Dr. David Bell: Magufuli kukataa lock down nchini Tanzania kuliokoa maisha ya maelfu ya watu

Dr. David Bell: Magufuli kukataa lock down nchini Tanzania kuliokoa maisha ya maelfu ya watu

Mchambuzi kwenye gazeti hilo ambaye ni mfanyakazi aliyepita wa shirika la afya duniani (WHO) amesema kitendo cha Magufuli kukataa lock down nchini Tanzania kuliokoa maisha ya maelfu ya watu hasa akina mama ,wazee na watoto.
Mchambuzi huyo amesema kwenye nchi ambazo walifungia watu ndani(lockdown) maelfu ya watu walikufa kutokana na njaa pamoja na magonjwa mengine na siyo Corona.View attachment 1801211
Watu walikuwa wanademonize juhudi za huyu mwamba ila wasioficha ukweli wanatoka hadharani kuzipongeza juhudi zake.
Tatizo mama saizi ameingia kwenye mtengo ambao kutoka haitakuwa rahisi. Kikwete na Kenyatta wamemlisha matango pori. Sijawahi ona wao wanahangaika na barakoa, ila mtaani ni mwendo wa covid-free life. Akili za kuambia changanya na zako.
RIP Magu.
 
Hajasema vifo vya uviko-19, bali ukosefu wa chakula na lishe, hususan ni kwa watoto. Muwage mnasoma kabla ya kutoa maoni.
CC: Daudi Mchambuzi

Ameandika

"He rightly predicted that Covid-19 mortality in Africa would be very low compared to other major killers like malaria, tuberculous (TB) and HIV-Aids, and followed good public health principles in prioritising these higher burden diseases that particularly afflict the young, while telling Tanzanians not to panic."

Sasa amejuaje hayo kama takwimu za COVID hana? Au wewe ndiyo hukuisoma?
 
Sasa angeweka lockdown hizo pesa za kukamilisha SGR na miradi zingetoka wapi
 
Kama takwimu za COVID hazikutolewa, huyo mchambuzi anajuaje wangapi walikufa au hawakufa na COVID?
Hata kama taarifa hazikutolewa, utafiti hauwezi kufanyika bila hizo taarifa? Ulisoma hadi darasa la ngapi? Mimi niliishia darasa la saba tu. Ila ninajua kuwa huwezi kuficha taarifa inayohusisha jamii fulani. Utakosa takwimu lakini taarifa za jumla utapata tu.
 
Kuna tetesi zinasemwa kuhusu hizi chanjo kuingiliana na matumizi ya internet kwa mtu aliyechanjwa vp zina ukweli wadau?
 
Ugonjwa wa aina yake,

Lazima utoe takwimu za waliopoteza maisha.

Lazima utoe takwimu za walioathirika.

Lazima ufungie watu ndani.

Lazima watu wakae mbali Mbali.

Lazima ununue Chanjo.
 
Kuna dada mmoja mlokole yupo Tegeta. Alikuwa anamsifia Magufuli kuwa kamaliza Corona Tanzania. Mwaka jana mwezi June/Julay mama yake na bibi yake walikufa kwa Corona. Walipishana siku mbili.

Hadi leo hataki kumsikia Magufuli. Yaani anamuona bonge ya tapeli na muuaji.
Ni kati ya wachache nchi nzima. Ana uelewa mdogo si wa kutolea mfano!
 
Kuna dada mmoja mlokole yupo Tegeta. Alikuwa anamsifia Magufuli kuwa kamaliza Corona Tanzania. Mwaka jana mwezi June/Julay mama yake na bibi yake walikufa kwa Corona. Walipishana siku mbili.

Hadi leo hataki kumsikia Magufuli. Yaani anamuona bonge ya tapeli na muuaji.
Kifo hupangwa na nani?
 
Back
Top Bottom