Dr. Bashiru Ally: Huwezi ukaitwa na Chama ukaacha kuitikia wito labda haujipendi

Dr. Bashiru Ally: Huwezi ukaitwa na Chama ukaacha kuitikia wito labda haujipendi

Ng'ombe Aliyekatwa Mkia Machungani Akirudi Zizini Wenzake Watajua Hana Mkia
 
Wameitwa Dom wakaenda Lumumba.. Siku waliyopangiwa hawakwenda bali wakaenda siku waliyotaka... Badala ya kuhojiwa wao ndio wakahoji...!!!

UKISIKIA CCM INA WENYEWE NDIO HAWA SASA

Jr[emoji769]
Na siku ile walipo "itikia wito" Bashiru alionekana amesawajika na kupwaya sana. Alikosa confidence kabisa akabaki kua anajichekesha tu mbele ya Kinana na Makamba. Kasubiri wameondoka huku nyuma ndio anakuna na hizi kauli!!?
 
wanaoitwa hawajipendi ndio wale wanaookotwa kwenye viroba ?
Bashiru amesema maneno ya ovyo kabisa.

Huyo msomi na wasiosoma hata hakuna tofauti.

Ni kitisho, kaongea kama mtu anayetisha wanachama kwamba hawana uhuru.

Sasa kama mtu akisema hataki kuitikia wito, anajiondoa chamani, watamfanya nini?

Watamuua? Watamzushia kesi ya kodi/uhujumu uchumi/ utakatishaji fedha? Watamnyang'anya mashamba? Watamvua uraia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuombe ufafanuzi wa kauli ya 'bwana yule' aliyemwambia bwana yule kuwa sumu haionjwi kwa kulamba labda Kuna uhusiano na ulichouliza
Kwani sio kweli sumu haionjwi? Hayo yana ulinganifu gani na kauli ya Bashiru ya "hajitaki" atakayeacha kuitikia wito was chama?
Kwani wito wa chama ni kitu cha mabavu siku hizi kwamba usipoenda utakiona cha mtema kuni?
Mtauana sana huko kwenu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupotea
kesi za kuzushiwa ie uhujumi uchumi
.............................................................
 
Mimi nadhani sio busara kwa KM kujibu kila kitu, mambo mengine awe ananyamaza tuu na kumuachia Polepole.
P
Sijui kwanini hawa watu hawajifunzi kwenye BUSARA ZA KUKAA KIMYA KUJUBUNKILA KIKTU NI TAFSIRI YA KUTOJUA KILA KITU MAMBO MENGINE TUNAYAACHA JAMII INAPIMA
 
Tuombe ufafanuzi wa kauli ya 'bwana yule' aliyemwambia bwana yule kuwa sumu haionjwi kwa kulamba labda Kuna uhusiano na ulichouliza
Kamuulize Pompeo alikuwa anamainisha Nini aliposema Makonda anaminya demokrasia na kile kilichoitwa "RIGHTS TO LIFE" ukitoka kwa Pompeo uje humu unijibu na mimi maswali yangu haya! Wale askari waliovamia Clouds wakiwa na silaha Nani aliwatuma? Je Magufuli analijua hili swala kuwa Clouds ilivamiwa? Baada ya Nape kutumbuliwa akaitisha press yule aliyemtolea bastola hadharani mchana kweupe alitumwa na nani? Kama huna majibu muulize Pompeo akusaidie.

Pia unaweza kumuuliza swali la kizushi kuwa walinzi wa area D walipokuwa siku Lissu anashambuliwa(eneo linalolindwa masaa 24 kwa artificial security na binadamu) halafu muulize Pompeo amewajibishwa Nani kwa kitendo cha walinzi kutoenda lindo area D kwenye makazi ya viongozi?

HITIMISHO: Ukiangalia aina ya matukio na njia zilizotumika kuanzia CLOUDS mpaka SHAMBULIO LA LISSU unagundua kuwa waliokuwa wanapanga na kutekeleza huu upumbavu Wana uwezo mdogo sana wa kufikili. Gwajima alisema Bashite hajawahi kufaulu mtihani wowote( alifeli darasa la nne,darasa la saba,form two na form four) Yaani hivi Hana chochote anachokuzidi hata wewe mlamba miguu yao tofauti na yale makalio yake na hips kubwa I stand to be corrected in case kama na wewe unamakalio makubwa like Bashite like Sabaya
 
Ukiangalia video - body language ya Kinana na Makamba wakiingia ofisini na jinsi wanavyopokelewa na Mangula na Bashiru, inaeleza mengi sana, inaonesha kama walioitwa kuhojiwa ndio wenye nguvu ya kuhoji na wanapaswa kuhoji wanajiandaa kuhojiwa.

Wahojaji wanaonesha kutojiamini na wanajichekesha na kuonesha urafiki wa kinafiki kwa wahojiwa, ni dhahiri kabisa kwamba wahojaji wanaonesha unyonge na inaonekana kama wamelazimishwa kuwahoji wahojiwa wenye nguvu
 
Wameitwa Dom wakaenda Lumumba.. Siku waliyopangiwa hawakwenda bali wakaenda siku waliyotaka... Badala ya kuhojiwa wao ndio wakahoji...!!!

UKISIKIA CCM INA WENYEWE NDIO HAWA SASA

Jr[emoji769]
Na wameenda kama kamati !!
 
Bashiru ni kama anaanza kupoteza uelewa. Sijui na mamlaka au tulikuwa tunamweka position ambayo siyo yake.
 
"Hakuna Kiongozi ambaye ameitwa na akakataa kuitikia wito uongo, huyo anajipenda au hajipendi?, mambo ya kuitana hayajaanza leo, Watu huitwa wengine hata kufukuzwa tangu enzi za TANU wakati mimi sijazaliwa wala Magufuli hajazaliwa,kuna jipya gani?”-Dkt, Bashiru Ally, Katibu CCM
Anajimwambafai tu ..... awaite Zitto au Lissu tuone kama nao wataitikia!!
 
Tuombe ufafanuzi wa kauli ya 'bwana yule' aliyemwambia bwana yule kuwa sumu haionjwi kwa kulamba labda Kuna uhusiano na ulichouliza
Sometimes muwe mnakiri viongozi wenu wamekengeuka na kutoa kauli ambazo hawajazipima!Adhabu kubwa anayoweza kupata mtu anayekaidi kuitwa na chama ni kufukuzwa uanachama,sasa kama ni hivyo,kinana na Makamba kwa mfano,wana kipi cha kupoteza mpaka wawe hawajipendi?Ingekuwa unaweza kumkamata kwa nguvu na kumsweka jela au kumuadhibu kifo ndio hapo unaweza kusema hajipendi!Hapo Bashiru kateleza,wala msihangaike kutafuta counter balance statements!
 
Kauli hii kama ni kweli imetolewa na Bashiru, Katibu Mkuu wa CCM, inadhihirisha yaliyosemwa kuhusu kugoma kwa hao wazee kwenda kuhojiwa.

Hapa anajibaraguza aonekane wazee iliwabidi waende kwa shurti, kumbe walienda kwa kubembelezwa.

Huyu Bashiru na kisomo chake chote kile anazidi kujionyesha jinsi alivyo na hitilafu katika kukiunganisha kisomo chake hicho na utendaji.

Kwa mfano: anapata wapi ujasiri wa kulinganisha TANU/CCM ya enzi zile na CCM hii ya vituko? Chukulia sababu walizoitiwa hao wazee; anao mfano wa aina yoyote kama huo uliopata kutokea enzi za TANU/CCM ya Mwalimu?

Viongozi wanaodhalilishwa, ili wakajitetee kwa kudhalilishwa kwao?

Bashiru anajiondolea heshima, hata hiyo ndogo iliyosalia.
CCM inawatoa akili wote wanaopita kwenye mlango wake
 
KM CCM ajifunze kuwa na Busara. Ni Mwalimu wangu ila sijapenda kabisa anavyobehave kama KM. Hekima imepotea kabisa. anapayuka na kutoa maneno yasiyo na utashi. Magufuli hatabirki. Kinana alisimamia uteuzi wa mgombe ndani ya CCM. nani alijua Kinana ataaibika hivi? Nenda taratibu Mwalimu wangu dunia pana
 
Back
Top Bottom