Dr: Huu ndio Unywaji salama wa pombe kwa wanaume, wanawake na wajawazito

Zikiisha kichwani umaskin palepale na atakupa mke na watoto umlelee
 

Kwa Dini ipi
Maana Ukristo na Uislam zote zinaharamisha Pombe.
Hapo vipi,au hivyo vipimo vimebarikiwa
 
hahahah umenikumbusha mwaka Fulani hivi, kuna jamaa yangu alikuwa na ndugu yake ametoka Ujerumani, basi aliporudi home akamwambia kaka yake pamoja na mie tutoke akatununulie kinywaji. Lahaula! kufika bar eti akaagiza bia moja ya Kilimanjaro akamwambia muhudumu alete glass 3, basi akasema tutagawana ile bia moja watatu na hiyo hiyo hakuna kuongeza eti ndio Ujerumani WANAKUNYWAGA hivyo? yaani kaka mtu alichukia sana akaanza kufoka "sasa wewe dogo nakuuliza hapa ni Ujerumani? kwanini umetusumbua kutuleta hadi huku halafu unaleta ujuaji wa Ujerumani" mie nikawa mbavu sina nilicheka na hata ninavyotype hapa nimeikumbuka hiyo story nina cheka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…