UTEUZI WA MAGUFULI HAUJAMALIZA MAKUNDI
CCM.
Wengi wanaamini kuwa uteuzi wa Magufuli ndio
umemaliza makundi ccm na ile vita ya kugombea
urais ndani ndani ya ccm.
Lakini sitakosea sana kusema ni umasikini wa fikra
kwa
mtu mwenye kuamini hivo. Kwa sababu
1. Lazima watu wawe wepesi wa kufikiri ili waweze
kutenda vyema.
Makundi mawili wakubwa ndani ya ccm ni moja, wale
wanaomwabudu Lowasa na la pili ni lile
linalomwabudu membe kupitia mjomba wa ikulu.
Hakuna jipya zaidi ya hilo, wengine wote wanaobaki
ni vibendera fata upepo.
Je magufuli ni malaika? Je hajazaliwa toka kwa
makundi hayo?
Hilo ni swali tunapaswa kujiuliza.
Kundi moja limekaa kimya na halijapinga chochote
au kuonyesha dukuduku yeyote juu ya uteuzi
huo.nini tafsiri yake? Je haitoshi kusema kuwa
magufuli ni membe aliyekuja kwa sura nyingine??
Tafakari.
Je vipi upande huu wa lowasa? Mbona wanalalama
sana? Wamegundua nini?nini tafsiri yake?
Je haitoshi kusema kuwa uteuzi wa magufuli ndani
ya ccm katika kuwania nafasi ya urais wa Tanzania
ni mwanzo mpya wa kuibua hisia za kimakundi ndani
ya ccm? Tafakari.
Tuwe wepesi wa kutofautisha kati ya uteuzi na
kuchaguliwa na mwisho kabisa kile kifo cha ccm
nlichokisema 2012 kitatimia pale October ambapo
sasa wapinzani watakaopoenda kupewa ushindi toka
kwa wale watanzania ambao wanatambua kuwa
tatizo la ccm sio Kikwete, magufuli ama lowasa bali
ni MFUMO endeshaji na TAWALA, SERA
ZISIZOTEKELEZEKA NA UNAFIKI.
kwa hali kama hiyo ata angewekwa malaika
kisayansi na kiutaalamu awezi kuleta lolote jipya
kwa mfumo huo. # UMEJIANDIKISHA .??
by activisty
activistyi@yahoo.com