DR Congo: Mamia waandamana Kishansa kupinga mapendekezo ya Katiba mpya kuongeza muhula wa Rais kuongoza

DR Congo: Mamia waandamana Kishansa kupinga mapendekezo ya Katiba mpya kuongeza muhula wa Rais kuongoza

Maandamano hayo yaliandaliwa na muungano wa Upinzani C64, ambao unamtaka Rais Félix Tshisekedi kuachana na mapendekezo hayo ya mabadiliko ya Katiba yanayoweza kufungua njia ya yeye kugombea muhula wa tatu
Mwafrika ni mwafrika Tu, Felix amekulia Ubelgiji alipokimbilia kama mkimbizi kwa sababu za Political suppression na yeye anafanya Yale Yale ya akina Mobutu na kabila
 
Huenda kipindi cha ukoloni kilikuwa ni kipindi bora kuliko nyakati hizi. Wakoloni weusi ni wabaya kipita wakoloni weupe.
 
DR Congo itapata kutulia na kupata maendeleo ikiwa tuu watampa nchi mtu mwenye akili timamu. Na mtu huyo ni Katumbi Chapwe.

Sijui kwa nini hiki kitu wacongoman hawakipigii kelele, huyu jamaa nakumbuka akiwa gavana wa Katanga vitu vingi na maendeleo ya hilo jimbo viliibuka na hata sasa usalama wa jimbo hilo umekuwa ukisuasua.

Naamini ipo siku hii nchi itakuwa chini yake japo kuna kesi walimfungulia kipindi fulani.
 
Sijui Kwanini hatuwezi kupokezana madaraka kwa adabu baadhi ya nchi Africa. Lazima tusumbuane linapokuja suala la kupeana nafasi za uraisi.
Hata Samia alijitwalia urais kwa damu za maandamano na atalazimishwa kutoka kwa maandamano. Hivi hivi huyu hatoki. Na mijinga ya kina Mwigulu inavyompigia magoti ndo kabisaa
 
Sijui Kwanini hatuwezi kupokezana madaraka kwa adabu baadhi ya nchi Africa. Lazima tusumbuane linapokuja suala la kupeana nafasi za uraisi.
Ubinafsi huo Mkuu..

Kipindi cha Uchaguzi hapa Africa ndio Kila ukatili hufanyika hasa mauaji ya Raia wema au washindani wa kisiasa.
 
Mamia ya waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kinshasa, kupinga pendekezo la serikali la kufanya marekebisho ya Katiba ambayo yanaweza kumruhusu Rais Félix Tshisekedi, aliyechaguliwa mwaka 2019 na kuchaguliwa tena mwaka 2023, kugombea muhula wa tatu endapo marekebisho hayo yatapitishwa kupitia kura ya maoni.

Takriban watu 10 wamekamatwa kufuatia maandamano hayo yaliyofanyika Septemba 15, 2026 jijini Kinshasa pamoja na Lubumbashi, hata baada ya zuio kutoka kwa mamlaka.

Maandamano hayo yaliandaliwa na muungano wa Upinzani C64, ambao unamtaka Rais Félix Tshisekedi kuachana na mapendekezo hayo ya mabadiliko ya Katiba yanayoweza kufungua njia ya yeye kugombea muhula wa tatu.

Ingawa uchaguzi ujao unatarajiwa kufanyika 2028, tayari kuna mvutano mkubwa kati ya serikali na wapinzani wake, baada ya bunge linalotawaliwa na chama cha serikali kuidhinisha pendekezo la kuongeza muda wa madaraka ya Rais.

Soma Bunge la Seneti Congo Lapitisha Muswada Unaoweza Kumpa Rais Muhula Mpya

Mamlaka zilisitisha maandamano yaliyofanyika Kinshasa mwezi Julai kupinga marekebisho hayo ya Katiba, huku baadhi ya wafuasi wa upinzani wakijeruhiwa katika mapigano. Umoja wa Mataifa ulisema angalau mtu mmoja aliuawa katika vurugu hizo. Katikati ya Julai 2026, Serikali pia ilitangaza kuandaa mazungumzo ya kitaifa ambayo yamekuwa yakidaiwa

Soma CONGO DRC: Rais Tshisekedi aita Mazungumzo ya Kitaifa kutuliza mivutano ya kisiasa, M23 wawekwa kando

Hata hivyo, kufuatia Katiba ya sasa ya Congo inamruhusu rais kuhudumu kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja ambapo Rais Tshisekedi alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na kuchaguliwa tena mwaka 2023 na Muhula wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.



=================

Hundreds of protestors gathered in the Democratic Republic of Congo's capital, Kinshasa, to voice their opposition to a government-proposed constitutional amendment that could allow President Felix Tshisekedi -- elected in 2019, then re-elected in 2023 -- to stand for a third term following a referendum.

Organised by the C64 coalition, the opposition is calling on President Felix Tshisekedi to "give up" proposed constitutional changes that could open the way for him to secure a third term.

Elections are two years away but tensions are already high between the government and its opponents since the ruling-party-majority parliament approved a proposal to extend the presidential mandate.

Authorities suppressed a July rally in Kinshasa against the constitutional amendment and several opposition supporters were injured in clashes in which the UN said at least one person was killed.

In mid-July, Kinshasa also announced the organisation of a national dialogue long demanded by the opposition, without specifying its terms.

The proposed constitutional change comes as much of the country is riven by conflict, particularly to the east, where the Rwanda-backed M23 armed group seized swathes of territory last year.

Source: African news, Reuters & Anadolu Ajansi
Hawa mazafakas wa nchi zetu za Kiafrika sijui wamerogwa na nani. Kwenye siasa hakunaga overtime. Muda wako wa kazi ukiisha, you must check out. Any work-in-progress becomes the responsibility of the next elected official.
 
Sijui kwa nini hiki kitu wacongoman hawakipigii kelele, huyu jamaa nakumbuka akiwa gavana wa Katanga vitu vingi na maendeleo ya hilo jimbo viliibuka na hata sasa usalama wa jimbo hilo umekuwa ukisuasua.

Naamini ipo siku hii nchi itakuwa chini yake japo kuna kesi walimfungulia kipindi fulani.
Moise kupata urais DRC ni ngumu, na ndio maana yeye anaunga mkono Martin Fayulu na Delly Sesanga ,nashangaa Felix tamaa kaitolea wapi ya kujiongezea awamu nyingine ya tatu..kweli Kasai ni kasai tu
 
Sijui Kwanini hatuwezi kupokezana madaraka kwa adabu baadhi ya nchi Africa. Lazima tusumbuane linapokuja suala la kupeana nafasi za uraisi.
mie Felix ndio kanishangaza kweli kweli nikikumbuka 2016-18 ,walivyokua wanapambana kumzuia Josee ,leo hii yeye kaingia mtego ule ule ,halafu wenzie aliokua nao wamekua maadui,
 
Back
Top Bottom