Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Pasco,

Nikijumlisha hapo kwenye bluu napata jumla ya alama 148......! Kwa maana hiyo binti yako hakufikisha alama 150!
Halafu anashindwaje kuelewa kuwa passmarks sio kigezo cha mwisho cha kuchagua, kama wapo waliofanya vizuri zaidi ya huyo mtoto wake je?
 


Sijui umequote vipi maelezo yangu kiasi kwamba umeyachanganya na yako ila nimekusoma kuwa unataka mitihani iwe diluted kisa ufundishaji ni duni kwa baadhi ya shule....aisee....Sasa hizi percentage za level of difficult umezitoa katika theory gani ya assessment nasi tufaidike na huo mchanyato wa 25% magumu, 25% marahisi na 50 ya kati?

Je kwa analysis yako mtihani uliopita, mchnganuo ulikuwaje kwa kila somo? Kumbuka kuna masomo zaidi ya 30....
 
Wewe pasco
msitafute kumsingizia ndalichako
unadhani 'malalamiko' ya walimu yanatoa matokeo memaa?
Unasahau kila siku wakidai haki zao wanakejeliwa kwa kuitwa 'mbayuayu\?
Unakumbukumbu dhaifu sana kama umeshasahau.....

Usisahau walimu mbali ya kulilia maslahi yao...wanalilia vifaa vya kufundishia havipo...

Usisahau sasa hivi watoto hawana adabu kwa walimu; nadhani kama na wewe ni 'mzazi' utafanana na walewale ambao mtoto akiadhibiwa kwa utovu wa nidhamu...mwalimu anafungiwa kibwebwe na kupewa mkong'to....habari iliyotokea kigoma wiki hii hii (je nidhamu mbovu za watoto ambazo wanafundishwa na wazazi wao' unadhani zinamwezesha mtu kupata div 1,2,3...ni failures tu....
 
NECTA wanapotunga mitihani, lazima wazingatie mambo mengi. waelewe kuwa kuna shule hazina walimu wakutosha, maabara, nk...... lazima kuwe na 25% ya maswali mepesi sana, 50% ya maswali ya kati na 25% ya maswali magumu.

Mkuu wangu hii ndio tunaita kuingiza siasa kataika taaluma. Si wajibu wa NECTA kujua kama shule hazina walimu wa kutosha, maabara nk......ni jukumu la idara zingine za serikali pasi na kukumbukla kuwa mitihani si kwa shule za serikali tu....mantiki ya kuppozesha mitihani kwa asilimia ulizoweka sijaielewa.....nijuavyo mitihani inatakiwa kulingana na mitaala iliyopo na likifanyika hili hakuna mtihani mgumu. Nilipofanya mimi mtihani tulikuwa 42 darasa letu na 14 tukapata divisheni wani katika shule ya serikali......leo naona aibu sana na haya matokeo!
 
Afadhali hata ya kibwebwe mkuu je na wale wanaolazwa nje kishirikina? au kufanyiwa vitu vibaya?walimu wanashida sana hasa huko vijijini
 
Kata rufaa
mzizi wa fitina dawa yake ipo,.....kata rufaa ili uoneshwe mitihani ilivyosahihishwa
 
Hivi anasahihisha ndalichako ?
Au jopo la walimu wa somo husika?
Mjuao nijulisheni
 
hivi tulitegemea matokeo gani?kama waliofeli darasa la saba wakapelekwa secondary si ndo hao hao tena wamefeli leo form four?na kusema ukweli pia pass mark ya kuingia form five ikishushwa kwa hawa form four wa this year basi matokeo ya form six 2015 yatakua dizasta.
 



ndugu yangu sikubaliani na wewe. mwalimu anapotunga mtihani shuleni, lazima ajiulize kuwa syllabus imefundishwa hadi wapi. akitunga mtihani wa muhula wa kwanza, itakua ajabu akiweka topics ambazo hajazifundisha. zinafaa kufundishwa
muhula wa pili. huo ndiyo upimaji (evaluation)

ile formula ya kcaase kwa waliyo chukua ualimu wanaelewa umuhimu wake. kugawa maswali kwa 25. 50 na 25% kama nilivyo andika awali ni muhimu sana. kwa mwalimu bora, akipelekwa senegal kutunga mitihani, hawezi kukurupuka kutunga kabla ya kuzingatia vipengele vingi. baadhi yake ni kuuliza kama hapajatokea mafuriko au vita au janga lolote lililofanya syllabus zisifundishwe kwa ukamilifu, maabara zipo mashuleni, ufaulu wa mwaka uliopita ulikuwaje, nk......

ufaulu mzuri ni ule ambao umekaa kama bakuli lilofunikwa. pande za pembeni ziko chini na upande wa katikati uko juu. namaanisha kuwa wanaofaulu kwa division 1 wachache, wanaopata div 11 na 111 wengi, na wale wa iv na 0 wachache. mwaka huu wa iv na 0 ndiyo wengi! hii ni hatari. sababu zitafutwe naamini ni nyingi lakini lazima waliyotunga nao wana swali la kujibu. dkt. ngalichako ajiuzulu
 
Inabidi kuanza kufundisha watoto ili kuelewa (kufanya education user friendly).., zama za kukesha na kunywa kahawa huku umeloweka miguu kwenye ndoo na kukariri nadhani imepitwa na wakati.., vijana siku hizi wanataka vitu laini laini na vinavyovutia.., (tuwafanye watoto wapende kusoma sio kulazimika kusoma)
 

Eti wana wa Tanzania hawakufaulu kwa kiwango kinachotakiwa! zaidi ya asilimia 60 wamepata sufuri kwa maana ya alama zilizowekwa ktk kila swali, kwa maana nyingine walizopata hazikutosha! lakini wamepata ila awamo ndani ya mshindi wa 1 - 4 (madaraja).
Ebu tujiulize, ni mitihani gani wanapewa wana wa Tanzania? Hii mitihani inausiana vipi na changamoto tulizonazo kwa sasa; kiuchumi, Kisiasa, kiimani, na kijamii kwa ujulma? Inamaana hao 60% hawafai, hawanamaarifa yoyote?

Je, ili sio tatizo la mfumo wa elimu yetu?!
Je, waliofaulu ni kweli wamepata ujuzi wa kutatua changamoto zilizopo au wamepata alama nyingi ktk kila swali?
Je, mfumo wa maswali ya kuchagua tunautamzamaje, hauna uhusiano na matokeo haya?
Je, ambao hawakufaulu mwaka 2011 wako wapi, na wa mwa 2012 wanaelekea wapi, na wa 2013.....????
Kama chakula kimepikwa lakini hakikuiva inavyotakiwa, kinafaa kutumika? Je, nani alaumiwe: Kuni/mkaa/gasi, maji, chungu/sufuria, jiko, MPISHI, au mazingira/system inayotawala kanuni za upishi?
 
acha siasa kwenye kutafuta majibu ya majanga kama haya. huku jamvini tunaangalia uzito wa hoja na si jina au umaarufu wa mtoa hoja. sasa yakubidi kuwa makini katika uwasilishaji na tathmini ya hoja zako ewe mtoa mada
 
Pasco UCHOCHEZI JAMII (Public Incitement) una sura nyingi sana.........ikiwemo hii
Tangu lini mtu kusema ukweli ukawa uchochezi? Hakuna sehemu yoyote duniani wanaweza kukubali matokeo ya aina hii zaidi ya Tanzania. Kuna haja ya kuisuka upya wizara ya elimu kama siyo serikali nzima.
 
mzee kajipange urud kivingine, hoja yako imekosa mashiko watu wote wamekukataa, kiukwel umekuja na hoja nyong"onyevu, yaani elim imekua na matabaka yote hayo unamlaum ndalichako
 
mkuu hakuna udanganyifu katika mitihani hii ,jiulize kwanini wengine wamefaulu??? Kuna shule ya serikali ya kata mtaani kwangu na imefaulisha na hamna walimu jiulize?juhudi binafsi zinahitajika as a student.


Ufaulu wenyewe siyo huo tulioutegemea, nimejaribu kufuatilia shule nyingi sikuona point 7 au 8. Hata watoto waliofaulu bado wengi wao hawaamini kilichotokea. Ukitaka kuelewa vizur zitafute shule zilizoingia top ten mwaka huu halafu angalia na top ten ya mwaka jana ndo ulinganishe matokeo ya mwaka huu na ya mwaka jana. Sitetei wabovu ila kitenndo cha point 7 & 8 kutokuonekana kinanipa wasi wasi.
 
Mkuu Pasco nadhani hapa umeenda pembeni ya mstari, sidhani kama NECTA walifanya hicho ulichoandika, na unavyosema hivyo ni unawakosea hao unaodhani ni wajinga mpaka NECTA wawe na uhakika kuwa kwa mtihani huu wakina fulani watashinda na kina fulani watashindwa.
 

minadhani tuandamane atoke kawambwa au mnasemaje mazee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…