Dr. Bashiru Ally: Huwezi ukaitwa na Chama ukaacha kuitikia wito labda haujipendi

Dr. Bashiru Ally: Huwezi ukaitwa na Chama ukaacha kuitikia wito labda haujipendi

Wameitwa Dom wakaenda Lumumba.. Siku waliyopangiwa hawakwenda bali wakaenda siku waliyotaka... Badala ya kuhojiwa wao ndio wakahoji...!!!

UKISIKIA CCM INA WENYEWE NDIO HAWA SASA

Jr[emoji769]
Haya yote tutajua baada ya kupewa kipigo cha mbwa koko mwezi oktoba mwaka huu. Nyie endeleeni kushangilia vitu visivyo na maana badala ya kupigania tume huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga,
Jamaa anaonekana hana busara .... Tatizo, JPM akivutiwa na uongeaji wako basi unapata cheo. Hawa akina Bashiru, Poleple na Kabudi wako hapo walipo kwa ajili ya midomo yako tu.
 
"Hakuna Kiongozi ambaye ameitwa na akakataa kuitikia wito uongo, huyo anajipenda au hajipendi?, mambo ya kuitana hayajaanza leo, Watu huitwa wengine hata kufukuzwa tangu enzi za TANU wakati mimi sijazaliwa wala Magufuli hajazaliwa,kuna jipya gani?”-Dkt, Bashiru Ally, Katibu CCM
Hivi huyu Bashiru hataki tu kukubali yaishe? Tunajua alishafungwa bao la dobo na Kinana na Makamba, sasa hizi kelele za kuonyesha CCM ndio walioshinda ni dalili za kuwa na inferiority complex.
 
Wameitwa Dom wakaenda Lumumba.. Siku waliyopangiwa hawakwenda bali wakaenda siku waliyotaka... Badala ya kuhojiwa wao ndio wakahoji...!!!

UKISIKIA CCM INA WENYEWE NDIO HAWA SASA

Jr[emoji769]

Suggets wamekwenda kwa masharti yao ambayo ni pamoja na kutohojiwa na kamati.
 
Bashiru ni kama anaanza kupoteza uelewa. Sijui na mamlaka au tulikuwa tunamweka position ambayo siyo yake.

Kuwa mwalimu mzuri wa chuo kikuu na uongozi wa kisiasa, hasa siasa za kijima za zama hizi ni mbingu na ardhi. Badhiru alifanya kosa kubwa sana kukubali nafasi ya KM wa ccm kipindi hiki.
 
Hivi huyu Bashiru hataki tu kukubali yaishe? Tunajua alishafungwa bao la dobo na Kinana na Makamba, sasa hizi kelele za kuonyesha CCM ndio walioshinda ni dalili za kuwa na inferiority complex.

Very egocentric! Huwa hawakubali kushindwa. Miezi kadhaa baada ya waraka wa maaskofu waliibuka na agizo la kuyataka makanisa yafute huo waraka na baadhi kutishiwa kufungwa. Kabla ya hapo walimtafuta msomi wa kanisa mojawapo kusaidia kukosoa waraka. Waziri aliyepinga mkakati wa kudhalilisha makanisa hatimaye aliliwa kichwa.
 
Back
Top Bottom