Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Pamoja na kuwa mimi sifungamani sana na masuala ya kisiasa ila ...tumseme makuful kwa mabaya na mazuri pia...ili tuwe fair
BARABARA: Ukweli ni kuwa Barabara zetu ni nzuri na zinabeba uzito kuliko barabara za jirani yetu Kenya ambao wengi hupenda kumtolea mfano.
TATIZO:
Tunatakiwa tufufue reli ili mizigo mizito ipitie huko... hicho tu ndio kitaokoa barabara.
Sina hakika kama umepata bahati ya ketembelea jirani zetu Kenya na kuvinjari mikoa ya huko; tofauti na hapo Nairobi huko kwingine barabara zimekwisha..Ila tatizo la msingi ni kama la kwetu. Mizigo mizito inapitishwa barabarani badala ya relini. Kwao tatizo ni kubwa zaidi kuliko sisi kwani stanani ya barabara zao za highway zinajengwa kwa uzito wa chini kidogo kuliko kwetu...sio kwa uzembe ila ni utaratibu wao.
HOJA YA VIWANJA VYA NDEGE NA MADAWA YA KULEVYA?????
Hivi watu wa migration na airport security si wapo chini ya wizara ya mambo ya ndani? Waziri wa ujenzi anatoka wapi huko?
KUHUSU KUBORESHA VIWANJA VYA NDEGE
Sisi watu wa uchumi tuna sema kinachofanyika kwenye ujenzi wa viwanja vya ndege ni Opportunity cost;
kwa sababu bajeti haitoshi, ni suala tu la kuamua ujenge kiwanja mbeya ...kule kusini nao wawe na kiwanja au ukarabati hivi vilivyopo kule kusini wasubirie neema ya mungu ..bajeti itakapo tosha.
UFANISI KATIKA VIZARA ALIZOPITA:
Binafsi nahisi tofauti na wizara ya Ujenzi Makufuli amekuwa akihamishwa hamishwa sana hivyo hakupata nafasi ya kuonesha kipaji chake vya kutosha...project zote ambazo ni long term katika hizo wizara alizopita hakuweza kuzitekeleza/kuzimaliza...
Ni kwa mfano kiongozi atumie hela nyingi kufeka shamba...na kabla haja anza kuotesha ahamishwe...anayekuja kuchukua nafasi yake asioteshe kama ilivyo kusudiwa...kwa kila mmoja kuangalia vipaumbele vyake kwenye wizara husika. Watu wataishia kufikiri kiongozi wa kwanza amechezea hela nyingi kwa kufweka shamba ... kitu ambacho sio sawa
RELI NA SHIRIKA LA NDEGE
Nikiangalia kwa sura ya kiuchumi, suala la reli na Ndege sio la kuachia wizara moja...hizo ni project kubwa zinatakiwa budget itoke kwanza ya kumaliza matatizo yote yalioko ambayo ni makubwa karibia kuliko capital investiment .. ndio wizara iachiwe ianzie hapo kufanya kibiashara. Kwa hizi bajeti za wizara tegemea miujiza kutoka kwa mungu...reli na Ndege havita fufuka na hata ukitafuta shirika la kuprivataize hutapata au litamshinda. Nani atapokea matatizo na madeni yenye dhamani kuliko capita investiment????
Sijachangia hoja za kisiasa kwa miezi sasa ila...nimeshangazwa na mawazo yako unayo yawakilisha kwa hisia na hivyo kukosa mtiririko....nafikir tukiwa fair kidogo na sio ushabiki usio kuwa na maana tunavutia watu na kutuunga mkono.
Peoples!!!!!!!!