





Eti wana wa Tanzania hawakufaulu kwa kiwango kinachotakiwa! zaidi ya asilimia 60 wamepata sufuri kwa maana ya alama zilizowekwa ktk kila swali, kwa maana nyingine walizopata hazikutosha! lakini wamepata ila awamo ndani ya mshindi wa 1 - 4 (madaraja).
Ebu tujiulize, ni mitihani gani wanapewa wana wa Tanzania? Hii mitihani inausiana vipi na changamoto tulizonazo kwa sasa; kiuchumi, Kisiasa, kiimani, na kijamii kwa ujulma? Inamaana hao 60% hawafai, hawanamaarifa yoyote?
Je, ili sio tatizo la mfumo wa elimu yetu?!
Je, waliofaulu ni kweli wamepata ujuzi wa kutatua changamoto zilizopo au wamepata alama nyingi ktk kila swali?
Je, mfumo wa maswali ya kuchagua tunautamzamaje, hauna uhusiano na matokeo haya?
Je, ambao hawakufaulu mwaka 2011 wako wapi, na wa mwa 2012 wanaelekea wapi, na wa 2013.....????
Kama chakula kimepikwa lakini hakikuiva inavyotakiwa, kinafaa kutumika? Je, nani alaumiwe: Kuni/mkaa/gasi, maji, chungu/sufuria, jiko, MPISHI, au mazingira/system inayotawala kanuni za upishi?