Mbaga Jr
JF-Expert Member
- May 28, 2018
- 29,028
- 69,666
Sio dokta sasaNingelikuwa mimi ni Dokta, ningelisubiri baada ya uchaguzi ndio niandike haya. Ningelikuwa Dokta lakini!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio dokta sasaNingelikuwa mimi ni Dokta, ningelisubiri baada ya uchaguzi ndio niandike haya. Ningelikuwa Dokta lakini!
Pumbavu aliyekuleta dunianiN
NINYI NDIO MIJOKA MIJINGA MNAFIKIRI MTAMUUA KIRAHISI TENA? MUNGU AMESHAMLINDA NA MMESHASHINDWA WAPUMBAFU NYIE
KABISA MBOWE AMEWASALITI WANACHADEMA NA KUGEUZA CHAMA KAMA NI CHA FAMILIA YAKE.Acha kisombwe kitajengwa upya kuliko msaliti. Acha kife kwani kitakachodumu ni milima
Jibu hilo tayari, uliza swaliUnamaanisha ni mchuchu wa dj?
Naamini unaelewa Kiswahili.Sio dokta sasa
Sasa basi kwa umri huo ulipaswa kuwa mtulivu zaidi kifikra. Inaonekana upo impulsive sana au huwa unafikiri kwa mtindo wa one way traffic.Ngoja nikupe taarifa kidogo
Nilimaliza UDSM Bsc 1983, MSc...1990................nikafanya kazi kooooooooooooooote unakoweza kufikiria. sasa nipo nyumbani nakula kapensheni kaduchu 😀 😀 😀 ..... (nitacheki miaka vema)
Hivyo you can guess my age... siajiliwi kokote at this age, ila bado niko very energetic, quite energetic na vimiradi vyangu vya kunifanya niweze kukaa kwenye desktop kuwasiliana nawe hapa JF!
Have a nice Sunday
aliondoka zito na chadema ikaimarika mara 10 sembuse mwehu.MAJARIBIO YOTE YA KUTAKA TUNDU LISSU AONEKANE MSALITI NDANI YA CHADEMA YAMESHINDWA VIBAYA SANA.
WATANZANIA NA WANACHADEMA WAMEKATAA NA MBINU HII IMESHAFELI VIBAYA SANA.
Je! UPEPO WA LISSU UTAPITA KAMA WALIVYOPITA WENGINE?
KUELEKEA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA CHADEMA - TAIFA
Sehemu III
"Kila kizazi kinapaswa kuwa na dhamira yake ya kutimiza au kuisaliti, katika hali ya uwazi kabisa" Fratz Fannon
Oktoba 1993 alifariki mtu aliyeitwa Rajab Omar Mbano Kakolwa, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini kwa tiketi ya CCM. Hii ilimaanisha kungekuwa na uchaguzi mdogo kwa ajili ya kujaza nafasi iliyoachwa wazi. Mapema mwaka uliofuata, 1994 uchaguzi mdogo uliwakutanisha miamba minne ya siasa za Kigoma; Azim Premji wa CCM, Kashugu Anzaruni wa TADEA, Hussein Beji wa NCCR na Dr. Amani Walid Kaborou wa CHADEMA. Matokeo ya uchaguzi huo yalimpa ushindi Azim Dewji wa CCM kwa kupata kura 9453 akifuatiwa na Dr. Amani Walid Kaborou wa CHADEMA kwa kura 5325.
Hatahivyo Dr. Kaborou alipinga matokeo hayo mahakamani kwa hoja 14, zikiwemo hoja za mgombea wa CCM kusaidiwa na serikali ya Rais Mwinyi kwa kupewa usafiri wa serikali, upendeleo kupitia redio ya serikali (enzi hizo Radio Tanzania Dar es Salaam au RTD) kwa Azim Dewji, na kutumia fedha nyingi kinyume na sheria za uchaguzi. Agosti 1994, mahakama kuu ilifuta matokeo ya uchaguzi na kuacha tena jimbo la Kigoma likiwa wazi. Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali ilikata rufaa na kupeleka kesi hiyo Mahakama ya Rufa, lakini kufikia Desemba 1994 tume ya uchaguzi ilitangaza kutokuwa na uchaguzi tena katika jimbo hilo hadi Uchaguzi Mkuu wa 1995.
Dr. Amani Kaborou, mkufunzi wa Historia aliyekuwa akifundisha huko Marekani, na baadaye kurudi Kigoma kujiunga na siasa za upinzani mapema kabisa baada ya kukubalika kwa mfumo wa vyama vingi, alitumia muda uliobaki kuikuza CHADEMA katika mkoa wa Kigoma. Katika uchaguzi mkuu wa 1995, Dr. Kaborou alimshinda Azim Premji wa CCM na kuwa mmoja kati ya wabunge wanne wa CHADEMA wa bunge la kwanza la vyama vingi Tanzania. Hata hivyo ubunge wake huo ulipingwa mahakamani na Azim Premji na kisha Dr. Kaborou akapoteza katika uchaguzi wa marudiano. Lakini mwaka 2000 aligombea tena na kushinda. Aliwahi kuwa kiongozi wa upinzani bungeni kwa muda mfupi kabla ya kumuachia Dr, Wilbroad Slaa, naye wa CHADEMA mwaka 2003.
Mwaka 2005 akiwa Katibu Mkuu wa Chama - Taifa, Dr. Kaborou alipoteza ubunge kwenye uchaguzi mkuu. Na baada ya minyukano ndani ya CHADEMA, aliamua kuhamia CCM mwaka 2006 na punde akachaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Huyu ni mtu aliyependwa sana pale Kigoma na katika siasa za upinzani. Alikuwa msomi, anayeijua dunia, aliyezungumza kwa ushawishi. Aliwahi kubebwa juujuu na mashabiki wake kutoka stesheni ya reli Kigoma hadi Ujiji, umbali wa Km 8.
Ukiacha Dr. Amani Walid Kaborou, kuna Dr. Wilbroad Slaa ambaye sitakuwa na haja ya kumuelezea hapa kwani nguvu yake akiwa CHADEMA inajulikana. Lakini tunakubaliana jambo moja, kwamba kugombea Urais kwa Dr. Slaa mwaka 2010 kulikuwa sababu ya CHADEMA kupata ushindi katika majimbo mengi mwaka huo. Ni kama kugombea kwa Lowasa mwaka 2015 kulivyosaidia CHADEMA kushinda viti vingi vya wabunge na udiwani na hata kuongoza halmashauri za majiji makubwa (Dsm, Arusha, Mwanza, Mbeya) na hata manispaa kubwa kama Iringa na Moshi. Naam upepo wa Dr. Kaborou ulipita, upepo wa Dr. Slaa ulipita, upepo wa Lowasa ulipita, Je! Upepo wa Lissu utapita? Utapitaje?
Kuna watu wengi waliokuwa wakitazamwa kama mashujaa wakiwa CHADEMA lakini walipoondoka wamepuuzwa. Hawa walitazamwa kama wasaliti, waroho wa madaraka na pesa, watu wasio na misimamo, mamluki na majina yanayofanana na hayo. Je! Lissu naye anafanana na majina hayo?
Kama kuna kosa kubwa CHADEMA itafanya ni kumtazama Lissu kama hao ndugu wengine hapo juu. Nimezungumza na marafiki wengi ndani ya Chama na kuonya kuwa wakati huu ni wakati tofauti. Kinachomtofautisha Lissu na hao wengine sio ushawishi alionao, naam Lowasa alikuwa na ushawishi mkubwa zaidi, na hata Slaa alikuwa na ushawishi mkubwa zaidi kwa jamii kuliko Lissu (hili naweza kulitetea zaidi baadae). Kinachomtofautisha Lissu na hao wengine ni NYAKATI.
Naam, wakati Dr. Kaborou anahama chama mwaka 2006, mwenyekiti Mbowe alikuwa na miaka 2 tu kama mwenyekiti wa chama. Wakati Chacha Wangwe akipinga yanayoendelea ndani ya Chama mwaka 2008, mwenyekiti Mbowe alikiwa na miaka minne tu kama mwenyekiti. Na zaidi mwaka 2010 chama kilifanya vema zaidi kwahiyo, ya kale yakawa hayanuki.
Kati ya mwaka 2010 hadi 2015 chama kiliendelea kukua mara nyingi zaidi ingawa kulikuwa na migogoro ya hapa na pale (ni kawaida kwa taasiso zote za kisiasa) iliyopelekea kuondoka kwa Zitto Kabwe, David Kafulila, Kitila Mkumbo na wengine. Ujio wa Lowassa mwaka 2015 ulimuondoa Dr. Slaa, na hapo akabadilishwa jina na kuwa msaliti. Mafanikio makubwa ya Chama yaliyopatikana mwaka 2015 yalitusahaulisha zaidi kuhusu Dr. Slaa, na upepo wake ukawa umepita.
Je! Upepo wa Lissu nao utapita? Utapitaje?
Kwa mara ya kwanza mtu aliyeonekana kutibua hali ya hewa ndani ya Chadema anaungwa mkono na kundi kubwa la watu wenye ushawishi kwenye jamii. Watu wengi waliowatazama akina Slaa, Zitto nk wasaliti hawamtazami Lissu kama msaliti wa Chama. Na hii sio kwa sababu ya nguvu ya Lissu, no, ni kwa sababu ya mazingira yaliyopo katika siasa za leo ndani ya nchi yetu. Vituko vya CCM vya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, na uchaguzi mkuu wa 2020 ambavyo vimerudiwa tena 2024, na vinaweza kurudiwa tena 2025 vimerudisha sana morali ya wanambadiliko na kuitazama Chadema kama chama kisicho na uwezo wa kukabiliana na vituko hivyo. Chama kilichokuwa na wabunge 116, sasa kina mbunge mmoja (wa kupewa). Ingawa inajulikana fika kwamba haya ni matokeo ya 'UPUMBAVU' wa dola la Tanzania chini ya CCM, lakini pia inawapa sababu ya watu kutamani mabadiliko katika siasa za upinzani. Wapo watu wengi wanaomini Chadema haijaweza kujitetea vya kutosha dhidi ya 'UPUMBAVU WA DOLA LA TANZANIA CHINI YA CCM'. Katika mazingira hayo, Lissu ambaye anaonekana kuwa mtu wa siasa kali (radical) anaweza kuongoza jaribio la kuikabili dola la wazandiki la CCM. Sambamba na hilo, wapo wanaoamini uongozi wa Chadema uliopo umeshindwa kujabiliama na wazandiki wa CCM; Watekaji, Watesaji, Wauaji na Waharibifu wa demokrasia. Wapo pia wanaoamini baadhi ya viongozi wa Chadema wanakula CCM na kulala Chadema. Hayo yanamfanya Lissu kuwa mtu wa tofauti na wengine walionekana 'kutifuana' na Uongozi wa Chadema huko nyuma.
Naam, jaribio la kumpa Lissu jina la usaliti lilishindwa mapema baada ya ofisa wa karibu wa Mwenyekiti Mbowe, Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kufananisha kitendo cha Lissu kuchukua fomu ya uwenyekiti na uhaini, na kuahidi kumshughukia. Jaribio lingine ni lile la Yericko Nyerere la kutaka kuharibu taswira ya Lissu kwa kuandika makala ndefu yenye mambo mengi kuelezea sababu za kwanini Lissu hafai kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Majaribio hayo mawili yamekutana na upinzani mkali, si kutoka CCM, bali ndani ya Chama na hata kwa watu wa nje ya chama ambao mara nyingi wameiunga mkono Chadema. Ni upepo tofauti.
Hitimisho!
Pamoja na kwamba hakuna ushahidi wowote wa kisayansi kwamba Lissu anaweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya Chadema, lakini kuna idadi kubwa ya watu - hasa wanachama wa chini wanaomuunga mkono. Na hapa niseme, watu hawa si kwamba wanamtaka zaidi Lissu la! Ni kwamba wamepoteza tumaini na hali ilivyo sasa.
Upepo wa Lissu ni tofauti na upepo wa kina Dr. Slaa. Ni upepo ambao kama utapita hautapita na Lissu peke yake, ni upepo unaoweza kukisomba na kusambaratisha chama.
Hekima ya viongozi wa Chadema waliopo madarakani, ambao wengi wao hawamuungi mkono Lissu, ndio inayoweza kukiokoa Chama au kukiacha kisombwe na upepo wa Lissu.
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.
LISSU – FEDHA ZA ABDUL – WENJE; UKWELI KIDOGO, UONGO MWINGIKABISA MBOWE AMEWASALITI WANACHADEMA NA KUGEUZA CHAMA KAMA NI CHA FAMILIA YAKE.
Binafsi nataka kura zikampe hiyo busara. Watakao laumiwa ni wajumbe kwa wale wanaotamani mbowe apumzike.Mbowe atumie busara watu wamemchoka
Wajumbe 75% ni chawa wa MboweBinafsi nataka kura zikampe hiyo busara. Watakao laumiwa ni wajumbe kwa wale wanaotamani mbowe apumzike.
Tuope demokrasia nafasi tushuhudie ukubwa wa cdm.
Basi mapinduzi yafanyike inaonekana demokrasia haitafua dafu dhidi ya mwamba 😂😂.Wajumbe 75% ni chawa wa Mbowe
Mbowe alijipanga mapema sababu hii nafasi anaitakaBasi mapinduzi yafanyike inaonekana demokrasia haitafua dafu dhidi ya mwamba 😂😂.
SielewiNaamini unaelewa Kiswahili.
Uenyekiti sio sehemu ya majaribio, binafsi natamani Lissu akabiliane na Mbowe kidemokrasia na hata akishindwa abakie hapo naye ajipange kwa uchaguzi unaofuata. Hizi mambo za kulala na kuamka unaitaka nafasi bila ya kuwa na maandalzi haina afya. Unaweza kuwa unapelekwa pelekwa tu.Mbowe alijipanga mapema sababu hii nafasi anaitaka
Mlipofikia it's either Lisu for a chairperson position or keep your party for yourselves, naona vitu ambavyo ni obvious kabisa mnakaa kuzungukazunguka tu. Mbowe amefanya sehemu yake, nyakati hizi na mtindo wa siasa na matukio yanayoendelea hawezi. Keep that Mbowe man in a shelf and let you watch the party moving.LISSU – FEDHA ZA ABDUL – WENJE; UKWELI KIDOGO, UONGO MWINGI
TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tanzania Bara, alishusha tuhuma kuhusu mtu anayeitwa Abdul, mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwenda nyumbani kwake kumhonga.
Alizungumza kwa mara ya kwanza Iringa Mei 2024 kwenye mkutano wa hadhara. Aliendelea kurejea maneno hayo katika mikutano mingine. Nchi nzima inajua kuwa Lissu alifuatwa kuhongwa fedha na Abdul, akakataa.
Ambacho hakijawahi kusemwa ni kuwa hongo ambayo alitakiwa kupewa lengo lilikuwa nini. Lissu, alishusha tuhuma hizo kipindi ambacho maneno kuwa viongozi wa Chadema “wamelambishwa asali”, yamechukuwa nafasi tangu chama hicho kilipofanya maridhiano ya kisiasa na CCM mwaka 2022.
Mtuhumiwa mkuu wa kulamba asali ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Januari 21, 2023, Mbowe akiwa kwenye mkutano wa hadhara, viwanja vya Furahisha, Mwanza, alitetea maridhiano na kueleza kuwa kuna wenzao ndani ya chama hawaungi mkono.
Yupo mtu angeweza kuunganisha alama na kupata majibu kuwa Lissu aliposema alifuatwa na Abdul kuhongwa, akakataa, alitaka kufikisha ujumbe kuwa yeye siyo kama wengine wanaohongeka. Hafanani na “walamba asali”. Ukifika hapo, jina la Mbowe halipo mbali.
Kilichomponza Mbowe ni kuunga mkono maridhiano. Akayavaa kama beji ya heshima. Maridhiano yalifungua milango na madirisha, hivyo kuruhusu hewa mpya kuingia. Kesi za kisiasa zote zilifutwa, mikutano ya hadhara ilifunguliwa, waliokuwa wamekimbia nchi, walirejea. Unawezaje kumsimanga?
Wengi wanasahau. Mbowe alikaa jela miezi saba, kabla ya kuachiwa, hivyo kufungua milango ya maridhiano. Mbowe, alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya ugaidi. Alikamatwa Julai 21, 2021 na kuachiwa huru Machi 4, 2022. Je, alilamba asali ili aachiwe huru na kuunga mkono maridhiano?
Nani hakumbuki? Maridhiano yalifanyika wakati wa uongozi wa Rais Samia. Kabla yake, Ikulu alikuwepo Dk John Magufuli, ambaye hakutaka kutazamana na wapinzani wake wa kisiasa kwa tabasamu. Kesi nyingi za kisiasa, mazingira ya kufanya siasa yalifunikwa na giza, wanasiasa walikimbia nchi. Nani wa kubeza maridhiano?
Turejee kwenye fedha za Abdul. Lissu alisema kulikuwa na jaribio la kumhonga. Yupo mtu hakumtaja, ama alimweka kiporo au alimhifadhi kwa sababu zake. Mbio za uenyekiti Chadema zikafanya Lissu amtaje. Ni Ezekia Wenje, Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Ziwa.
Nilimsikia Lissu akisema: “Aliyemleta Abdul nyumbani kwangu aje kunihonga, ametangaza kugombea umakamu mwenyekiti na amesema kwa maneno yake mwenyewe anaamuunga mkono Mwenyekiti (Mbowe).” Mtajwa ni Wenje.
Neno “afterthought”, hutumiwa sana na wanasheria kwenye mijadala ya kisheria. Lissu ni mwanasheria. Ni kwa nini siku zote Lissu alilihifadhi jina la Wenje? Je, alikaa nalo kama kifungo ili Wenje asiende kinyume naye? Walikuwa na makubaliano ambayo Wenje ameyakiuka? Hakuwa na mpango wa kumtaja ila amekasirika kuona Wenje anamuunga mkono Mbowe dhidi ya yake?
Hutakuwa mbali na ukweli endapo utasema Lissu kumtaja Wenje ni afterthought, yaani fikra zilizofuata baada ya kuona anamuunga mkono Mbowe, ambaye anashindana naye katika mbio za uenyekiti wa Chadema. Yupo anayeamini leo kuwa Wenje na Lissu wana mengi, wakibanwa, wataeleza.
Nilimsikia Wenje akijibu tuhuma dhidi yake. Kwanza hakukataa, isipokuwa amefafanua ukweli upande wake ambao anadai unapindishwa na Lissu. Ukimsikiliza Wenje, unapata jibu moja; hakukuwa na kuhongwa. Habari ya hongo ni tungo nje ya uhalisia.
Wenje anasema kuwa alikutana na Abdul kama bahati kwenye shughuli moja, na baada ya utambulisho, moja kwa moja alimhoji: “Kwa nini Serikali ya mama yako haitaki kumlipa Lissu fedha zake za matibabu?” Lissu alishambuliwa kwa risasi nyingi Septemba 7, 2017.
Ni tukio baya kwa kipimo chochote. Ajabu, uliibuka mvutano wa fedha za matibabu ya Lissu. Sera ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), inaelekeza rufaa ya matibabu kwenda nje ya nchi kutolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili. Lissu alishambuliwa kwa risasi Dodoma, akapelekwa Hospitali ya Mkoa ya Dodoma. Kisha, akasafirishwa kwa ndege ya kukodi hadi Hospitali ya Aga Khan, Nairobi, Kenya. Hakupita Muhimbili.
Sababu za kutompitishia Lissu Muhimbili zilikuwa zinajitosheleza kabisa. Alishambuliwa, waliomshambulia hawakuwa wamepatikana. Nadharia zilikuwa nyingi. Hofu kuwa waliotaka kumuua wangeweza kumfuata Muhimbili, ndiyo ilisababisha apelekwe Nairobi.
Msimamo wa Serikali haukubadilika. Kwa kutambua kuwa Lissu alihitaji matibabu na hakuwa na bima, iliitishwa michango nchi nzima hadi diaspora. Mwitikio ulikuwa mkubwa. Tatizo ni moja, ulikosekana uwazi wa michango ya matibabu ya Lissu. Ukiacha Sh200 milioni zilizotangazwa na Mbowe Septemba 23, 2017, hakuna taarifa nyingine.
Zaidi, Watanzania hawakuwahi kuambiwa kama fedha walizochanga, zilitosha kugharamia matibabu ya Lissu au kinyume chake. Hivyo, inaleta ukakasi kuona Serikali bado inadaiwa fedha za matibabu ya Lissu. Je, tafsiri ya ile michango ni ipi? Lissu anataka apewe fedha za matibabu ambayo ameshalipiwa na Watanzania? Zingatia, hata Serikali ikilipa ni fedha za Watanzania.
Tusiondoke kwa Wenje; kwa nini alianzisha mada ya fedha za matibabu ya Lissu baada ya kutambulishwa kwa Abdul? Je, Lissu amewahi kumtuma au alijituma mwenyewe? Nilimsikia Wenje akisema fedha za matibabu ya Lissu zinamhusu kwa sababu naye kuna za kwake. Lissu alichangiwa, ina maana Wenje anataka kurudishiwa fedha alizomchangia Lissu kwa ajili ya matibabu?
Wenje anasema Abdul ni muungwana sana, maana alikubali kuongozana naye mpaka Tegeta, nyumbani kwa Lissu. Naunga mkono. Abdul ni muungwana, maana alipaswa kushangaa suala la matibabu ya Lissu kupelekewa yeye ambaye siyo waziri wa afya, katibu mkuu wa wizara hiyo wala mkurugenzi mkuu wa NHIF.
Mtu mmoja Kariakoo kwenye kijiwe cha kahawa, alisema: “Nashindwa nimwamini yupi, Lissu au Wenje?” Jibu langu ni kuwa mkweli ni yule anayezungumza taarifa na siyo fumbo. Wenje, ama kwa ukweli au kumsingizia Lissu, alichokizungumza ni taarifa (statement). Lissu, hoja yake ilikaa kwenye mabano. Ilihitaji kufumbuliwa. Ndiyo maana anavyofumbua inabeba tafsiri ya afterthought.
Swali la jumla ni je, nani anamsingizia mwenzake? Lissu kaamua kumsingizia Wenje kwa sababu ametofautiana naye katika uchaguzi ndani ya chama? Hata hivyo tuhuma za jaribio la kuhongwa alizitoa kabla ya moto wa uchaguzi ndani ya Chadema. Wenje amechagua kumkaanga Lissu ili kujinasua na kashfa? Wazungu husema “time heals all boo-boos” – “muda hutibu majeraha yote.” Tuwape muda.
Nilitazama mahojiano ya Lissu kwenye kituo cha Star TV. Nilimwona na nikamsikia Lissu akisema alifuatwa na “mwana malkia”, huyo “mwana malkia”, aliahidi kumsaidia kupata fedha za matibabu. Lissu akasema: “Nilimwambia yule mwana-malkia, ukinisaidia kupata hizi fedha utakuwa rafiki yangu.”
Rejea mkutano wa hadhara, Singida Juni 8, 2024, Lissu alisema: “Namfahamu mtoto wake mmoja anaitwa Abdul. Aliniletea rushwa nyumbani kwangu, nikamwambia shenzi. Kahonge wanaohongeka.”
Upande mmoja, Lissu anasema, alimwambia Abdul kuwa angemsaidia kupata fedha za matibabu, wangekuwa marafiki. Upande mwingine, Lissu anasema, alimfukuza, akamwambia ‘shenzi’. Lissu yupi mkweli?
Katika mahojiano Star TV, Lissu alisema “watu wema” ndiyo walimpeleka Abdul nyumbani kwake. Alikataa kuwataja hao watu wema. Baada ya Wenje kutangaza kumuunga mkono Mbowe, Lissu hakungoja kuulizwa, alimtaja moja kwa moja.
Kuna mwana-Chadema kutoka Magu, Mwanza, aliniandikia ujumbe unaosema: “Nahisi Lissu na Wenje walikuwa na makubaliano yao, wamegeukana, sasa wanatajana. Upo ukweli zaidi wa kuuchimba ndani ya vifua vyao. Wanachikitoa sasa kina uongo mwingi kuliko ukweli kwa sababu wanakomoana.”
punguani hutoa hoja haziko na mashiko.
kama ni cha familia una maana watakaompigia kura ni mwehu kama mwehu wenu lisu
Lisu ni mzoefu sn lakini pia tunataka mtu ambaye CCM hawatalalaUenyekiti sio sehemu ya majaribio, binafsi natamani Lissu akabiliane na Mbowe kidemokrasia na hata akishindwa abakie hapo naye ajipange kwa uchaguzi unaofuata. Hizi mambo za kulala na kuamka unaitaka nafasi bila ya kuwa na maandalzi haina afya. Unaweza kuwa unapelekwa pelekwa tu.
Lisssu ni mashine nyingine kabisa haina wa kuilinganishiaPamoja na kwamba hakuna ushahidi wowote wa kisayansi kwamba Lissu anaweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya Chadema, lakini kuna idadi kubwa ya watu - hasa wanachama wa chini wanaomuunga mkono. Na hapa niseme, watu hawa si kwamba wanamtaka zaidi Lissu la! Ni kwamba wamepoteza tumaini na hali ilivyo sasa.