Elections 2015 Dr. John Magufuli halisi usiyemjua na yule unayemjua kupitia CCM! Ni HATARI kwa Taifa!

Elections 2015 Dr. John Magufuli halisi usiyemjua na yule unayemjua kupitia CCM! Ni HATARI kwa Taifa!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Daktari wa falsafa John Pombe Magufuli Mnyatuzu halisi kutoka Biharamuro Geita Kaskazini mwa Tanzania ni mmoja ya wasomi wa chache wenye kutokeza mbele ya uso wa binadamu kwa kigere na tashwishwi la ushomire kwa upinde wa magharibi ya Biharamuro.
Daktari huyu ni nguli wa kemia na uhandisi wa majengo na barabara akidumia katika unakili wa takwimu kwa vibwebwe vya mwafrika wa ubwa. Magufuli anatajwa kuwa ni miongoni mwa waswahili wa chache wacha-Mungu na wachapakazi machoni pa walimwengu lakini nyuma yake akilaza uhalisia wa Magufuli.
Magufuli amepitia vilima na vilindi mpaka madaraka kamili aliyonayo sasa huku historia yake ikigusa ubedui na shababi wake halisi toka vilindi vya karagwe. Kisa kikuu kinachomtambulisha kwetu Magufuli ni kutoka viunga vya Katoke, mwaka 1977 alifukuzwa shule Katoke seminari Biharamuro akiwa kidato cha 3 na alikuwa anasomea upadri alipofukuzwa akaenda Mwanza Lake Sekondari, wajua alifukuzwa kwa kosa gani? Atajibu yeye!

KWA NINI MAGUFULI SIYO JEMBE

1.MAGUFULI HAWEZI KAZI (UNDERPERFOMANCE)
Magufuli amewahi kufanya kazi wizara tatu za JMT ambazo ni UJENZI, ARDHI na MIFUGO
Amekuwa Waziri wa wizara ya ujenzi haijagawanywa kipindi cha Mh. Mkapa na Kipindi cha Mh. Kikwete ambapo chini yake kulikuwa na taasisi zifuatazo:-
1. Barabara - TANROADS ( Tanzania National Roads Agency)
· Anasifika kwa quantity and not quality
2. MAJENGO/NYUMBA - TBA ( Tanzania Buildings Agency)
· Kauza nyumba za serikali
· Kashindwa kujenga mpya kama alivoahidi
3. Vivuko /Taa za barabarani- TEMESA ( Tanzania Electrical, Mechanical and Electronics services Agency
4. Bandari - TPA ( Tanzania Ports Authority)

· Mapungufu yameeleza hapo chini
5. Viwanja vya ndege - TAA ( Tanzania Airports Authority)
· Madawa ya kulevya yanapita sana hapa na hakuwahi kusema chochote.
· Viwanja vingi vya ndege ni vibovu sana
6. Air Tanzania Corporation - ATC
( kuna mikataba mibovu sana ATC, uchunguzi unaonyesha ilifanyika wakati wake. Mikataba kama kukodisha ndege ambayo haikuleta manufaa, kulipia parking fee kwenye viwanja vya ndege nje ya nchi wakat ATC haina ndege hata ya maonyesho kwa vizazi vijavyo tu n.k).
Katika idara zote hizo Magufuli anasifika idara moja tu ambayo ni Barabara - TANROADS ambayo hata katika hiyo anasifika kwa wingi (quantity) na siyo ubora (quality).
Je ukimpa nchi yote ataweza kama ameshindwa wizara moja tu?



BANDARINI
· Hajawahi kuzungumzia matatizo na kukosa ufanisi kwa bandari yetu, kumbukeni wateja walikuwa wanaaza kukimbia. Bandari ni lango kuu la uchumi lakini Magufuli alifeli.
· Mwakyembe kwa kubadirisha tu utaratibu wa malipo kutoka CASH kwenda kulipia bank, mapato yaliongezeka maradufu.
· Aliuza nyumba za serikali na hivyo kuipatia serikali gharama za kuwapangishia maafisa wa serikali. Pia Magufuli aliliahidi bunge kuwa atajenga nyumba mpya 5,000 lakini hadi leo hata nyumba 500 hazijafika!
· Alipokuwa wizara ya ardhi alishindwa kutatua migogoro ya ardhi na utendaji wa wizara ulikuwa hauna ufanisi. Leo hii Mh. Lukuvi amefanya kazi kubwa sana kwa miezi michache tangu ateuliwe. Leo hii unaweza kupata hati ya ardhi ndani ya wiki mbili tu!

· Alipokuwa wizara ya Mifugo bado alishindwa kufikia malengo ya maendeleo ya mifugo, ikumbukwe Tanzania ni ya tatu kwa mifugo afrika. Lengo ilikuwa kuongeza mapato kwa kuuza nyama nje ya nchi. Mtakumbuka JK alisema kuwa ng'ombe na wafugaji wote wamekonda,

· Magufuli huyuhuyu kwa ubabe ameingilia mchakato wa ujenzi kiwanda cha kusindika nyama mkoani pwani kwakushinikiza zabuni ya ubunifu na ukadiriaji majenzi wapewe SUMA JKT ambao kitaalamu na kisheria hawana sifa hiyo kwakuwa wao wamesajiriwa kama makandarasi wa ujenzi tu, kibaya zaidi wakalipwa malipo ya awali zaidi ya nusu kinyume na utaratibu wa PPRA unaoweka ukomo wa malipo ya awali uwe chini ya 30% ya gharama za mradi.

Matokeo yake mradi huo haujaishi kwa miaka yote tangu uanze.

Je huyu mtu tukimpa nchi ataweza?

2. Magufuli anatenda kazi kwa hasara.
i. Magufuli kwa maamuzi ya kukurupuka na ubabe alibomoa nyumba/majengo akidai yako barabarani na wamiliki walikwenda mahakamani na kushinda kesi na serikali imelipa mamillionii ya fidia. Pesa hizi zingetumika kutengeneza madawati mengi sana.
ii. Akiwa Mifugo alikamata meli ya wavuvi na samaki (maarufu kama Samaki wa Magufuli) kwa kukurupuka na hatimaye serikali ikashindwa kesi na kulipa TZS…………… Pesa hizi zingeweza kulipa madeni ya waalimu na kuongeza maendeleo ya elimu nchini.
iii. Pia kwa maamuzi ya kukurupuka na kibabe amesababisha kukwama kwa mradi machinjio ya kisasa ya RUVU. Magufuli aliilazimisha NARCO (National Ranch Corporation) kuwapa tenda ya kujenga JKT. JKT hawakuweza kukamilisha huu mradi na serikali imekosa fedha nyingi za kigeni ambazo zingetookana na kusafirisha nyama nje ya nchi.
Magufuli amenunua kivuko kikuu (chakavu) cha MV DAR kwa mabilioni ya pesa za kitanzania, Meli ya bakharesa mv Kilimanjaro inabeba abira 500, imetengenezwa mwaka 2015 bei ni billion 6, safari ya kwenda unguja inachukua saa moja na robo tu,
Wakati Meli hiyo chakavu ya Magufuli maarufu kama Mv Dar safari ya kwenda bagamoyo hapo tu inatumia saa tatu, imetengenezwa mwaka 1978, inabeba abiria 350 na imenunuliwa kwa billion 8, Meli hizi zote zinalingana ukubwa!


iv.
v. Kwa kuuza nyumba za serikali, Serikali inatumia gharama kubwa kuwapangishia nyumba maafisa wake ikiwa ni pamoja na kuwaweka hoteli kubwa maafisa ambao hawajapata nyumba.
vi. Kwa ujenzi wa barabara mbovu, serikali inatumia gharama kubwa sana kukarabati barabara. Pesa hizi zingetosha kujenga barabara kilomita 3600 mpya za barabara
vii. Pia kwa barabara mbovu anawatia hasara kubwa watumiaji wa barabara (wenye magari) kwani inawalazimu kutengeneza magari yao mara kwa mara
viii. Barabara nyingi zisizo na viwango na zenye mashimo zimekuwa chanzo kikubwa cha ajari za barabarani.
ix. Kwa kushindwa kusimamia vyema bandari na ATC, uchumi wa nchi unazidi kudumaa na tunazidi kuwategemea wafadhiri. Mh. Kagame aliwahi kusema yeye akipewa bandari ataweza kuendesha nchi!




Watanzania hebu tujiuulize,
Magufuli aliyefeli wizara zote alizopitia na aliyetia hasara kubwa taifa hili anafaa kuwa raisi?
Magufuli mwenye maamuzi ya kibabe akiwa waziri, akipewa uraisi si ndo atafanya ubabe mkubwa zaidi?

Sio kazi yangu kukuchagulia rais, ila ni wajibu wangu kuliponya taifa kwakuzuia wahujumu taifa hili wasiiguse Ikulu ya Tanzania.

IN LOWASA WE TRUST!
 
Hoja zako ni too general. Ndo maana Dr Slaa akakuambia Shut Up Yeriko. Mpaka ukapigwa ban ya wiki. Sasa umeanza kuandika mambo ambayo hayana uhalisia

Kuna hoja unayoweza kuijibu kijana?
 
bw Yericko,
ingekuwa vizuri zaid ukitumia nafasi yako kutuleza kwanini tuiamini chadema wakati mlituaminisha kwamba LOWASSA ni fisadi na alihusika na RICHMOND alafu leo hii mnatuambia ni msafi na muadilifu??

Kama mmeyakana maneno yenu mchana kweupe, Je mkiingia ikulu SI MTATUSALITI ALFAJIRI NA MAPEMA??

Mwisho naomba niulize LIST OF SHAME NI ILE ILE AU IMEKUWA EDITED???
 
kuna hoja unayoweza kuijibu kijana?

najua nafsi inakusuta tu kwa kuwa mnafiki hata mbele za mungu kama kweli wewe ni mkritu kweli unatumia karama aliyokupa mungu kumtukana mtu ambaye kwa miaka 10 amefanya kazi ya heshima katika nchi hii?
Fany siasa ya hki ambyo inabaraka hata kwa mungu achana na majitaka yako mungu aliyempaga atakuawa maana hakuna ambaye anaweza kupinga mpango wa mungu,
chukua ushauri huu utakusaidi,
 
Yaliyoandikwa kuna uhalisia mkubwa! Uwani kwa takwimu za kimya kimya maengineer wa tanroads wanaongoza kwa mali ambazo hazina maelezo na barabara nyingi ni substandard!
 
naamin magufuli hawezi kunyanyua mdomo na kumsema lowassa

yaan watu wanaona bararaba tu na hawajiulizi kuhusu idara zingine alizozisimamia zilivyooza
 
bw Yericko,
ingekuwa vizuri zaid ukitumia nafasi yako kutuleza kwanini tuiamini chadema wakati mlituaminisha kwamba LOWASSA ni fisadi na alihusika na RICHMOND alafu leo hii mnatuambia ni msafi na muadilifu??

Kama mmeyakana maneno yenu mchana kweupe, Je mkiingia ikulu SI MTATUSALITI ALFAJIRI NA MAPEMA??

Mwisho naomba niulize LIST OF SHAME NI ILE ILE AU IMEKUWA EDITED???

MKUU NAWASHANGAA HAWA JAMAA WANASEMA SIASA SIO VITA WALA UGONVI WALA UNAFIKI LKN MTU AMBAYE ANA AKILI TIMAMU ETI ANAPONDa KAZI ALIYOIFANYA MAGUFULI KATIKA TAIFA HILI ,KWA MWENYE AKILI NI WENDAWAZIMU, UNAMSHAngilia mtu ambaye amekuwa kimia pasipo kujadirihoja yeyote ya maslai ya taifa ndani ya miaka 7 na kumchafua magufuli,ni bora kuchukua mda kumsifia lowasa kwa yale aliyoyafa kuriko uchafu wao,
 
  • Thanks
Reactions: tyc
naamin magufuli hawezi kunyanyua mdomo na kumsema lowassa

yaan watu wanaona bararaba tu na hawajiulizi kuhusu idara zingine alizozisimamia zilivyooza

nikuulize swali upana wako wa kusafiri nchi hii unakomea wapi na umeaza kusafiri nchi hii tangu mwaka gani?

naomba majibu kama kweli unachokisema unakijua,

 
Najua Yericko Nyerere, tatizo ni umalaya wa siasa na kukubali kutumika hata kama unajua ukweli wa kitu na kujitia wendawazimu kwa siasa chafu,sitaki kusema mengi ila jiulize maswali haya ,unapomkashi magufuli kiasi hiki kwa sababu ya kutumika tu

1. Wewe umelifanya nini taifa hili kwa umri wako kiasi cha kuona alichokifanya magufuli ni upuuzi kiasi hiki?
2. Kushidwa kwa magufuli unakupimaje ili hali mgombea wako ameongoza wizara ya maji hadi anatoka baro maji yalikuwa janga la taifa?

Miaka saba ya ukimia unawezaje kulinganisha na magufuli kwa kile alichokifanya japo macho yenu ya kipofu wa siasa hamuyaoni hayo bali miaka saba ya ububu ndo shangwe kwenu,ni aibu kwa siasa za naman hii,
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom