Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi, ametangaza mpango wa kuanzisha mazungumzo ya kitaifa yenye lengo la kupunguza mvutano wa kisiasa nchini humo, ambao umeongezeka kutokana na muswada ambao wakosoaji wanadai unaweza kumuwezesha kutafuta muhula wa tatu wa urais.
Tshisekedi alisema katika hotuba iliyorushwa na televisheni ya taifa Agosti 27, 2026 kwamba mchakato huo utaanza kwa mashauriano katika majimbo yote 26 ya Congo, kabla ya kufikia kilele chake katika mazungumzo ya kitaifa yatakayofanyika Kinshasa, mji mkuu wa nchi hiyo.
Mchakato wa Mazungumzo
AFC/M23 hawatashiriki
Tshisekedi amesema makundi yenye silaha pamoja na watu wanaofanya kazi kwa niaba ya mataifa ya kigeni hawataruhusiwa kushiriki. Hatua hiyo inawaondoa wazi wapiganaji wa AFC/M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na ambao wanadhibiti maeneo makubwa mashariki mwa Congo.
Watakaoshiriki
Mazungumzo hayo yatahusisha vyama vya siasa, mashirika ya kiraia, viongozi wa dini, viongozi wa kimila, wawakilishi wa wafanyabiashara, wasomi, vijana, mashirika ya wanawake pamoja na raia wa Congo wanaoishi nje ya nchi.
Rais Tshisekedi amesema tarehe rasmi na masharti ya mchakato huo yatatangazwa baadaye, huku mazungumzo yakitarajiwa kuchukua muda usiozidi miezi mitatu.
Wafuasi wa Tshisekedi wamekuwa wakitoa wito wa kufanyiwa marekebisho Katiba ili kumruhusu kugombea tena. Mapema mwaka huu, Tshisekedi alisema angekubali kuwania muhula mwingine endapo wananchi wa Congo wangetaka afanye hivyo.
Madai ya Upinzani
Mpango wa kufanya marekebisho ya Katiba umekosolewa na Kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa pamoja na makundi ya upinzani. Mwezi Juni 2026, maandamano ya upinzani dhidi ya mabadiliko hayo yalivunjwa kwa nguvu na vyombo vya usalama.
Wapinzani wamekuwa wakitaka mazungumzo hayo yawe shirikishi zaidi, yakihusisha pia makundi ya waasi pamoja na wafuasi wa Rais wa zamani wa Congo, Joseph Kabila.
Katiba ya sasa inasemaje?
Katiba ya Congo inamruhusu rais kuhudumu kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja. Tshisekedi alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na kuchaguliwa tena mwaka 2023. Muhula wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.
Democratic Republic of Congo President, Felix Tshisekedi
Source: Reuters