Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karibu mjumbe ila mwambie tumechoka kunywa maji ya visima tulitaka walau fedha za mfuko wa jimbo zingetumika kusambaza maji katika maeneo yenye shida kubwa ya maji hasa buzirayombo.
Thubutu!Kura zote kwa Bi. Husna Saidi jembe kutoka CHADEMA
Siku zote kila mtu hutafuta ambacho hana.ila naweza kusema watanzania hawariziki,,imagine mwananchi wa chato nae analalamika hawajafanyiwa maendeleo jimboni kwao,,,,
kila zama na vipaumbele vyake.SHIDA ZA WANACHATO AMESHINDWA KUZITATUA JOHN MAGUFULI ZAIDI YA MIAKA15 MNAMLAUMU KALEMANI KWA MIAKA5????? Chagueni upinzani tu Ccm haijawahi kua na wema miaka 59+ ya uhuru
Anatetea ugali wake mkuuLugola Ametufanyia Kitendo Kibaya Sana
Kumwita Mheshimiwa Hilo Jina Haa 😀😁😂😅😄😄
Siyo Sawa
Ameleta fisi 30 kutoka serengeti,uwanja wa ndege za kimataifa bado ataleta mlima kilimanjaro huko mda si mrefuKwako mbunge wangu Mh Medard Matogoro Kalemani na waziri kamili wizara ya nishati, kwa niaba ya wanachato wapenda CCM tunakuomba tu upumzike siasa na uwaachie wengine watakao weza kuleta maendeleo chanya jimboni kwetu.
Kwa muda wa miaka yako mitano kama mbunge wa jimbo letu pendwa naomba nikiri wazi hujafanya lolote wewe kama mbunge.
Shida za wanachato bado ni nyingi sana licha ya kwamba zinaweza kupatiwa ufumbuzi ndani ya muda mfupi tu.
Tukiacha miradi yenye ufadhili wa serikali kuu moja kwa moja kama vile ujenzi/uboreshaji wa hospitali ya wilaya pamoja na vituo na zahanati mbali mbali, uboreshaji wa shule, ujenzi wa chuo cha VETA na usambazi wa umeme vijijini wacha tuongeze na shule ya Nyabilezi inayojengwa kwa ufadhili wa Yoweli Museveni unaweza kutuambia wewe kama mbunge ni kipi hasa umefanya?
Sehemu nyingi za jimbo lako bado kuna shida kubwa sana ya maji ukianzia maeneo ya Buseresere, Bwanga, Njoo mpaka Mkungo na buzirayombo, Nyamirembe, Kibehe mpaka Muganza hadi Bwongera huku kote upatikanaji wa maji safi na salama bado ni shida kubwa sana licha ya kwamba tupo kando kando ya ziwa victoria linalohudumia mikoa ya shinyanga na Tabora.
Tuachane na suala la ajira maana hili ni janga la kitaifa na kwa nchi yoyote inayopitia kipindi cha mpito ili kuyafikia maendeleo ni lazima tu kundi fulani liumie ili badae wengi waje wafurahie ila sasa ni aibu sana kwa kushindwa ata kuweka barabara za mitaa jimboni kwako yaani pako zig zag tu. Hapa sisemie Chato mjini nazungumzia kata zote zilizo nje ya mji wa Chato.
Bado huduma ni mbovu sana katika hospitali yetu ya wilaya kwani watoa huduma hawako na spidi kubwa yaani unaweza wahi mapema asubuhi ila ukaondoka jioni saa kumi na moja bila kupata majibu ya vipimo ulivyopima.
wacha tu niishie hapa kwa leo ila ni mengi sana bado hujayafanya.
TUPISHE TU MHESHIMIWA.
Mwambieni alietumia mabilioni kujenga uwanja wa ndege na kuleta fisi 30Karibu mjumbe ila mwambie tumechoka kunywa maji ya visima tulitaka walau fedha za mfuko wa jimbo zingetumika kusambaza maji katika maeneo yenye shida kubwa ya maji hasa buzirayombo.
mkuu unaota ama?? fedha za mfuko wa jimbo Mil 40-60 uatasambaza maji gani?Karibu mjumbe ila mwambie tumechoka kunywa maji ya visima tulitaka walau fedha za mfuko wa jimbo zingetumika kusambaza maji katika maeneo yenye shida kubwa ya maji hasa buzirayombo.
WAPUMBAVU TUU KAMA WATAMLAUMH KALEMANI WA MIAKA MITANO NA KUACHA KUMLAUMU MAGUFULI ALIYEWAONGOZA ZAIDI YA MIAKA10haya maajabu ya dunia sasa chato katika wamu hii mkilia kule kantalamba si watabubujika machozi ya damu.
Wewe umeshawahi kumiliki kibanda hata cha Room 1?je matumizi ya manunuzi ya umeme unayajua?kila mteja anayenunua umeme anakatwa asilimia ambazo zinaenda kuingia kwenye umeme wa Rea,umeme wote unaouona WANANCHI ndiyo wamewasambazia wanyonge wa vijijini, Serikali haijatoa hata Senti, na Rea haijaanzia awamu ya tano.WanaChato nyamazeni huyo Kalemani kaitumikia TZ yote kwa ujumla, kasambaza umeme vijijini na sasa upo 80% Nchi nzima
Kama hamumtaki tuleteeni huku kwetu tu,lipie Fomu ya Ubunge
Jafo kalipiwa na Wamaasai kwa kufunguliwa Dispensary na kafika Kisarawe kakuta kalipiwa tena.
Mwacheni Kalemani arudi kwenye Nishati amalizie kusambaza umeme wake, Bei ya umeme imeshuka, kadhibiti wale wahujumu mitambo waliokuwa wakijizimia hovyo pale Ubungo
Kasimamia Stigler Godge hebu mpeni Ubunge
Kama waliomba maji wakapelekewa uwanja wa ndege.ila naweza kusema watanzania hawariziki,,imagine mwananchi wa chato nae analalamika hawajafanyiwa maendeleo jimboni kwao,,,,
2015 Kalemani mwenyewe aliponea chupu chupu.Jimbo la Chato huwa mbunge huwa achaguliwi kwa njia ya kidemokrasia kupitia kura halali za wananchi, bali mbunge anasimikwa kupitia sarakasi nyingi za kimazingaombwe.