Dr. Hamisi Kigwangalla aibua upya mjadala wa uwekezaji wa Mo Dewji. Ni wapi Anakosea?

Dr. Hamisi Kigwangalla aibua upya mjadala wa uwekezaji wa Mo Dewji. Ni wapi Anakosea?

Nakumbuka wakati marehemu David Ngonya [ Gorbachev] akiwa Katibu mkuu wa klabu hiyo kulikuwa hakuna ujinga wa wawekezaji kuchezea hiyo club!
na katika enzi zake mafanikio ya timu yalikuwa yapi?
 
Shabiki mwenye uchungu mkubwa na timu ya SimbaSC Tanzania Dr. Hamisi Kigwangalla amejikuta akipata Maumivu makali kwa timu yake pendwa kutolewa kwenye kombe la ASFC na Mabingwa wa kihistoria wa Ligi KUU Tanzania bara.

Maumivu yaliyompelekea hata kurudi mitandaoni na kuhoji namna ambayo Klabu iyo inaendeshwa.

Baada ya kutoa maoni yake baadhi ya wachambuzi, mashabiki na viongozi wakubwa wa ndani ya klabu wakaanza kumtumia jumbe za matusi na kebehi.

Je ni wapi Dr. Hamisi Kigwangalla anapokosea kwa kuhoji?

View attachment 2242638
View attachment 2242639
View attachment 2242640
Hana lolote,yeye ile sanamu ya mwalimu ni ya kweli?
 
Tatizo leno ni kutojitambua kuwa hao mnaowaita wawekezaji wanatumia uzuzu wenu kwa faida zao wenyewe!! Nyinyi maishani mwenu mtabakia washangiliaji tu!! Fungueni akili acheni upumbavu huo!! Hiyo mnayodanganywa cheki ni ya benki gani hapa nchini? Jibuni maswali msilete matusi mimi sio size yenu!!!

Nakumbuka wakati marehemu David Ngonya [ Gorbachev] akiwa Katibu mkuu wa klabu hiyo kulikuwa hakuna ujinga wa wawekezaji kuchezea hiyo club!
Wawekezaji wote wanataka faida, kuanzia madrid hadi simba
 
Tatizo leno ni kutojitambua kuwa hao mnaowaita wawekezaji wanatumia uzuzu wenu kwa faida zao wenyewe!! Nyinyi maishani mwenu mtabakia washangiliaji tu!! Fungueni akili acheni upumbavu huo!! Hiyo mnayodanganywa cheki ni ya benki gani hapa nchini? Jibuni maswali msilete matusi mimi sio size yenu!!!

Nakumbuka wakati marehemu David Ngonya [ Gorbachev] akiwa Katibu mkuu wa klabu hiyo kulikuwa hakuna ujinga wa wawekezaji kuchezea hiyo club!
Ni lini watu walionesha cheki halisi ya benki siku ya kusaini mkataba au zawadi?
Mfano wa hundi unataka iwaje?
 
Yeye Bwana Amisi Amechangia kiasi gani kwenye club ya simba mapaka sasa? Atuonyeshe Kwanza ndio Ahoji.
 
Hoja yake inasubiri timu ifanye vibaya?aache chuki binafsi baadhi ya mambo yake yangeenda vizuri tusingemsikia
 
Bahati mbaya imefika hatua nampuuzia Kigwangala kwa lolote, am sorry to say ni mtu asie na msimamo, mzabizabina na sio mkweli niki reflect maisha yake ya siasa. He is not a real man.
 
Hata angeweka hiyo 20b, kakoranya asingedaka lile shuti
 
Kabla ya Mo wote tulikuwepo akiwemo yeye Bw Kigwangala...je aliwahi kufanya lolote kwa Simba kabla ya MO?...kama bado ni nini kinamvutia sasa hivi tofauti na huko awali?....na kama leo Mo ataondoka Simba hakuna kitu Kigwangala atafanya zaidi ya kupata amani yake ya moyo ya kufurahi kuwa amemkomoa MO...kwa maelezo mengine kilio cha Hamisi ni unafiki wa kuridhisha nafsi yake pekee na wala sio kwa manufaa ya Mashabiki...yaleyale ya Joka la Mdimu.

Sio mbaya kutoa maoni yake kwani anatimiza haki yake kikatiba, na kama anadhani ana hoja ya Msingi basi tuende kwa Mashabiki tuwaulize wao wanataka nini....Hivi kweli Mimi Shabiki wa Simba niliyeko huku Sitimbi uniambie nichague kati ya kufuatilia Mo anapata nini na Timu kushinda Mataji na kuifunga Yanga nitambe mtaani kwamba nitachagua kutaka kujua MO anapata nini?.

Kwa nini Kigwangala asituletee pia gharama za kuindesha Simba kwa Mwaka akalinganisha na inachoingiza Timu nayo atuwekee kwenye page yake...huenda labda atasema hawampi ushirikiano wa kuona Vitabu, basi aje na makadirio tu....nadhani sio ngumu sana kujua Chama analipwa wastani kiasi gani, na Ma pro wengine n.k...Safari za ndani na Nje, Malazi na matumizi mengine ni rahisi kwa Wanamichezo wazoefu kutoa makadirio.

Mimi ni Shabiki wa Simba sio MO, hivyo hivi leo kama Kigwangala akileta Mtu mbadala akaniambia kuwa ana mipango mizuri na uwezo wa kisimamia Simba labda nitamuelewa kuliko anachojaribu kueleza hapo....najua yeye "Joka La Mdimu" hawezi kusema yeye ndio ana uwezo huo.

Mimi nikimuona Manula uwanjani, Sakho, Banda n.k najua wanalipwa ndio maana bado wapo Simba...au nikiambiwa Chama anatakiwa na Yanga lakini mwishowe tukafanikiwa kuwadhibiti wakashindwa kumchukua kwangu inatosha...hivi kweli unataka nitoke nikamuhoji MO umemlipa nini Chama Yanga wakashindwa kumchukua?...ili iweje?...na akiniambia nichangie mshahara wake wa mwezi nitasema nini?.

Kama Bw Kigwangala anadhani ana namna bora zaidi ya kushauri uendeshaji wa Jambo na liwe na ufanisi si ajikite kwenye sekta anayoitumikia? au huko keshamaliza na kila kitu kiko sawa?.....basi kama anatamani biashara na Michezo basi aanze kuisadia Timu yoyote kwanza wakati anasubiri MO aachie Simba aingie yeye...kuna timu inaitwa Kitayose inatokea kwake Tabora kama sikosei...hebu awe karibu nayo awaisaidie Timu ifike mbali hata ikiwezekana waipiku Simba hii anayotuambia inapunjwa.

Kuna wakati nakumbuka amemshambulia Dokta Mwaka na mpaka leo sijafanikiwa kujua ni vipi kati ya wote wanaofanya shughuli kama za Dk Mwaka akamchagua yeye....na je alifanikisha kwa alilotaka kwake?.

Kama wapo wanaodhani Kigwa ana hoja basi sawa, lakini Mimi kwa kweli sioni hoja zaidi ya visa tu na ubinafsi...MO lazima ahakikishe Timu inarudisha faida ya anachowekeza tofauti na hapo Yeye na Timu wote watakufa.
 
Hamna Cha maana, Simba shida yake sio hela.
Shida ya Simba ni poor management
Kama sio hela unasajiri vipi wachezaje wapya pasipo kuwa na fungu, Mo ana shida ameisaidia club lakini ana upotoshaji sana na ameshatuona maboya hatuwezi hoji kitu tupo tupo tu machawa
 
Back
Top Bottom