DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Kwa kuwa zimwi la kampuni ya DPW ni la kudumu kama mkataba walioingia na serikali, nimeona ni busara tukawa na munakasha maalumu kuhusu kampuni hii tata iliyoingia mkataba wa kilaghai na serikali ya CCM kununua bandari zote kwenye bahari na maziwa makuu, anga la nchi, special economic zones, na njia zote za usafiri kwa mkataba wa milele.
Katika munakasha huu, wanaJF wakiwa kama wananchi wenye maslahi na rasilimali za nchi hii, watakuwa wakipeana updates kuhusu kila jambo linaloendelea kuhsu DPW. Hapa ndipo wale wanaopinga mkataba na wale wanaoukubali watakuwa wanakutana na kutoa hoja zao bila wasiwasi. Wapingaji watatakiwa kuleta data zinazoonyesha ubaya wa mkataba na hasara za kuuza nchi. Na wanaoukubali mkataba watakuwa wakisema uzuri wa mkataba na manufaa ambayo nchi itapata kwa kuingia mkataba huu. Hatimaye tutafikia muafaka wa suala hili ijapokuwa tayari mkataba umeishasainiwa na serikali ya CCM.

Kupitia majadiliano haya, wapingaji na wanaokubali mkataba watafikia hatua ya kuelewana bila matusi wala kukaripiana. Ikiwa wanaopinga watakuwa na hoja nzuri zaidi yafaa wanaoukubali mkataba wawasikilize na ikiwa hawakueleweka watatakiwa kuweka data na facts zaidi ili waeleweke. Hali kadhalika, wanaoukubali mkataba watatakiwa kuja na hoja kuntu zitakazowashawishi wapingaji kuelewa. Sio mtu unakuja hapa unasema eti mkataba una manufaa kabla ya kuweka bayana vifungu vyenye manufaa na kuweka wazi manufaa hayo. Na pia wapingaji watatakiwa kusema vifungu vyenye utata na jinsi vitakavyoleta hasara na athari mbaya kwenye nchi.

Nisiwachoshe na maneno mengi. Nimeishaweka wazi dhima ya munakasha huu. Nawaomba moderators muugandishe munakasaha huu ili wachangiaji waweze kuufikia kwa urahisi. Kuwa na munakasha maalumu kutawezesha taarifa zote zinazohusu DPW kuwekwa pamoja ili wananchi, wanasiasa, watafiti na watu wengine wenye nia njema na nchi hii wapate taarifa kwa wakati na kwa haraka zaidi.

Nawasilisha.
 

Attachments

1688036401928.jpeg
 
 
Umefanya Jamba jema sana ili baadaye tuje tufanye rejea ya nani alipatiq na nani alipuyanga.
Tunataka tuweke historia sawa ili hapo mbeleni tusije tukakimbiana mkuu. Nafahamu wanaospoti mkataba huu wa kimangungo mambo yakienda kombo watajitenga na kujidai hawakuwahi kusapoti.
 
Hivi tunadhani Bandari na Rasilimali zetu (Natural) wapi kuna faida?
Zote zina faida mkuu. Lakini nasikia hata mbuga zetu za wanyama wamezigawa kwa waarabu hao hao wa DPW. Inauma sana.
 
Tunataka tuweke historia sawa ili hapo mbeleni tusije tukakimbiana mkuu. Nafahamu wanaospoti mkataba huu wa kimangungo mambo yakienda kombo watajitenga na kujidai hawakuwahi kusapoti.
Mkataba una umangungo upi?
 
Hauna ukomo na umehusisha bandari zote za kwenye bahari na maziwa special economic zones na anga la nchi. Kimsingi tumeuza nchi nzima.
Hauna ukomo kivipi? Kwa mujibu wa yale makubaliano mwekezaji kapewa eneo lipi hadi uulize ukomo?

Kwani pia kuna nwekezaji kapewa bandari yeyote au ziwa lolote au special economic yeyote kwa mujibu wa ule mkataba?
 
Back
Top Bottom