Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Pasco umeongea point ambayo watu wengi hawataki kuiona.
Kwangu Mimi suala si Dr Ndalichako tu, ila hata Waziri Kawambwa na viongozi waandamizi have to go. Hatukatai kuwa kuna watoto ambao hawasomi, hilo tunalijua maaana wote tumesoma sekondari. Sasa sababu za kufeli haiwezi kuwa moja tu ya uzembe wa wanafunzi.

Sababu zinaweza kuwa zifuatazo:
1. Uzembe wa wanafunzi
2. Mfumo mbovu wa elimu
2.1. Kutokuwa na mitaala ya kueleweka
2.2. Kuwa na shule bila walimu
2.3. Kutokufanya ukaguzi wa kutosha
2.4. Kutokuwa na motisha kwa walimu
2.5. Kutoboresha shule za kata n.k.
3. Utendaji mbovu wa Baraza la Mitihani
3.1. Kutunga mitihani ambayo haiendani na mihutasari waliyopewa walimu kufundisha na wanafunzi kusoma (nakumbuka wakati nasoma Sekondari, nilisoma Book-Keeping na kulikuwa na kitabu kinaitwa Book Keeing for Tanzania Secondary Schools kama sikosei ambacho kilikuwa kinatolewa na Wizara ya Elimu, lakini hata siku moja hutapata swali kutoka ndani ya hicho kitabu. Maswali karibu yote yalikuwa yanatoka kwenye Frank Wood-Business Accounting ambacho wakati huo kukipata ilikuwa mbinde)
3.2. Kutokuwa makini katika usahihishaji
4. Kutowajibika kwa nchi (Uzembe wa Viongozi) (viongozi hawajui kuwa wanatakiwa kulijenga taifa hili kwa kupitia elimu). Nakumbuka kuna bwana mdogo ambaye alishindwa kuendelea na shule akiwa Form Three kutokana na uwezo mdogo. Baada ya miaka kadhaa ya kujishughulisha na biashara akapata fedha akataka kurudi shule ili aendelee. Ile shule aliyokwenda ili ajiendeleze kama Private Candidate akaambiwa alete barua toka ile shule aliyokuwa anasoma. Ile shule aliyokuwa anasoma wakampa barua, kwenda kwenye shule mpya wakamwambia aje na matokeo ya Form Two akawajibu kuwa mwaka wao mitihani ya Form Two ilikuwa imefutwa, ili ilikuja kurudishwa baadaye. Wakamwambia nenda baraza la mitihani ukachukue barua kuthibitisha hilo. Kwenda baraza la mitihani wakasema huweza kwenda form three mpaka ufanye mitihani ya Form Two upya. Huyo bwana mdogo akaamua kuachana na masuala ya shule aendelee na maisha yake mengine. Nimetoa huu mfano kuonyesha jinsi viongozi wasivyoona jinsi wanavyojenga taifa la wajinga kwa kutowajibika kwao. Sasa hao watoto 240,000 wanakwenda wapi? Kama siyo kuanza kufuga majambazi na machangu.
Pasco watu wengi, hawataona ulichosema, lakini hawa viongozi lazima waje na maelezo ya kutosha kuhusu sababu hizi zote. Vinginevyo they have to go.

Pia waangalie cha kufanya. Kwangu mimi kuna mambo mawili tu:
1. Mitihani isahihishwe upya
2. Mitihani itungwe upya na wanafunzi wafanye tena. Hili si mara ya kwanza maana mitihani ya Mwaka 1998 (kama sikosei) ilirudiwa mwaka 1999 baada ya kuona kuwa kuna udanganyifu mkubwa.

Samahani wadau nimeandika sana.
 
Wanabodi,

Kwa maoni yangu, kitendo cha NECTA kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio NECTA, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.

Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa NECTA utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.

Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.

Kibonde anahusikaja apo?!
 
Pasco! Baraza la mitihani haliandai mitaala! Halifundishi.baraza ni wakala wa serikali wa kufanya sumative assessment kwaajili ya kutoa vyeti, baraza hufanya assessment kulingana na vile client wake(wizara ya elimu) .alivyoonyesha kuwa alifundisha nini kwa hao wAtahiniwA. Kama wizara inaweza kuthibitisha kuwa baraza lilitahini tofauti na mtaala /mwongozo basi ndalichako aaadhibiwe
 
Wanabodi,

Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.

Mkuu Pasco, unapaswa kumpa Hongera Mama Ndalichako kwa kudhibiti wizi wa mitihani na kutunga mithani kwa kufuata syllabus zinazopaswa kufundishwa katika shule za Sekondari Tanzania. Kama wanafunzi hawakusoma sio kosa la NECTA, bali ni la yule anayesimamia hizo shule. Kama NECTA ingekuwa ndio Wizara Mama, huenda wangetunga mitihani rahisi unayoisema wewe ili kufurahisha Umma, jambo ambalo lingekuwa baya zaidi maana wanafunzi hao wangefel zaidi kidato cha sita au tungepata viongozi mbumbu baadaye. Watoto wa wenye nacho unaosema wamefaulu ni kwa sababu wamesoma kwenye shule ambazo zinafundisha vizuri na kuwajali walimu wake. Kazi ya kusimamia ufundishaji mzuri na kuwajali wali ili wawe na moyo wa kujituma na kufundisha vizuri sio kazi ya Joyce, ni kazi ya Wizara Mama. Joyce anatumika kama kupimo ili kuthibitisha ubora kazi inayofanywa na Wizara ya Elimu. HONGERA DR. NDALICHAKO.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapa kwa kweli ume-press wrong key!kwani hiyo mitihali si ilikuwa reviewed bfore madogo hawajafanya?unataka kutuambia NECTA wana mitaala mingine na Shule wao wanayo mingine?
C'mon Pasco, hebu Chui na aitwe Chui na sio kumbatiza eti Nyau mkubwa...wewe hujui shule za kata hazina walimu wala vitendea kazi? Na kama hiyo haitoshi,walimu wanalipwa vizuri?si kila siku mnawabeza!niambie mkuu katika watumishi wote wa serikali wanaolipwa low kabisa ni nan kama sio walimu...halafu eti mnasema ooh ualimu ni wito...kwa hiyo hata mtoto wa mwalimu ana wito??
Tatizo ni wizara,big up sana kwa NECTA,hii ndio tunataka,kusimamia maadili na kuacha siasa..maana kama NECTA wangekuwa kama TBC then tungeambiwa 90% wamefaulu! Safi Sana Ndalichako,kaza buti mama hatutaki wasomi Vilaza!
For ur information,kuna wanafunzi form 2 hawajui hata kusoma vizuri..anayebisha aseme na shule tumtajie!
 
hapo umenena, haiwezekani hata shule tulizoea kufaulisha zkafeli, kwani watu weng kwa sasa wanalaum migomo ya walim lakn tujiulize swali la pili je hata shule za binafsi kulikuwa na mgomo?? Je ni kwel wanafunzi na walim hawana akili? Je tugeuzie macho upande wa pili kumekuwa na mambo yanayofanyika kimchezomchezo, angalia suala la mikopo kwa watu wanaochukua taaluma ya ualim, je ni kila mtu awe mwalimu? Hapa ina maana baadhi ya watu kutokana na watu kuwa na maisha magum anaenda kukidhi mahitaji, fatilia kwa umakini utaona baadhi ya watu wanabadilisha fani katikat ya safar ama anabadl mda akpata hela na kwenda anapotaka. Hili ni janga la kitaifa, tena si mchezo
 
katika maisha yangu sikuwahi kuona mtu wa ajabu kama wewe Pasco
nina maswali muhimu nataka nikuulize wewe kijana
1.je ulitaka mitihani ya namna gani watungiwe hawa vijana?
2.kwa nini wengine wamefauli kama hiyo mitihani siyo?
3.je ndalichako ana link gani directly na wanafunzi na mitihani yao?
nikutaarifu tu.
4,kwanini matokeo ya mwaka huu kuanzia formart na kila kitu yamekinzana sana na matokeo yote hapa nchini yaani yamekuwa tofauti?

NOTE:
1.hakuna kitu kibaya kama kuingiza mambo ya siasa ,udini na upendeleo katika mambo au jambo muhimu kama AFYA NA ELIMU.mark my word !!!.
2.walimu wana malalamiko yao serikali imepuuzia ,zimejengwa shule nzuri za kata hamna nyumaba za walimu za kuishi kwanini walimu wasikimbie ,
3.Binafsi nasema kuwa mmoja afe kwa ajili ya wote nimefurahishwa na matokeo haya sanatena sana sababu jamii na serikali imetupilia suala la elimu porini tupate pakuanzia kwa ajili ya jamii inayofuata tukiendelea kupuuza haya haya yataendelea .ilizoeleka wanafaulu tu kwa standardazation sasa hivi hamna ni computarization .
mwisho.mimi nimesima shule hizi za serikali kuanzia kidudu mpaka chuo kikuu ,hata siku moja baba yangu hakuwahi niuliza nafundishwa nini alikuwa anataka riportform na niwe nimefaulu period!!nafundishwa sifundishwi yeye alikuwa halijui hilo juhudi binafsi zinahitajika wazazi wengi wamekuwa wakiwakingia nakuwaaminisha kuwa wanafelishwa,wacha msumeno ukate pande zote Pasco ili tutie akili.
 
Pia waangalie cha kufanya. Kwangu mimi kuna mambo mawili tu:
1. Mitihani isahihishwe upya
2. Mitihani itungwe upya na wanafunzi wafanye tena. Hili si mara ya kwanza maana mitihani ya Mwaka 1998 (kama sikosei) ilirudiwa mwaka 1999 baada ya kuona kuwa kuna udanganyifu mkubwa.

Samahani wadau nimeandika sana.

Hakuna sababu ya kusahihisha mitihani upya, labda kama watoto wote wangekuwa wamefeli,lakini hapa wengine wamefalu. Wala hakuna sababu ya kufuta matokeo, kwa sababu mitihani haikuibiwa. Wizara ya Elimu imepeleka wanafunzi ambao hawakuandaliwa vizuri kwa maana ya kufundishwa vizuri. Je, mitihani ikitungwa upya wanafunzi watakuwa hao hao au wengine ? Ina maana lengo ni kwamba wafaulu na sio aina ya watu wanaofaulu; ni elimu bora au bora elimu ?
 
Mkuu Pasco, unapaswa kumpa Hongera Mama Ndalichako kwa kudhibiti wizi wa mitihani na kutunga mithani kwa kufuata syllabus zinazopaswa kufundishwa katika shule za Sekondari Tanzania. Kama wanafunzi hawakusoma sio kosa la NECTA, bali ni la yule anayesimamia hizo shule. Kama NECTA ingekuwa ndio Wizara Mama, huenda wangetunga mitihani rahisi unayoisema wewe ili kufurahisha Umma, jambo ambalo lingekuwa baya zaidi maana wanafunzi hao wangefel zaidi kidato cha sita au tungepata viongozi mbumbu baadaye. Watoto wa wenye nacho unaosema wamefaulu ni kwa sababu wamesoma kwenye shule ambazo zinafundisha vizuri na kuwajali walimu wake. Kazi ya kusimamia ufundishaji mzuri na kuwajali wali ili wawe na moyo wa kujituma na kufundisha vizuri sio kazi ya Joyce, ni kazi ya Wizara Mama. Joyce anatumika kama kupimo ili kuthibitisha ubora kazi inayofanywa na Wizara ya Elimu. HONGERA DR. NDALICHAKO.

Unaweza kuthibitishaje kuwa walitunga mitihani kutokana na syllabus? Unajua kuna madudu mengi sana katika sekta ya elimu (hapa ikiwemo Wizara na Baraza lake la Mitihani), hivyo tukiwa wakweli mioyoni mwetu na kuacha kuwajadili vibaya tusiowapenda na kuwajadili vizuri tunaowapenda tutaisaidia sana nchi yetu.
 
Wanabodi,

Kwa maoni yangu, kitendo cha NECTA kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio NECTA, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.

Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa NECTA utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.

Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.
Naungana nawewe kamanda ,inashangaza kuona kwamba mtihani huu wa mwisho ndio unapewa uzito mkubwa kuliko maendeleo ya mtoto akiwa darasani na mwalimu
Haingii akilini mwanafunzi afundishwe na mwalimu asiye na vifaa /nyenzo na motisha, halafu mwanafunzi aje apewe mtihani na NECTA (wenye mazingira mazuri ya kazi,vitendea kazi,motisha nk,hata kama watajitetea kua walimu wanaitwa kutunga na kusahihisha mitihani ,something must be wrong)

Hapa kuna tatizo kubwa sana ,uchunguzi wa kina unatakiwa ufanyike kuhusiana na hili swala, la sivyo hivi visasi vya NECTA vitalipeleka taifa shimoni
 
3. Utendaji mbovu wa Baraza la Mitihani
3.1. Kutunga mitihani ambayo haiendani na mihutasari waliyopewa walimu kufundisha na wanafunzi kusoma (nakumbuka wakati nasoma Sekondari, nilisoma Book-Keeping na kulikuwa na kitabu kinaitwa Book Keeing for Tanzania Secondary Schools kama sikosei ambacho kilikuwa kinatolewa na Wizara ya Elimu, lakini hata siku moja hutapata swali kutoka ndani ya hicho kitabu. Maswali karibu yote yalikuwa yanatoka kwenye Frank Wood-Business Accounting ambacho wakati huo kukipata ilikuwa mbinde)
3.2. Kutokuwa makini katika usahihishaji

Ndugu Mkodoleaji, ukikodoa sawa sawa utaona maelezo yako hapo kwenye RED na mfano ulioutoa vinahitilafiana!! Unadhani mitihani ingetungwa nje ya Muhtasari hayo maandamano yangezuilika???

La hasha. Sidhani kama kuna swali lilitoka nje ya Muhtasari na kama kuna mwenye ushahidi aweke humu. Pili unanishangaza unapotaka eti mitihani itungwe toka kwenye kitabgu/vitabu fulani...Nadhani cha msingi ni kuzingatia mada zilizopo kwenye muhtasari na maarifa anayotakiwa kuwa nayo mtahiniwa wa level hiyo. issue sio kitabu!!
 
Last edited by a moderator:
pasco umeongea point ambayo watu wengi hawataki kuiona.
Kwangu mimi suala si dr ndalichako tu, ila hata waziri kawambwa na viongozi waandamizi have to go. Hatukatai kuwa kuna watoto ambao hawasomi, hilo tunalijua maaana wote tumesoma sekondari. Sasa sababu za kufeli haiwezi kuwa moja tu ya uzembe wa wanafunzi.

Sababu zinaweza kuwa zifuatazo:
1. Uzembe wa wanafunzi
2. Mfumo mbovu wa elimu
2.1. Kutokuwa na mitaala ya kueleweka
2.2. Kuwa na shule bila walimu
2.3. Kutokufanya ukaguzi wa kutosha
2.4. Kutokuwa na motisha kwa walimu
2.5. Kutoboresha shule za kata n.k.
3. Utendaji mbovu wa baraza la mitihani
3.1. Kutunga mitihani ambayo haiendani na mihutasari waliyopewa walimu kufundisha na wanafunzi kusoma (nakumbuka wakati nasoma sekondari, nilisoma book-keeping na kulikuwa na kitabu kinaitwa book keeing for tanzania secondary schools kama sikosei ambacho kilikuwa kinatolewa na wizara ya elimu, lakini hata siku moja hutapata swali kutoka ndani ya hicho kitabu. Maswali karibu yote yalikuwa yanatoka kwenye frank wood-business accounting ambacho wakati huo kukipata ilikuwa mbinde)
3.2. Kutokuwa makini katika usahihishaji
4. Kutowajibika kwa nchi (uzembe wa viongozi) (viongozi hawajui kuwa wanatakiwa kulijenga taifa hili kwa kupitia elimu). Nakumbuka kuna bwana mdogo ambaye alishindwa kuendelea na shule akiwa form three kutokana na uwezo mdogo. Baada ya miaka kadhaa ya kujishughulisha na biashara akapata fedha akataka kurudi shule ili aendelee. Ile shule aliyokwenda ili ajiendeleze kama private candidate akaambiwa alete barua toka ile shule aliyokuwa anasoma. Ile shule aliyokuwa anasoma wakampa barua, kwenda kwenye shule mpya wakamwambia aje na matokeo ya form two akawajibu kuwa mwaka wao mitihani ya form two ilikuwa imefutwa, ili ilikuja kurudishwa baadaye. Wakamwambia nenda baraza la mitihani ukachukue barua kuthibitisha hilo. Kwenda baraza la mitihani wakasema huweza kwenda form three mpaka ufanye mitihani ya form two upya. Huyo bwana mdogo akaamua kuachana na masuala ya shule aendelee na maisha yake mengine. Nimetoa huu mfano kuonyesha jinsi viongozi wasivyoona jinsi wanavyojenga taifa la wajinga kwa kutowajibika kwao. Sasa hao watoto 240,000 wanakwenda wapi? Kama siyo kuanza kufuga majambazi na machangu.
Pasco watu wengi, hawataona ulichosema, lakini hawa viongozi lazima waje na maelezo ya kutosha kuhusu sababu hizi zote. Vinginevyo they have to go.

Pia waangalie cha kufanya. Kwangu mimi kuna mambo mawili tu:
1. Mitihani isahihishwe upya
2. Mitihani itungwe upya na wanafunzi wafanye tena. Hili si mara ya kwanza maana mitihani ya mwaka 1998 (kama sikosei) ilirudiwa mwaka 1999 baada ya kuona kuwa kuna udanganyifu mkubwa.

Samahani wadau nimeandika sana.
mkuu hakuna udanganyifu katika mitihani hii ,jiulize kwanini wengine wamefaulu??? Kuna shule ya serikali ya kata mtaani kwangu na imefaulisha na hamna walimu jiulize?juhudi binafsi zinahitajika as a student.
 
Hakuna sababu ya kusahihisha mitihani upya, labda kama watoto wote wangekuwa wamefeli,lakini hapa wengine wamefalu. Wala hakuna sababu ya kufuta matokeo, kwa sababu mitihani haikuibiwa. Wizara ya Elimu imepeleka wanafunzi ambao hawakuandaliwa vizuri kwa maana ya kufundishwa vizuri. Je, mitihani ikitungwa upya wanafunzi watakuwa hao hao au wengine ? Ina maana lengo ni kwamba wafaulu na sio aina ya watu wanaofaulu; ni elimu bora au bora elimu ?

Elimu bora ni ipi? Unaweza kuthibitisha kwamba wote waliopata sifuri hawajaelimika? Suala hapa ni kuangalia suala la mitihani na lengo la kuwajenga watoto kitaaluma. Kama huna walimu, wanafunzi wanababia katika kusoma tafuta mbinu za kuwatahini watoto kutokana na kile wanachokipata. Huwezi kuchukua mitihani ya uingereza na kuileta hapa kisa syllabus ni moja wakati mwanafunzi hajawahi kufundiswa hiyo syllabus. Sasa Baraza la Mitihani siyo tu kijiwe cha kutunga mitihani, bali linatakiwa lisaidiwe kuishauri Wizara namna muafaka ya kuwatahini watoto katika mfumo wetu wa utoaji elimu.
 
Pasco. Hata kama mdogo wako amefeli huwezi mlaumu Ndalichako,ilaumu serikali yenu ya magamba kwa kutokuwekeza kwenye elimu.
 
Last edited by a moderator:
kuna kutunga mtihani mgumu na kuna kutunga mtihani ambao sio ili kuwakomoa kina fulani!.
Pasco unaeneza udini hapa watch ua mouth ,katika mambo muhimu toa udini.unamaanisha hamna hao kina nanii waliofaulu???? Na kama kweli nikuwakomoa kwanini wakakomeleka kama walikuwa fit??? So baraza la mitihani limeprove kuwa there is something wrong katika hao watu fulani !!prove it pasco la sivyo i wll sue u acha ujinga wakutuaminisha haya
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom