Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Tangu ulipoanza huu mchakato wa kutuia nia pamoja na uchaguzi wa kumtafuta mpeperusha bendera ya CCM mwaka huu huyu Ndugu J.P Magufuli sikutegemea kabisa kama angeibuka kidedea.

Pamoja na hali ya mezingwe unayosemekana kutokea katika zoezi zima la uchijaji wa majina naamini huyu anaweza kuifanya CCM isiwe na upinzani mkubwa wa kimakundi ndani kwa ndani.

Natumai atakuwa kiongozi atakayebeba shida zetu kama shida za familia yake.

Hakuna kiongozi wa aina hiyo toka CCM. Endelea kushuhudia madudu ya CCM miaka nenda miaka rudi.
 
Ujinga ni kumshangilia Magufuli wakati nyumba yako/yenu ipo ndani ya hifadhi ya barabara.
😂😂😂?
 
HONGERA SANA MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI, TUNAKUOMBA USIJE TU UKABADILIKA UTAKAPO JAALIWA KUINGIA MAGOGONI NA KUWA JOHN ALCOHOL PADLOCKS rejea wimbo wa zamani wa marehemu MARIJANI RAJABU YULE ALIYEPATA MADARAKA AKAJIITA JOHN SMITH. TEHE.....TEHE........TEHE.EEEEE...........!!
 
Edit hizo hesabu haziko sawa. Nimeshangaa hata makinda anasema Asha Rose kapata 59% ya kura. Kwa maana hiyo angekuwa mshindi na 87% za magufuri singekuwepo
 
Sio lazima Mgombea mwenza achukuliwe katika 3 Bora
Gharibu Bilali aligombea kuteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar na wala hakuomba ya Tanzania nzima kule Kizota, lakini aliliondoa jina akabakia Shein na JK aliposhinda alimuomba wala hakumchukua Salim Ahmed aliyeingia naye 3 Bora na Mwandosya
Kwa hiyo ni matakwa ya Magufuli kumchukua amina au kumuacha

Mkuu umechanganya matukio mawili hapa la 2005 na 2010. maana awamu ya kwanza JK aliitumikia akiwa na Shain na ndio kipindi alipochuana na hao uliowataja.
 
A%20S%20thumbs_up.gif
:cheer2: :busu


:smiling:
 
Huyu mkurupukaji asiyefuata sheria?! Haya tutaona.Usije ukanikumbuka tu.

Wewwewewewe hakuna mtu anayefanya kazi kwa kufuata sheria kama Mr. Pombe. Kumbuka huyu mtu anasoma sana sheria zinahusu madaraka ya uwaziri wake, kwa vyovyote tabia hii haitakoma akifika magogoni. Ila kwa upande wangu mimi ni Ukawa.
 
Wakuu Magufuli ni kiongozi mzuri pamoja na makosa yake madogo madogo ambayo naweza kuyaita kuwa ni udhaifu wa kawaida wa kibinadamu. Hakuna binadamu aliye mkamilifu 100%

Tatizo kubwa Sana ninaloliona kwa Magufuli Ni mfumo wa chama alichomo. Ni vigumu Sana yeye as an individual kuubadilisha mfumo huo kwa sababu Kuna wakongwe ndani ya chama ambao hatakuwa na ubavu wa kuwaweka sasa. Hawa ndiyo waliyoliuwa azimio la Arusha.

Tone moja la maji safi haliwezi kufanya maji ya pipa ya masafi, haiwezekani. Hivyo Ni kuuondoa mfumo mzima ili nchi i-experience mfumo tofauti na ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka 50 bila mafanikio yaliyotarajiwa na ahadi nyingi ambazo zimeshindikana kutekerezeka.
Iko wapi nguvu mpya, Ari mpya na Kasi mpya? Iko wapi nguvu mpya zaidi, Ari mpya zaidi na kazi mpya zaidi? Yako wapi maisha bora kwa kila mtanzania? Iko wapi Kigom kama Dubai ya Tanzania? Ziko wapi meli zilizoahidiwa kule Victoria, Tanganyika, Nyasa?

Bila kubadili mfumo ni sawa na kuweka kilaka kwenye suruali ya zamani amakuweka mvinyo wa zamani kwenye kiriba kipya. Suruali itakuwa Ni ile ile ya zamani na mvinyo utakuwa Ni ule ule wa zamani. What we need is a complete chemical change not physical change.
 
mi nalia tu na elimu yetu.mheshimiwa kama atashinda ninamuomba aje apige msasa kwenye sector hii ya elimu. tunahitaji mabadiliko makubwa sana
 
Back
Top Bottom