#COVID19 Dr. Anthony Diallo: Corona bado ipo, apendekeza 'Level seat' kwenye daladala na Mask

#COVID19 Dr. Anthony Diallo: Corona bado ipo, apendekeza 'Level seat' kwenye daladala na Mask

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mwandishi: Kwanini unanisalimia hivi(Alimpa mkono, Diallo akampa gonga), wakati fulani tulipita hapa tukawa tunaamini tumeshatoka kwenye Covid. Awamu iliyopita tulikuwa tunasali na kumuomba Mungu, Covid haipo. Bado una wasiwasi na Covid

Dr. Diallo: Covid ipo, jana nilimsikia mkuu wa mkoa akitahadharisha watu lakini pia mimi ningependa warudie hatua ambazo zilitusaidia wakati ule ile ya 'Level; sitting kwenye daladala, ilikuwa vizuri pia kabla hujaingia kwenye basi au kwenye daladala uvae mask. Nadhani hiyo itasaidia, watu sasa hivi wanaonekana kuna wanaojali, wengine wanaonekana wala hawajali

Mazungumzo haya aliyafanya jana na mwandishi Aloyce Nyanda. Dr. Anthony Diallo aliwahi kuwa Mbunge Mwanza vijijini sasa inafahamika Ilemela pia Naibu waziri maji na baadae maliasili. Kwa sasa Diallo ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza.
 
Mbona hakuyasema wakati Yule bwana mkubwa anasema Tanzania hakuna korona!
 
Makalla aje kutoa tamko na hapa, au atasema hapana ili kuchochea biashara kwa wenye daladala, kichwa chake kinawaza biashara tu hakumbuki usumbufu kwa abiria.
 
Back
Top Bottom