Mkodoleaji
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 458
- 138
Daima watunga mitaala huwa wanatoa vitabu vya aina mbili; vitabu vya kiada na vya ziada (text books and reference books). Mtunga mitihani anachojali wakati wa kutunga mtihani ni concept iliyopo kwenye syllabus, kama kwenye syllabus watoto wanajifunza osmosis, mtunzi wa mtihani atatafuta sweli linalohusiana na concept ya osmosis kulingana na level ya mtoto. Hatatunga swali la form six akalileta kwa form four. Na uzuri ni kwamba utunzi wa maswali ya mitihani haufanywi na mtu mmoja. Random sample ya walimu kutoka mashuleni plus representative wa TIE huwa wanaparticipate. So mtu kukaa chini na kuanza kumrushia mawe Ndalichako, ni kutafuta visingizio visivyo na maana. Ukweli ni kwamba curriculum implementation haikuwenda sawa, walimu wapo kwenye Mgomo. Pasco asitake kukwepa ukweli. awaambie wakubwa wake kwamba walimu wapo kwenye mgomo, serikali itafute namna nzuri ya kusikiliza matatizo ya walimu.
Lukolo nakubaliana na wewe kwa maelezo uliyoyatoa, lakini kitu kimoja ufahamu matokeo ya mitihani ni zao la Baraza la Mitihani. Matokeo yakiwa mabaya watu watalalamikia Baraza la Mitihani. Kwa nini basi inakuwa ni kwa sababu Baraza ndio linalochagua watungaji, baraza ndilo linachagua wasahihishaji na baraza ndilo linatoa mitihani. Sasa kama syllabus haikutekelezwa yote, mitihani ingetungwa kutokana na kile kilichotekelezwa. Huwezi kutunga nje ya kile kilichofundishwa na kuwaita watoto wamefeli, watu watasema umewafelisha.
Sasa kama ulivyosema kumvagaa Ndalichako peke yake kwa kweli siyo sahihi maana mfumo mzima wa elimu una matatizo na ndiyo maana hata mitaala haikutolewa bungeni. Hivyo kuna haja kabisa ya kuufumua mfumo mzima wa elimu ili kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata elimu iliyo bora

