Wakuu Magufuli ni kiongozi mzuri pamoja na makosa yake madogo madogo ambayo naweza kuyaita kuwa ni udhaifu wa kawaida wa kibinadamu. Hakuna binadamu aliye mkamilifu 100%
Tatizo kubwa Sana ninaloliona kwa Magufuli Ni mfumo wa chama alichomo. Ni vigumu Sana yeye as an individual kuubadilisha mfumo huo kwa sababu Kuna wakongwe ndani ya chama ambao hatakuwa na ubavu wa kuwaweka sasa. Hawa ndiyo waliyoliuwa azimio la Arusha.
Tone moja la maji safi haliwezi kufanya maji ya pipa ya masafi, haiwezekani. Hivyo Ni kuuondoa mfumo mzima ili nchi i-experience mfumo tofauti na ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka 50 bila mafanikio yaliyotarajiwa na ahadi nyingi ambazo zimeshindikana kutekerezeka.
Iko wapi nguvu mpya, Ari mpya na Kasi mpya? Iko wapi nguvu mpya zaidi, Ari mpya zaidi na kazi mpya zaidi? Yako wapi maisha bora kwa kila mtanzania? Iko wapi Kigom kama Dubai ya Tanzania? Ziko wapi meli zilizoahidiwa kule Victoria, Tanganyika, Nyasa?
Bila kubadili mfumo ni sawa na kuweka kilaka kwenye suruali ya zamani amakuweka mvinyo wa zamani kwenye kiriba kipya. Suruali itakuwa Ni ile ile ya zamani na mvinyo utakuwa Ni ule ule wa zamani. What we need is a complete chemical change not physical change.