Hivi hatuna cha kuzungumzia kuhusu Magufuli zaidi za uuzwaji wa nyumba za Serikali!!!
Mbona suala hili limekwisha fafanuliwa na Waziri mkuu mstaafu Mh.Sumaye kwamba uuzaji wa nyumba za Serikali ulifanywa na baraza la Mawaziri chini ya Rais, sasa kwa nini mnakazania kumkandia Mh.Magufuli as if ulikuwa ni uhamuzi wake binafsi!
Mnapenda sana kutoa an impression kwamba Mh.Magufuli ana act like unguiged missile!!!
Tunacho sahau ni kwamba yeye alikuwa ni mtekelezaji mahamuzi ya Serikali. Nyumba hizo ziliuziwa Watanzania wenzetu,kwani tatizo liko wapi, je mlitaka wauziwe wageni? Mh.Sumaye alisema kama Serikali ingeuza nyumba hizo kwenye open market basi wanunuzi wangekuwa Wazungu na Wahindi, je nyinyi mlitaka wauziwe wageni na si waswahili wenzenu au!!! Huu kama sio wivu ni nini?
Tafuteni hoja nyingine zenye mshiko,mkijitia kug'ang'ania hoja ya uuzwaji wa nyumbani za Serikali kama ndio hoja ya kumu corner Mh.Magufuli basi nasikitika kuwambieni hoja hiyo inekwisha tupwa kwenye trashcan.