kufanyika.

Baada ya yote hayo, nasi akina yahe tunaonyukana humu humu JF, nasi tutaendelea kupanua mjadala huo.
 
wanaopinga watakuwa na hoja nzuri zaidi yafaa wanaoukubali mkataba wawasikilize na ikiwa hawakueleweka watatakiwa kuweka data na facts zaidi ili waeleweke.
Siuoni muujiza wa kumfanya Faiza Fox akubaliane na lolote kutoka kwa wanaopinga; lakini Hee! hilo ni wazo tu. Kuna wanaopigia chapuo ambao wana akili timamu za kusikia wanayosema wengine.
 
PROFESA SHIVJI APENDEKEZA NINI CHA KUFANYA KUHUSU MKATABA WA KIMANGUNGO WA BANDARI

Alisema yafuatayo:

"Kwa ujumla kwa kuhitimisha, mkataba huu sisi wanasheria tunauita honoracy provitions na tukikubaliana hivyo je kuna njia gani ya kujitoa kwenye mkataba huu? Hii sitorudia kusema kwa sababu the destiny ilikuwa ni bunge kuto ridhia mkataba huu lakini kwa sasa na kwa busara zake bunge limeona mkataba huu unafaa na limesha uridhia.

Njia ya pili imependekezwa na chama cha wanasheria na Mzee Warioba, aliposema kwamba tuurekebishe mkataba huu na tufute vipengele vinavyo lalamikiwa. Je njia hii inawezekana? (haiwezekani!) kwa mkataba huu mshirika wako ni lazima akubali ndipo marekebisho yafanyike.

Kama alivyosema Bwana Richard (mzungumzaji aliyetangulia.) kwamba kama mshirika ananufaika na kifungu hiki hatoweza kukubali kurekebisha. Na hata ukisema anakubali je mkataba huo sasa baada ya kurekebishwa utarudi tena bungeni? kwa sababu huo ulio rekebishwa utakuwa haukupitishwa na Bunge!

Jambo jingine nilisikia kwenye clip kutoka kwa Dr. Slaa akisema kwamba kuna muda wa mwaka mmoja kujitoa akinukuu ibara ya tano ya mkataba huu. Nafikiri amekosea tafsiri ya jinsi alivyosoma mkataba huu, ibara ya 5 inasema tu kwamba kama katika muda wa miezi 12 baada ya kusainiwa kwa mkataba na endapo kama hawajakubaliana kupitia project agreement na negotiation, serikali ya Tanzania itakuwa na uwezo wa kutafuta proporsal sehemu nyingine, haisemi kabisa kujiondoa.

Njia ya tatu ya kuingia mahakamani kama wenasheria wengine walivyofanya hapa kuna matatizo. Kama tunavyojua mahakama zetu zinachukua muda mrefu sana kufanya maamuzi, pale kesi itakapo kuja kusikilizwa muda utakuwa umepita na wahusika watakuwa wamesha saini project agreements, mahakama itashindwa kufanya maamuzi ya haki baada ya muda huo kupita na kwakuwa uamuzi wake kwa kipindi hicho hautakuwa na maana yeyote ndivyo watakavyo sema.

Njia mojawapo sijui kama wenzangu wamefikiria hiyo, kwenda kufile case na kuomba inaction ili kuzuia serikali kusign any proporsal about agreement mpaka pale kesi ya msingi iwe imeamuliwa, inategemea kiasigani wataweza kuwasilisha hoja zao lakini kisheria inawezekana hiyo. Swali ni je, utakapoingia mahakamani utakuwa unachallenge nini? Huwezi ukachallenge mkataba (IGA) bali utakuwa unachallenge azimio la bunge kwamba ni unconstitutional kwasababu limeridhia mkataba ambao ni unconstitutional. Kwahiyo azimio la bunge liwe ni unconstitutional kwa kuridhia mkataba ambao ni unconstitutionala ihope itakuwa vizuri.

Njia nyingine ambayo inawezekana kabisa, Mheshimiwa waziri mkuu amesema watafanya amendment lakini kama nilivyosema haiwezekani. Bunge laweza kupitisha azimio kurevorke azimio lake la kwanza na bunge lina mamlaka sovereignity power ya ku unvoke it's status. Wabunge wanaweza sema baada ya kusikiliza wananchi wetu tumeona kuwa azimio hilo halikuwa sahihi na tunalifuta inawezekana kabisa na kama azimio likifutwa hakuna rectification na kama hakuna rectification mkataba umefutwa, sasa njia hii pekee inawezekana.

Ni kwa kiasigani wananchi wataweza kuwashinikiza wabunge wao kuwalazimisha wakae tena bungeni warevorke azimio hilo na kufunga huo mjadala inategemea na uwamuzi wao wananchi. Kusema kweli bunge haliko chini ya Dubai hata sheria za kimataifa haziwezi kuli zuia ndio maana ya sovereignity of parliament kwa hivyo uamuzi wa Bunge utaheshimiwa.

Jambo la mwisho kama ninavyopenda kusema kuhusu mchakato mzima wa ubinafsishaji. Kila mara ubinafsishaji unahalalishwa kwa kusema kwamba sisi kama serikali hatukuwa na tija katika uendeshaji wa shirika hili, hiki ni kisingizio na kimetumika kubinafsisha mashirika yaliyokuwa yanaleta faida, nani anataka shirika linalotia hasara? Kuna sekta nyeti katika uchumi huwezi kuweka mikononi mwa watu na bandari ni sekta nyeti mojawapo, huwezi kuiweka mikononi mwa watu kwa sababu mbalimbali.

Mali yetu yote tuna export kupitia bandari, madini yetu yote yanapitia bandarini, mali yote tunayoleta kutoka nje yetu na ya wengine inapitia bandari na mali zenyewe ni sensitive. Sasa huwezi kuweka hiyo bandari mikononi mwa private company bila ya wewe kuwa na control na all say power hujui wataforward nini kupitisha ama watafaidika nini na huwezi kuzuia.

Kama kuna tatizo la ufanisi ni bora kuajiri management kutoka nje, ingawa itakuwa chini yetu kama vile Dubai wanavyoajiri watu kutoka nje kwani lazima ubinafsishe? Na hii sio ukodishaji kama watu wanavyosema ni ubinafsishaji kwa sababu unaweka control mikononi mwa private company bila ushindani kinyume na katiba ya nchi.

Kwa upande wangu mi naona kuna sekta nyeti za uchumi ambazo ni lazima zibaki mikononi mwa serikali na bandari ni moja wapo, fedha ni muhimu na nishati ni yatatu. Unaweza kubinafsisha hoteli au maduka lakini sio bandari wala sekta ya fedha, hata ukiruhusu mabenki binafsi lakini ni lazima uwe na commercial bank ya serikali ni lazima." Amesema Prof Shivji kwenye mjadala huo.
 
Huo mkataba wa makubaliano hupo wapi kwenye huu uzi wako?.
Tunajadili nini sasa kama huo mkataba haujauweka?.
 
ASKOFU ATOA ORODHA YA WANAOPASWA KULAUMIWA JUU YA MKATABA WA BANDARI!

Sisi Askofu Mwamakula tutakuwa ni watu wa mwisho kumlaumu Rais Dkt. Samia kutokana Serikali ya Tanzania kuingia mkataba tata wa Bandari na Ufalme wa Dubai. Wanaomharibia Rais Samia ni washauri wanaoshika nafasi za kikatiba serikalini akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu hadi sasa hakuna hata mtu mmoja aliyejiuzuru akipinga mkataba huo.

Biblia inatufundisha kuwa mfalme au mtawala anapofanya makosa, wa kwanza kulaumiwa ni viongozi wa juu walio na madaraka ya kikatiba ya kumshauri mfalme au mtawala huyo. Hii ni kwa sababu wo wote unaotokana na watu ni lazima wawepo watu wa kushauri uongozi huo.

Mfalme Sauli alipotenda jambo la sana wakati wa utawala wake ambalo lingepelekea mauti yake yeye na majemedari wake, hakulaumiwa yeye kama mfalme Sauli. Badala yake, Mfalme Daudi alimlaumu Jenerali Abner, aliyekuwa ni Mkuu wa Majeshi ya Israeli ambaye kikatiba ndiye alikuwa mshauri Mkuu wa Mfalme Sauli (1Samweli 26:1-25).

Ni kwa mantiki hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa Watanzania wote kutoelekeza lawama zao kwa Rais Samia, bali lawama hizo zielekezwe kwa wakuu walio ndani ya Serikali walio na madaraka ya kikatiba ya kumshauri Rais na Serikali yake katika masuala ya sheria, uchumi, diplomasia, siasa, dini na usalama. Washauri wa masuala ya kidini wanaingizwa hapo kwa sababu wao wanajua msimamo wa viongozi wa dini walio wengi lakini wameamua kutokumueleza ukweli Mheshimiwa Rais.

Kundi la pili la watu wa kulaumiwa ni Baraza la Mawaziri, kwa kuwa haiwezekani mkataba huo usipitie katika Baraza la Mawaziri. Kundi la tatu ni Spika, Naibu Spika kwa kuruhusu mkataba huo ujadiliwe kwa kukiuka tamaduni na kanuni za Bunge. Kundi la tatu ni wale Wabunge wote ambao walimpitisha mkataba huo.

Kundi la mwisho lakini lililo la muhimu sana ni CCM ambacho ndicho Chama kinachounda na kuongoza Serikali. CCM itakuja kulaumiwa kwa jambo hili kwa kuwa haikuweza kuisimamia serikali yake ipasavyo na hadi ikaingia mkataba ulio tata ambao haukuzingatia maslahi mapana ya nchi yetu na taifa letu kwa ujumla.

Sisi Askofu Mwamakula, pamoja na kutoa wito huu, tunaweka haya katika kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo hasa wajukuu na vitukuu wetu ili na wao waje wasome kuwa kulikuwepo watu walioonya na kushauri katika zamani zetu sawasawa na Maandiko Matakatifu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
Dar es Salaam; 29 Juni 2023; 13:07 pm.
 
Back
Top Bottom