Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Of all the people ndugu Pasco unatoa hii, naamini wamekuibia password na kupost hii kitu.
 
plz kabla ya kuandika chochote fikiri kwanza mm na masters pia ni mwalimu mitihani waliyofanya f4 ni saizi yao hakuna kilichotolewa nje ya mada zao.....kwa ujumla wanafunzi wengi wao ni wazembe hawapendi kujisomea.
 
Of all the people ndugu Pasco unatoa hii, naamini wamekuibia password na kupost hii kitu.

We unamfahamu sana hadi uone si Pasco aliyeandika? si ndio huyu huyu huwa anaona kuwa ccm ni watawala wazuri? kawambwa ndio!
 
Last edited by a moderator:
Ufaulu wenyewe siyo huo tulioutegemea, nimejaribu kufuatilia shule nyingi sikuona point 7 au 8. Hata watoto waliofaulu bado wengi wao hawaamini kilichotokea. Ukitaka kuelewa vizur zitafute shule zilizoingia top ten mwaka huu halafu angalia na top ten ya mwaka jana ndo ulinganishe matokeo ya mwaka huu na ya mwaka jana. Sitetei wabovu ila kitenndo cha point 7 & 8 kutokuonekana kinanipa wasi wasi.
malalamishi ya wazazi wao ndio yamepelekea anguko hilo.hakuna standardisation iliyofanyika na mitihani ilisahishwna systems ,hakuna huruma ya aliyekuwa anakaribia jibu au la kilichotakiwa ni jibu sahihi tu upate maksi.tatizo kubw ani secta binafsi zilizoingilia secta ya elimu nakutaka wafanye kam wao watakavyo kitu ambacho si sawa wjipange upya .unataka wqafaulishwe kama wale darasa la saba wanafika form 2 hawajui kusoma nkauandika?
 
Baadhi ya Wahandishi wa Habari epukeni kufikiria kwa kutumia masaburi!
Kusema za ukweli nilimheshimu Pasco ila hii sredi imenishangaza kweli. Hebu Pasco ikarabati ili ikufanane. Ukipata ujumbe usioufurahia katika barua iliyotumwa kupitia posta, utalaumu posta au mwandishi?
 
Sikubaliani nawe Pasco kwa hili. Tangu ameingia Dr. J. Ndalichako hapo NECTA wizi wa mitihani hamna. Kabana kona zote. Je ni yeye anayefanya wanafunzi wakose learning materials, facilities, walimu wakose teaching morale etc zinazosababisha vijana wafeli. Tutafute mzizi wa tatizo then tuchukue hatua!
Githeri wewe jembe!
 
ndugu yangu sikubaliani na wewe. mwalimu anapotunga mtihani shuleni, lazima ajiulize kuwa syllabus imefundishwa hadi wapi. akitunga mtihani wa muhula wa kwanza, itakua ajabu akiweka topics ambazo hajazifundisha. zinafaa kufundishwa
muhula wa pili. huo ndiyo upimaji (evaluation)

ile formula ya kcaase kwa waliyo chukua ualimu wanaelewa umuhimu wake. kugawa maswali kwa 25. 50 na 25% kama nilivyo andika awali ni muhimu sana. kwa mwalimu bora, akipelekwa senegal kutunga mitihani, hawezi kukurupuka kutunga kabla ya kuzingatia vipengele vingi. baadhi yake ni kuuliza kama hapajatokea mafuriko au vita au janga lolote lililofanya syllabus zisifundishwe kwa ukamilifu, maabara zipo mashuleni, ufaulu wa mwaka uliopita ulikuwaje, nk......

ufaulu mzuri ni ule ambao umekaa kama bakuli lilofunikwa. pande za pembeni ziko chini na upande wa katikati uko juu. namaanisha kuwa wanaofaulu kwa division 1 wachache, wanaopata div 11 na 111 wengi, na wale wa iv na 0 wachache. mwaka huu wa iv na 0 ndiyo wengi! hii ni hatari. sababu zitafutwe naamini ni nyingi lakini lazima waliyotunga nao wana swali la kujibu. dkt. ngalichako ajiuzulu
Sawa umesema vyema kwani hao NECTA wametunga mtihani nje ya silabasi ya o, level?au ulitaka waangalie kitu gani
 
Ufaulu wenyewe siyo huo tulioutegemea, nimejaribu kufuatilia shule nyingi sikuona point 7 au 8. Hata watoto waliofaulu bado wengi wao hawaamini kilichotokea. Ukitaka kuelewa vizur zitafute shule zilizoingia top ten mwaka huu halafu angalia na top ten ya mwaka jana ndo ulinganishe matokeo ya mwaka huu na ya mwaka jana. Sitetei wabovu ila kitenndo cha point 7 & 8 kutokuonekana kinanipa wasi wasi.
Mkuu kwani wapi imeainisha lazima kila mwaka zipatikane points 7 au 8 ndio kiwe kipimo cha ufaulu, kuna miaka ya nyuma kwa A, level points 3 ilikuwa inatamkwa tu ila kupaikani ilikuwa ishu
 
malalamishi ya wazazi wao ndio yamepelekea anguko hilo.hakuna standardisation iliyofanyika na mitihani ilisahishwna systems ,hakuna huruma ya aliyekuwa anakaribia jibu au la kilichotakiwa ni jibu sahihi tu upate maksi.tatizo kubw ani secta binafsi zilizoingilia secta ya elimu nakutaka wafanye kam wao watakavyo kitu ambacho si sawa wjipange upya .unataka wqafaulishwe kama wale darasa la saba wanafika form 2 hawajui kusoma nkauandika?

Mkuu ndio maana nikasema kua sitetei wajinga, wasiwasi wangu yawezekana kukawa na kitu ambacho kinaendelea sisi hatukijui lakini kinatugharimu. Sakata la Islamic knowledge lilimlenga Ndalichako moja kwa moja lakini yasemekana kuna watu walimtega kwa maksudi ili ionekana kua anahusika, na ndio maana serikali baada ya kufanya utafiti ikagundua kua hakua na hatia(ulikua ni mpango maalum wa kumchonganisha na jamii fulani). Ndani ya NECTA kuna watu wana matatizo na wanajua wazi kua anaebeba mzigo ni Ndalichako. Ninachoweza kusema(ninavyoona mimi) ni kua NECTA kuna tatizo na tatizo lenyewe ni zaidi ya Ndalichako mwenyewe.
 
je hilo tatizo limeanza kujitokeza hii 2012???kwanini sio long time .nafikiri kila aliyepata ilikuwa ni sahihi kwake na NECTA haina tatizo ,sehemu nyeti zimekaliwa na hawa jamii fulani sas wanataka na huko NECTA wawepo ili wafanye mambo yao ya upendeleo.
NINAHAKIKA NECTA HAINA TATIZO TATIZO NI WANAFUNZI WENYEWE KILA MWAKA WANABEBWA NA STANDADIZATION SASA HAIKUWEPO BASI CHALIIII WANAONA SHIDA,LAWAMA JE WAZIRI WA ELIMU HAPASWI KULAUMIWA?KATI YA KAWAMBWANA NDALICHAKO NANI ANA DIRECT IMPACT NA WATAHINIWA????MSIMTWIKE DDA WA WATU FEDHEHA ALISOMESHWA NA WAZAZI WAKE NDIO SABABU YUKO PALE NA KIUTENDAJI YUPO VIZURI THATS WHY SHE IS THERE.
 
Mkuu kwani wapi imeainisha lazima kila mwaka zipatikane points 7 au 8 ndio kiwe kipimo cha ufaulu, kuna miaka ya nyuma kwa A, level points 3 ilikuwa inatamkwa tu ila kupaikani ilikuwa ishu

Mkuu siku hizi mazingira ya kusoma ni tofauti na ya zamani.
 
Mkuu siku hizi mazingira ya kusoma ni tofauti na ya zamani.
Nakubaliana na wewe mkuu ila hayo mzaingira ndio yanachangia kuwaharibu wengi badala ya kuyatumia vizuri yawasaidie wamekuwa na mambo mengi kuliko hata walezi wao,inawezekana moja ya kuongezeka kufail kwao ni kutotumia vizuri technologia
 
Naogopaga kuwabishia waandishi wa habari na watangazaji kwa sababu wanaonekana kuwa na akili nyiiingiiii!

Sijawahi kujiuliza kama hii kazi unaisomea ukiwa na Div gani? Je ni % gani ya waandishi walipata Div I O-level na A-level.

Isije ikawa mtu kaandika kinachomhusu "nilifeli kwa sababu pepa ilikuwa siyo".
 
Pasco unaingia kwenye mtego wa kwamba mtihani ulikuwa mgumu?? kisa watoto wako wamefeli?
Wewe mwenyewe mtoto wako alikuambia mtihani ulikuwa mrahisi,iweje sasa hivi usema NECta walitungabmtihani mgumu??

Msitafute visingizio visivyo na maana,msijifanye kama hamuoni tatizo la Elimu kushuka ni nini?

Mbona mnajifanya kutoona utendaji wa serikali towards elimu?

Nikuambie ukiiongea na wanafunzi wengi wanasema mtihani ulikuwa fair sana,mfano Civics kulikuwa na swali la kwanza What is the importance of Civics? Ugumu huu waapi bwana Pasco,kama mwandishi mkongwe kama wewe unaandika haya basi sishangai kwanini watoto wako wamefeli.

Msitafute pa kutokea,wizara yenye dhamana ndio wa kuanza kuwanyooshea kidole,husipepese macho na kuanza kuandika upuuzi wenu kwa kuipeperushia serikali lawama hizi.

Wewe muandishi Pasco,ulifuatilia majibu ya kidato cha pili miaka miwili iliopita

Wana JF Pasco ni mtu mbaya sana,mchochezi mkubwa mnajua hilo kundi analoliita "watu fulani" ni wakina nani? mmeshalijua mnakumbuka sakata lao last year PAsco anajua kundi hilo wasivyo na subira na uwezo usio mkubwa kufikiri ndio maana kalenga kwenye kundi hilo awawashe hasira.
 
Mkuu Fidelity, sijutii uamuzi wangu kusomesha vijana wangu shule za kata, bali naumizwana kijana wangu kichwa wa hisabati, kupata daraja C.

Mwaka juzi, binti yangu last but one, aliomba kujiunga St. Marian Girls nini nikamgomea wife akawasha moto, hadi kumpeleka kufanya usahili, matokeo alikosa, alilia sana baada ya kuambia cut off point ni makisi 150/200. Akamthibitishia mama yake kuwa amedhulumiwa, hawezi kukosa average ya 75 kwa mitihani mitatu waliofanya!, binti analia tuu, hatimaye nikakubali, mimi, binti na mama, hao Bagamoyo kwa mkuu wa shule, tuki demand kuona matokeo halisi ya mwanetu!.

Kwanza tulikataliwa, nilipoeleza sababu nyeti nilizozisikia kuhusu selection ya St. Marian, Mkuu wa shule akanikubalia, ikaitishwa file, narking scheme na pepa za mwanangu, wamefanya pepa 4. hesabu, sayansi, Kiingereza na maarifa!. Kila pepa maswali 50 na kila swali makisi 1. Cut of point ni makisi 150/200. Binti kapiga 42, 32, 38 na 36. Total ni zaidi ya 150/200 hivyo ni over and above ile cut off point yao, kuuliza sasa kwa nini hakuchaguliwa, nikaletewa hadithi!.

Kufuatia matokeo haya mabaya, wale wazazi tunao waaminia wenetu, hatuwezi kukubali hili likapita hivi hivi tuu!.
Mimi ni kama Tomaso, sikubali mpaka nione pepa moja tuu, ya hesanu ya kijana wangu!. Kiukweli, pamoja na mengine yote, " The games that NECTA plays on poor people!, its very dangerous gamea!".
Pasco.
Ukisifiwa unajua kukimbia utapita kwenu
 
Mawazo mgando. Mdogo wangu mwenyewewe kafail na si wa upande huo. Nyie watu nyie?
Wanabodi,

Kwa maoni yangu, kitendo cha NECTA kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio NECTA, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.

Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa NECTA utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.

Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.

I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.

Pasco.
 
minadhani tuandamane atoke kawambwa au mnasemaje mazee

Huyu Kawambwa has failed in all the positions that his relative [who happens to be the President] has given him undeservedly!! Huyu ndio wa kutimuliwa kwani amehatalisha uhai wa Taifa na sio Dr. Ndalichako. Wasitafute mchawi kwani anajulikana.
 
quote_icon.png
By Pasco Mkuu Fidelity, sijutii uamuzi wangu kusomesha vijana wangu shule za kata, bali naumizwana kijana wangu kichwa wa hisabati, kupata daraja C.

Mwaka juzi, binti yangu last but one, aliomba kujiunga St. Marian Girls nini nikamgomea wife akawasha moto, hadi kumpeleka kufanya usahili, matokeo alikosa, alilia sana baada ya kuambia cut off point ni makisi 150/200. Akamthibitishia mama yake kuwa amedhulumiwa, hawezi kukosa average ya 75 kwa mitihani mitatu waliofanya!, binti analia tuu, hatimaye nikakubali, mimi, binti na mama, hao Bagamoyo kwa mkuu wa shule, tuki demand kuona matokeo halisi ya mwanetu!.

Kwanza tulikataliwa, nilipoeleza sababu nyeti nilizozisikia kuhusu selection ya St. Marian, Mkuu wa shule akanikubalia, ikaitishwa file, narking scheme na pepa za mwanangu, wamefanya pepa 4. hesabu, sayansi, Kiingereza na maarifa!. Kila pepa maswali 50 na kila swali makisi 1. Cut of point ni makisi 150/200. Binti kapiga 42, 32, 38 na 36. Total ni zaidi ya 150/200 hivyo ni over and above ile cut off point yao, kuuliza sasa kwa nini hakuchaguliwa, nikaletewa hadithi!.

Kufuatia matokeo haya mabaya, wale wazazi tunao waaminia wenetu, hatuwezi kukubali hili likapita hivi hivi tuu!.
Mimi ni kama Tomaso, sikubali mpaka nione pepa moja tuu, ya hesanu ya kijana wangu!. Kiukweli, pamoja na mengine yote, " The games that NECTA plays on poor people!, its very dangerous gamea!".

Pasco.

Kazi ya uandishi wa habari ni kipaji na sio shule (wao wanavyodai), waandishi wengi wa habari tulionao ni baadhi tu ya watu waliofeli mitihani yao ya NECTA form IV na VI.

Ndio maana kila kukicha tunaona madudu kwenye tasnia hii ya habari, tunawaita makanjanja, wachumia tumbo etc. Inshort kama ulifeli mitihani na hukujua kwa nini ulifeli wewe ni felia mbaya, na hii ndiyo inamwathiri mwanzilishi wa topic.

Please, advise your kids to work hard.
Kukiwa na cut-off ya 150%, tukawa tunahitaji watoto 80, kama 85 wamepata zaidi ya 150%, then tutachukua top 80, so mwanao atakuwa kwenye waiting list.
Enzi zetu tulikuwa na lugha ya umefaulu lakini hukuchaguliwa, unaielewa hii? Maana yake uko above average lakini nafasi ziko limited.
 
Pasco unaingia kwenye mtego wa kwamba mtihani ulikuwa mgumu?. Ugumu huu waapi bwana Pasco,kama mwandishi mkongwe kama wewe unaandika haya basi sishangai kwanini watoto wako wamefeli.

Wewe muandishi Pasco,ulifuatilia majibu ya kidato cha pili miaka miwili iliopita

Wana JF Pasco ni mtu mbaya sana,mchochezi mkubwa mnajua hilo kundi analoliita "watu fulani" ni wakina nani? mmeshalijua mnakumbuka sakata lao last year PAsco anajua kundi hilo wasivyo na subira na uwezo usio mkubwa kufikiri ndio maana kalenga kwenye kundi hilo awawashe hasira.
.
Mkuu Nokia Tochi, kwanza asante kwa posti hii, wewe uu mmoja kati ya wengi "who can read in between the line!". Nchi hii ukiwa mkweli sana huitwa "mchochezi!", hivyo sishangai!. Swali langu kwako ni jee is it fair kwa hilo kundi la "watu fulani?!", jee unaweza kufanya utafiti hao 60% waliozungusha ni kina nani?!, ukiwajua, huu utakuwa ni ukweli mchungu!. Niite mchochezi ila ukweli ndio huo!, kama hatutaukubali ukweli huu, haya yanayoendelea sasa ni rasharasha tuu, na ni dalili ya mawingu, mvua zinakuja!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom