Kama kweli alijua wana shida na akawafanya watumwa basi ashurutiwe tu!
- Kwanza, wamalawi kuingia nchini kinyemela sio jambo geni- Kwa hivyo sidhani kama aliletwa na hao marafiki wakijua fika kama huyo ni mzamiaji.
- Pili, Huyo Judith kavunja sheria...ni jukumu lake kuona ana nyaraka za kuingia nchini na zakufanya kazi!- Kama huyo Mama alijua haya au walizungumza kufanya hivyo basi wote wamevunja sheria mbali mbali.
Hivyo basi kama huyo Waziri ametumia advantage ya Judith kotokuwa na nyaraka za kuwa nchini na kumnyima haya chini...
- mkataba wa kueleweka
- Uhuru wake wa kuabudu siku ya Jumapili
- Masaa ya kazi ni kama yako ama yeye ni hadi utakapo lala ndipo naye awe wa mwisho kulala na wa kuanza kuamka...
Basi Waziri ashutumiwe na akemewe. Inatisha ukiona waziri ana mhamiaji kwake wakati tunajua Mwaziri saa nyingine wanakuwa na nyaraka za siri za taifa-Je kama huyo Judith ni jasusi? enewei!
Majina ambayo yamo humu ni ya wasichana yaani
Tabu, Jamila, Jesca,Eshter mlokole, na Judith mmalawi. Vijana majina yao yakowapi? Wapi hizo data?
Wajitokeze tu au ndio wote wahamiaji? na kama ndio hivyo Uhamiaji uingie kuona kama kuna ringi ya kuleta wahamiaji na kama huyo mama na marafiki zake wa mbezi(sijui mbezi ipi hii)wanahusika?
Kwa kweli sijui anasema nini bungeni lakini kama anasema na kufanya contrary na anayoyafanya au kuongea basi asurutishwe huko bungeni pia!
Haya ni maswali kwa mlengwa... Mhh?
"Je unaweza kusema hapa juu ya haki za watumishi hawa ambao kwa mateso na manyanyaso yakiwemo ya kuwazuia ku practice imani yao kisa wewe ulibadili dini kuwa Muislam basi unatamka wazi wazi kwamba Wakristo si watu na walio watu wa dini hiyo kwako they should stop practising it wakiwa watumishi wako ?"
"Hebu tueleze ya wachache ya hawa ulivyo wanyanyasa na kuwalipa kiasu cha shiling 100,000 tena siku unapo wafukuza ama wanapo amua kuondoka siku ya mwisho maana huwalipi miashahara yao bali una limbikiza na mwisho unawazika?"
Na haya pia...
"Kuna huyu Tabu alitoka Morogoro kakimbia majuzi na malipo yamekuwa ya maajabu.
Jesca kaondoka majuzi kwa kero ya kumzuia kwenda Kanisani na hata kutaja Yesu akiwa katika eneo lako. Umemnyanyasa hadi kutishia kumpeleka polisi ?"
"Kuna Jamila,Esther Mlokole ambaye amepambana na kuwa mtiifu kwako lakini kashindwa kwa manyanyaso ?"
Sasa kuna huyu Judith ambaye ameapa kwamba hata kwenda kanisani na sasa tunangoja kuona utafanya nini . Lakini kwa nini wewe ndugu waziri nawe uingie katika mkumbo wa kunyanyasa watumishi wako wa ndani na hata vijana wote wanakimbia ?Naomba unieleze juu ya Kibali cha Judith .
Nauliza hivi nikiwa na data kibao ambazo nangoja ujibu hoja ama watu wako wakujibie nizimwage ili watanzania wakujue kwamba ni mtu mwenye chuki na hata wafanya kazi wenzio kiasi kwamba unaogopa hata kula chakula ofisini unaogopa kupewa sumu ukidai kwamba wanakuchukia . Jiulize kwa nini wanakuchukia kabla huja anza kuwa mtu wa vituko.[/QUOTE]
Inaonekana wazi una yako pamoja na kwamba kuna yakuangalia...Simu, Data, Vijana wanakosekana humu!