Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Kati ya kura 6 zilizoharibika, imeghundulika pasipo Shaka kuwa moja ni Mheshimiwa Edward Lowasa, mbunge wa Monduli.
 
Katika hali isiyotarajiwa, majina matatu yanawapasua vichwa vigogo Nani awe mgombea Mwenza, ambao ni Shamsi Vuai Nahodha, Hussain Mwinyi na Seif Khatib, huku spika Makinda akimpendekeza Amina ili kupata kura za Zanzibar. Karume hataki jina la Nahodha na Dr Shein anaomba Bilal aendelee ili kupunguza uzito wa kampeni Zanzibar.

Source : Mlinzi wa kiongozi mwandamizi.

Update zitakuja baada ya muafaka.
 
Tangu ulipoanza huu mchakato wa kutuia nia pamoja na uchaguzi wa kumtafuta mpeperusha bendera ya CCM mwaka huu huyu Ndugu J.P Magufuli sikutegemea kabisa kama angeibuka kidedea.

Pamoja na hali ya mezingwe unayosemekana kutokea katika zoezi zima la uchijaji wa majina naamini huyu anaweza kuifanya CCM isiwe na upinzani mkubwa wa kimakundi ndani kwa ndani.

Natumai atakuwa kiongozi atakayebeba shida zetu kama shida za familia yake.
 
Hatimaye uchaguzi wa rais mwaka 2015 umekwisha:

Dr john pombe magufuli - rais wa awamu ya tano-tanzania
 
Umofia kwenu wana JF,

Mh Pombe alitumia madaraka yake vibaya na kujimilikisha viwanja nane vya Mbweni Beach JKT na kujenga ghorofa katika kila kiwanja na ghorofa jingine amemuweka nyumba ndogo. Huyu Pombe amepata wapi fedha za kujenga maghorofa nane (kila ghorofa kwenye kiwanja kimoja) simultaneously kuanzia mwanzo mpaka mwisho?

Tumekabidhi wizara kafanya haya ,Je akipewa urais si itakuwa balaa? Huyu mtu sio muadilifu kabisa, hafai kuongoza nchi hii.
Asante kutujuza. UKAWA umewaambia?
 
Tumeshuhudia watiania wengine wakiwa na confidence za hali ya juu kuliko huyu mzee Magufuli. Bila shaka ccm wamesema potelea mbali kwakuwa waliowategemea hawakupewa nafasi kwahiyo wakaamua kumpa magufuli kwa sababu moja tu yakukinusuru chama.
 
UKAWA inabidi wajipange sana kwa Magufuli. maana ni jembe kweli

Chama kinaweza kumshinda lakini serikali atainyoosha ..tunaomba CCM mtenganishe kofia ili chama apewe mwingine wa kukiweza, hapa ni Makongoro ili nidhamu irudi kotekote.
 
Hongera sana Dr. Magufuli, you real deserve. UKAWA nawaomben sana mjipange vizuri, otherwise tutachekesha.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Wale wa kugeuza ofisi vijiwe wataisoma ..tunaanza na Tanesco jengo la Ubungo lipishe barabara

Umenikumbusha huyu rais wako mtarajiwa alipotumia sheria iliyopitwa na wakati kutaka kubomoa nyumba za watu, bahati nzuri Pinda akastuka! Saa hizi serikali ingekuwa inadaiwa mabilioni.

Nyie shangilieni tu! Nipeni miaka minne ntarudi humu kuwaulizeni.

Uongozi sio sifa, inahitajika hekima.

Mpenda sifa siku zote hukosa hekima.

Labda ategemee wanaomzunguka kumnyoosha, and that is not good.
 
Back
Top Bottom