Hao wasio uona ubaya wa Maghufuli watakuwa wamevaa miwani ya mbao.
1. Wawe waangazi zaidi na washughulishe vichwa vyao kufahamu magnitude ya uuzwaji wa nyumba za serikali. (a) Kuna uhamishaji wa raslimali za umma kutoka mikononi mwa (serikali) na kwenda ktk miliki za watu fulani wachache sana na labda ndugu na jamaa za watoa maamuzi nyumba kuuzwa. (b) Hapakuwepo kufikiria thamani ya Ardhi pale nyumba ziliko (Kama Osterbay, Ocean Road, Mikocheni, Upanga, nk) Huko kwa maisha yote ardhi ya hapo itakuwa ikipanda kwa thamani kubwa sana na kamwe umma hautakaa upate hapo ardhi tena. Uwezo wa kujengea watumishi nyumba kwa haraka na kwa maeneo karibu na kazi ili kwamba watumishi hata bila kutumia magari wafike sehemu zao za kazi bila muda kuharibika. (c) Kuzingatia kuwa kuna watumishi waliishi katika hizo nyumba miaka nenda rudi wakizitunza sasa wamestaafu na aidha hawana nyumba au wana nyumba hafifu.
2. Ni viwango na vyanzo vya pesa ya kujenga barabara. Wamejenga barabara kwa viwango ambavyo barabara itatakiwa kujengwa baada ya muda mfupi. Wakati wanajenga wamekopa kutoka vyanzo vingi kwa ruksa ya Uwezo wa kukopesheka. Huo Uwezo kwa kukopa sana wameupunguza na wakijua kuwa muda wao hawapo barabara zitakuwa zimeharibika sana na zinahitaji pesa nyingi kukarabatiwa pesa ambazo tutakuwa hatuna kwa kuwa tutakuwa tunalipa madeni na tumemaliza Uwezo wa kukopa tena. Tutashindwa kuzikarabati na yatakuwa ni mashimo ndani ya Barabara za lami ambayo ni mabaya zaidi kwa mashimo ndani ya barabara za udongo. (b) Kwa nini wahandisi wa barabara wana utajiri mkubwa kuliko vipato vyao kwa mbali kuna siri gani kwenye barabara?
Nikiangalia hayo, nikachanganya na ubabe wa huyu Makufuli wenu, nashindwa kuona usafi wake. Angekuwa hakusoma tungesema elimu inamponza. Sasa kwa nini mambo hayafanani na elimu yake? Bila shaka yanayofanyika yanafanyika kwa makusudi kwa dhamira isiyo safi kwa sisi jamii. Maghufuri ni mbovu kama wabovu wengine. Amekiachia kizazi chetu madhara makubwa sana.