Dr: Huu ndio Unywaji salama wa pombe kwa wanaume, wanawake na wajawazito

Dr: Huu ndio Unywaji salama wa pombe kwa wanaume, wanawake na wajawazito

Zikiisha kichwani umaskin palepale na atakupa mke na watoto umlelee
 

Wanaume ni vipimo (units) 3 kwa siku au 21 kwa wiki.

Kipimo kimoja = chupa 1 ya bia; bilauri (glass) 1 ya mvinyo = Tot moja ya whisk, gin, konyaji nk.

Wanawake: Wasizidishe vipimo (units) 3 kwa siku au 14 kwa wiki.

Wajawazito: Hawaruhusiwi kunywa kabisa. Ikiwa ni lazima sana wanywe unit 1-2 mara moja au mbili kwa wiki na kabisa wasijaribu kulewa

Kwa Dini ipi
Maana Ukristo na Uislam zote zinaharamisha Pombe.
Hapo vipi,au hivyo vipimo vimebarikiwa
 
hahahah umenikumbusha mwaka Fulani hivi, kuna jamaa yangu alikuwa na ndugu yake ametoka Ujerumani, basi aliporudi home akamwambia kaka yake pamoja na mie tutoke akatununulie kinywaji. Lahaula! kufika bar eti akaagiza bia moja ya Kilimanjaro akamwambia muhudumu alete glass 3, basi akasema tutagawana ile bia moja watatu na hiyo hiyo hakuna kuongeza eti ndio Ujerumani WANAKUNYWAGA hivyo? yaani kaka mtu alichukia sana akaanza kufoka "sasa wewe dogo nakuuliza hapa ni Ujerumani? kwanini umetusumbua kutuleta hadi huku halafu unaleta ujuaji wa Ujerumani" mie nikawa mbavu sina nilicheka na hata ninavyotype hapa nimeikumbuka hiyo story nina cheka sana.
 
Back
Top Bottom