DR Congo: Mamia waandamana Kishansa kupinga mapendekezo ya Katiba mpya kuongeza muhula wa Rais kuongoza

Maandamano hayo yaliandaliwa na muungano wa Upinzani C64, ambao unamtaka Rais Félix Tshisekedi kuachana na mapendekezo hayo ya mabadiliko ya Katiba yanayoweza kufungua njia ya yeye kugombea muhula wa tatu
Mwafrika ni mwafrika Tu, Felix amekulia Ubelgiji alipokimbilia kama mkimbizi kwa sababu za Political suppression na yeye anafanya Yale Yale ya akina Mobutu na kabila
 
Huenda kipindi cha ukoloni kilikuwa ni kipindi bora kuliko nyakati hizi. Wakoloni weusi ni wabaya kipita wakoloni weupe.
 
DR Congo itapata kutulia na kupata maendeleo ikiwa tuu watampa nchi mtu mwenye akili timamu. Na mtu huyo ni Katumbi Chapwe.

Sijui kwa nini hiki kitu wacongoman hawakipigii kelele, huyu jamaa nakumbuka akiwa gavana wa Katanga vitu vingi na maendeleo ya hilo jimbo viliibuka na hata sasa usalama wa jimbo hilo umekuwa ukisuasua.

Naamini ipo siku hii nchi itakuwa chini yake japo kuna kesi walimfungulia kipindi fulani.
 
Sijui Kwanini hatuwezi kupokezana madaraka kwa adabu baadhi ya nchi Africa. Lazima tusumbuane linapokuja suala la kupeana nafasi za uraisi.
Hata Samia alijitwalia urais kwa damu za maandamano na atalazimishwa kutoka kwa maandamano. Hivi hivi huyu hatoki. Na mijinga ya kina Mwigulu inavyompigia magoti ndo kabisaa
 
Sijui Kwanini hatuwezi kupokezana madaraka kwa adabu baadhi ya nchi Africa. Lazima tusumbuane linapokuja suala la kupeana nafasi za uraisi.
Ubinafsi huo Mkuu..

Kipindi cha Uchaguzi hapa Africa ndio Kila ukatili hufanyika hasa mauaji ya Raia wema au washindani wa kisiasa.
 
Hawa mazafakas wa nchi zetu za Kiafrika sijui wamerogwa na nani. Kwenye siasa hakunaga overtime. Muda wako wa kazi ukiisha, you must check out. Any work-in-progress becomes the responsibility of the next elected official.
 
Moise kupata urais DRC ni ngumu, na ndio maana yeye anaunga mkono Martin Fayulu na Delly Sesanga ,nashangaa Felix tamaa kaitolea wapi ya kujiongezea awamu nyingine ya tatu..kweli Kasai ni kasai tu
 
Sijui Kwanini hatuwezi kupokezana madaraka kwa adabu baadhi ya nchi Africa. Lazima tusumbuane linapokuja suala la kupeana nafasi za uraisi.
mie Felix ndio kanishangaza kweli kweli nikikumbuka 2016-18 ,walivyokua wanapambana kumzuia Josee ,leo hii yeye kaingia mtego ule ule ,halafu wenzie aliokua nao wamekua maadui,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…