Dr. Elly: Siyo kila mtu anatakiwa avae maski bali wanaohudumia wagonjwa na wanaohisi wameathirika

Asante kwa hii, kiukweli elimu kuhusu Corona na jinsi ya kujinginga inahitajika sana!

P
Dah...tatizo mambo ya kitaalaam yanatolewa na wanasiasa....
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusambaza na kuambukiza... Bado elimu kubwa inahitajika...kwanini tuvae mask...tunawe mikono...tutumie sanitaiza...

Sent using Beretta ARX 160
 
Nimecheka sana bwashee!
Ha haaaa,niko kanda pendwa huku mkuu. Ila tujitahidi kupaza taarifa kwa wananchi.

Nadhani moja ya madhara ya kuvigeuza vyombo vya habari kuwa vituo vya propaganda za serikali ni hili.
Siku hizi watu hawaangalii tena hata taarifa za habari sababu wanajua watakutana na flai ova, standadi geji, mandege, tumbua/teua nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka watangazaji kwenye tv wamevaa mask, habari hazisikilizwi Bali tunaangalia mask zao. Studio kwa nini zisipulizwe dawa? Ulimbukeni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi kinachonikera ni watu kuvaa kidevuni, mfano Mbatia jana, alivyokua anaongea na waandishi wa habari, huku amevaa kidevuni, huo ni ulimbukeni tu, ni kama dr kumkuta nje au kwenye studio akihojiwa huku ametundika stethoscope mabegani.
Mbona hawatembei na syringe kwenye corido za hospitali!

Pia kwenye ishu ya corona, kumzuia mtu kuvaa mask hata kama ni kitambaa kuziba pua na mdomo, huku una msisitiza akipiga chafya ajizipe mdomo kwa kitambaa kuepusha kusambaza vijidudu ni kujichanganya, ni bora kusisitiza kuvaa mask kuliko kuwakataza.
 
Bwashee hujakatazwa kuvaa maski!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…