Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tangu ulipoanza huu mchakato wa kutuia nia pamoja na uchaguzi wa kumtafuta mpeperusha bendera ya CCM mwaka huu huyu Ndugu J.P Magufuli sikutegemea kabisa kama angeibuka kidedea.
Pamoja na hali ya mezingwe unayosemekana kutokea katika zoezi zima la uchijaji wa majina naamini huyu anaweza kuifanya CCM isiwe na upinzani mkubwa wa kimakundi ndani kwa ndani.
Natumai atakuwa kiongozi atakayebeba shida zetu kama shida za familia yake.
Sio lazima Mgombea mwenza achukuliwe katika 3 Bora
Gharibu Bilali aligombea kuteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar na wala hakuomba ya Tanzania nzima kule Kizota, lakini aliliondoa jina akabakia Shein na JK aliposhinda alimuomba wala hakumchukua Salim Ahmed aliyeingia naye 3 Bora na Mwandosya
Kwa hiyo ni matakwa ya Magufuli kumchukua amina au kumuacha
Awe Nahodha. Namkubali sana huyu.
Huyu mkurupukaji asiyefuata sheria?! Haya tutaona.Usije ukanikumbuka tu.
Watu kila mkikaa ni kukiombea CCM mivutano yani hamjajifunza kuwa CCM ni wazoefu katika haya mambo.
siku zote tunasahau kwamba makamu wa rais ni potential president likitokea lolote kwa aliyepo madarakani.
Ni vyema awe na sifa stahiki!