Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Ninashangaa sana wanaomkazania na kumpa chepuo mgombea urais wa chama cha mapinduzi mpaka inafika wakati unajaribu kuhoji uwezo wa akili zao.Leo hii Tanzania imefikia hatua CCM hata wakimsimamisha mgombea mwenye changamoto ya akili, kisha mgombea mwenye akili, uwezo na stahiki zote za kuwa rais bora akasimamishwa kupitia CHAUMA au ADC, bado kuna watu watajitoa akili na kuandamana kumuunga mkono mgombea wa CCM.
Siasa zimekuwa za kishabiki zaidi badala ya uhalisia! Jambo ambalo ni hatari kwa nchi, tofauti na nchi za demokrasia ya kweli kama Kenya na Marekani ambapo chama si muhimu kuliko mgombea mwenyewe!
Leo kama nchi ingehitaji kiongozi mwanamke,tukizungumza uwezo na tukiweka uchawa pembeni, Mgombea wa CCM hamfikii hata robo Dr. Asharose migiro au Dr. Mary Nagu kwa kila kitu, uwezo, akili na uongozi bora. Kama isingekuwa uzanzibari na uanamke wake, sidhani kama mgombea wa CCM angekuwepo kwenye rada za uongozi wa nchi hii!
Awamu zote za nyuma hakuna Rais aliyemwona anafaa kuwa hata mkuu wa mkoa? Achilia mbali uwaziri. Leo hii aongoze nchi? Si bure tumeshuhudia awamu mbovu na isiyokubalika kwa watanzania kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania.
Tunapaswa kujadili na kuzingatia uimara wa mgombea husika badala ya chama cha kisiasa