Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

mafuriko yaliyopo yanang'oa mpaka visiki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
But ujumbe umefika

Sidhani kama umefika...ni mpaka bosi wao mamvi aongee ndiyo na hao watatoka kutoa kauli....

Besides, mgeja na msukuma wote ni wafuasi wa mamvi, so no issues....

I bet msukuma anafanya biashara....if yes hatothubutu kusema kitu....siku akifungua mdomo the next day TRA watagonga hodi mlangoni kwake na kitakachofuat....he knows it...

Hawa wote ni wasaka tonge tu....Nape aliwaelezea kwa lugha nyepesi sana..."samaki anafurukuta ndani ya maji, nje ya maji ni marehemu"...
 
Daktari John Pombe Magufuli, alipataasilimia 87 % ya kura za wajumbe, hiyo ikiwa ni kura 2104.

Daktari John Pombe Magufuli, aliwashinda wapinzani wake Bi Amina Salulm Ali na dakta Asha-Rose Migiro.
Magufuli ni Nani?
Lakini je Daktari John Pombe Magufuli ni Nani?
Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.
Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera. Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati. Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia. Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT . Alizaliwa Oktoba 1959 Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge. Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu. Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.

Alianza siasa mwaka 1995
Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.
Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.
Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi. Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.

Anatambulika kuwa Mchapa kazi Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti. Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.

Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa Chato kabla ya kumkaribisha mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kuwasalimu,kujitambulisha na kuwashukuru wananchi kwa kipindi cha miaka ya 20 aliyoitumikia kama Mbunge.
 
Hayo mafuriko ya mamvi hatuyaoni coz wanaomfuata wote ni vibaraka na kama Dc Makonda alivyosema ni pamoja na huyo mngeja,msindai,hstutawashangaa coz walikuwa ccm kimaslahi na usaliti,tupa kulee!!!
 
Natamani kusikia kauli ya MWENYEKITI wa CCM mkoa wa shinyanga Musukuma
Mie nadhani msijipe matumaini makubwa kupitiliza. Ni watu wachache tu waliokuwa wafuasi wake watakaokuwa tayari kumeguka hata kama naye atameguka. Kumbuka ccm nayo ni taasisi, ila Lowasa ni mtu tu. Ningetamani ivunjike, ila sio rahisi kihivyo!
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa Chato kabla ya kumkaribisha mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kuwasalimu,kujitambulisha na kuwashukuru wananchi kwa kipindi cha miaka ya 20 aliyoitumikia kama Mbunge.

safi sana hawa chagasaccos wapo kama mafisi wanasubiri mizoga
 
Hayo mafuriko ya mamvi hatuyaoni coz wanaomfuata wote ni vibaraka na kama Dc Makonda alivyosema ni pamoja na huyo mngeja,msindai,hstutawashangaa coz walikuwa ccm kimaslahi na usaliti,tupa kulee!!!

Huyo Paul Makonda naye ameupata u-DC baada ya kulamba viatu vya mtoto wa mfalme!
 
Hayo mafuriko ya mamvi hatuyaoni coz wanaomfuata wote ni vibaraka na kama Dc Makonda alivyosema ni pamoja na huyo mngeja,msindai,hstutawashangaa coz walikuwa ccm kimaslahi na usaliti,tupa kulee!!!

Kuna ambao wapo ccm,na hawapo kuaslahi?

Ht huyo makonda mwenyewe ni walewale tu
 
Natamani kusikia kauli ya MWENYEKITI wa CCM mkoa wa shinyanga Musukuma

wakati Musukuma, Mgeja na wengine ndani ya NEC ya CCM wanatafakari kuendelea kukataa maamuzi ya Kamati Kuu, ndipo lilipotoka wazo kuwa kurudisha jina la Lowassa katika watano kutaongeza mpasuko, na badala yake wafuasi wote wa Lowassa wawe kwa Magufuli ili Membe na wengine wa Kikwete waanguke. Musukuma na Mgeja ni waasisi wa kumuibua Magufuli. Hayo ndiyo ya siasa
 
Dereva wa safari ya matumaini akiona picha kama hizi ndo anazidi kuchanganyikiwa. Yani yule aliyetua na chopa kwa mbwembwe pale Arusha siku yake ya kutangaza nia ndo anamnadi aliyemuangusha.
 
Ndugu zanguni upo msemo unasema Mungu hadhiakiwi na chochote apandacho mtu ndicho avunacho. Mh ndugu Lowasa aliamini akikusanya matirion ya pesa kwa kufanya ma deal haram atakuja kuwaonga wa Tz na mwisho watampigia kura, akazidi kujidanganya kwakutoa ma milion kwenye misikit na makanisa ili Wazidi kumuombea dhambi zake zipungue. Kumbe Mungu alikumbuka dhambi zake toka alipo anza kupiga deals aram ambazo kwa wakati mwingine ziliwatesa watu weng na hata wengine kupoteza maisha, Mungu alikumbuka mchezo wake wakuwaingiza watu kwenye mikenge ili yeye afaid wakat wenzake wakifukuzwa kaz nakuonekana wabaya na mengine meng siwez andika ila Mungu alimkata Lowasa, wala sio kamati kuu au nani! Mungu alimkataa Lowasa, Mungu alisema atatumia mpaka senti yake ya mwisho ila kamwe sii yeye au yeyote ktk familia yake atakuja kuwa rais. Mungu anajibu maombi Mungu anapenda mwanadam mwenye kiburi kama Lowasa ajuwe Yeye yupo na hakuna kama Yeye na tena anaenda mbali zaidi anataka mwisho kila got lipigwe. Lowasa ni kivul twakiona ila yeye hayupo alishapotea na sasa upepo upo kwa magufuli. Tusubiri Mungu akatukuzwe.
 
mbingu ipi? Labda kama ccm ina mbingu,

lakini mimi nijuavyo ccm ndio imetapikwa kabisa hata kwa MUNGU ndio maana imekua na harufu mbaya sana kwa wananchi,
 
Post ya Kijinga,toka Kwa Mjinga kwenda Kwa Welevu. Expect Miserable Responses.
 
Kutumia neno au jina la MUNGU katika mazingira alivyofanya mleta post sio sahihi inabidi tutumie busara kidogo waleta post we tumaini! embu tafakari halafu jiongeze.
 
Back
Top Bottom