Mnangagwa ni kama mamba ambae alikuwa hajitambui na pia haelewi ujazo wa maji na kina cha mto alokuwamo.
Ni sawa na mtu ambae hujawahi kuishi karibu na mlima lakini unaanza kujenga Imani potofu kuhusu ule mlima.
Lakini hapo hapo kandokando ya mlima wapo watu wanaishi na kukata kuni na kuendelea na shughuli zao mbalimbali kama kawaida.
Lakini cha kushangaza ni mlima huohuo kuanza kujenga imani potofu juu yake wenyewe na watu kutoka pande zingine wakaanza kujenga imani potofu juu ya mlima huohuo.
Hivyo basi Emerson Mnangagwa alikuwa ni kama mamba na pia alikuwa ni kama mlima.
Lakini hakuna siku hata moja milima inaweza kukutana na hivyo ndivyo jinsi ilivyotokea kwamba mzee Bob ukiwa ni mlima mwingine ulio mbali, akaona amwondoe Emerson Mnangagwa ambae wameshiriki wote kupigania uhuru wa Zimbabwe.
Mnangagwa ni mmoja wa watu hatari kabisa kuwahi kutokea kwenye serikali ya mzee Bob.
Alipoondolewa Joyce Mujuru mwaka 2014 Mnangagwa akapewa umakamu wa raisi kupitia mkono wa idara maalum iiltwayo "Lacoste", idara inayoshirikisha makachero na majasusi wote ambao wanaitwa "the invisible hand".
Lakini ni haohao "Lacoste" ambao wamemuondoa Mnangagwa kwa ajili ya kumpisha mtu mwingine ambae atajulikana baadae.
Kama unafuatilia hii power struggle ndani ya serikali ya mzee Jongwe basi bila shaka utakuwa unakumbuka jina la profesa Jonathan Moyo.