Valuhwanoswela
JF-Expert Member
- Jun 27, 2019
- 1,229
- 1,125
Kwako mbunge wangu Mh Medard Matogoro Kalemani na waziri kamili wizara ya nishati, kwa niaba ya wanachato wapenda CCM tunakuomba tu upumzike siasa na uwaachie wengine watakao weza kuleta maendeleo chanya jimboni kwetu. Kwa muda wa miaka yako mitano kama mbunge wa jimbo letu pendwa naomba nikiri wazi hujafanya lolote wewe kama mbunge. Shida za wanachato bado ni nyingi sana licha ya kwamba zinaweza kupatiwa ufumbuzi ndani ya muda mfupi tu. Tukiacha miradi yenye ufadhili wa serikali kuu moja kwa moja kama vile ujenzi/uboreshaji wa hospitali ya wilaya pamoja na vituo na zahanati mbali mbali, uboreshaji wa shule, ujenzi wa chuo cha VETA na usambazi wa umeme vijijini wacha tuongeze na shule ya Nyabilezi inayojengwa kwa ufadhili wa Yoweli Museveni unaweza kutuambia wewe kama mbunge ni kipi hasa umefanya? Sehemu nyingi za jimbo lako bado kuna shida kubwa sana ya maji ukianzia maeneo ya Buseresere, Bwanga, Njoo mpaka Mkungo na buzirayombo, Nyamirembe, Kibehe mpaka Muganza hadi Bwongera huku kote upatikanaji wa maji safi na salama bado ni shida kubwa sana licha ya kwamba tupo kando kando ya ziwa victoria linalohudumia mikoa ya shinyanga na Tabora. Tuachane na suala la ajira maana hili ni janga la kitaifa na kwa nchi yoyote inayopitia kipindi cha mpito ili kuyafikia maendeleo ni lazima tu kundi fulani liumie ili badae wengi waje wafurahie ila sasa ni aibu sana kwa kushindwa ata kuweka barabara za mitaa jimboni kwako yaani pako zig zag tu. Hapa sisemie Chato mjini nazungumzia kata zote zilizo nje ya mji wa Chato. Bado huduma ni mbovu sana katika hospitali yetu ya wilaya kwani watoa huduma hawako na spidi kubwa yaani unaweza wahi mapema asubuhi ila ukaondoka jioni saa kumi na moja bila kupata majibu ya vipimo ulivyopima. wacha tu niishie hapa kwa leo ila ni mengi sana bado hujayafanya. TUPISHE TU MHESHIMIWA.
Ungeeleweka kama ungemtaka mtangulizi wake awapishe kwa kutofanya lolote miaka 20 akiwa Mbunge na Waziri na miaka 5 akiwa Rais akizunguka na mabulungutu ya fedha akigawa kama njugu kwa watu wasio wa nyumbani. Mpeni huyo miaka mingine 5 atawafanyia maajabu ikiwa ni pamoja na flyover kama Ulaya mkimtupilia mbali mtangulizi wake aliyeahidi kuwatua ndoo ya maji wanawake kumbe ana maana ndoo tupu.Kwako mbunge wangu Mh Medard Matogoro Kalemani na waziri kamili wizara ya nishati, kwa niaba ya wanachato wapenda CCM tunakuomba tu upumzike siasa na uwaachie wengine watakao weza kuleta maendeleo chanya jimboni kwetu.
Kwa muda wa miaka yako mitano kama mbunge wa jimbo letu pendwa naomba nikiri wazi hujafanya lolote wewe kama mbunge.
Shida za wanachato bado ni nyingi sana licha ya kwamba zinaweza kupatiwa ufumbuzi ndani ya muda mfupi tu.
Tukiacha miradi yenye ufadhili wa serikali kuu moja kwa moja kama vile ujenzi/uboreshaji wa hospitali ya wilaya pamoja na vituo na zahanati mbali mbali, uboreshaji wa shule, ujenzi wa chuo cha VETA na usambazi wa umeme vijijini wacha tuongeze na shule ya Nyabilezi inayojengwa kwa ufadhili wa Yoweli Museveni unaweza kutuambia wewe kama mbunge ni kipi hasa umefanya?
Sehemu nyingi za jimbo lako bado kuna shida kubwa sana ya maji ukianzia maeneo ya Buseresere, Bwanga, Njoo mpaka Mkungo na buzirayombo, Nyamirembe, Kibehe mpaka Muganza hadi Bwongera huku kote upatikanaji wa maji safi na salama bado ni shida kubwa sana licha ya kwamba tupo kando kando ya ziwa victoria linalohudumia mikoa ya shinyanga na Tabora.
Tuachane na suala la ajira maana hili ni janga la kitaifa na kwa nchi yoyote inayopitia kipindi cha mpito ili kuyafikia maendeleo ni lazima tu kundi fulani liumie ili badae wengi waje wafurahie ila sasa ni aibu sana kwa kushindwa ata kuweka barabara za mitaa jimboni kwako yaani pako zig zag tu. Hapa sisemie Chato mjini nazungumzia kata zote zilizo nje ya mji wa Chato.
Bado huduma ni mbovu sana katika hospitali yetu ya wilaya kwani watoa huduma hawako na spidi kubwa yaani unaweza wahi mapema asubuhi ila ukaondoka jioni saa kumi na moja bila kupata majibu ya vipimo ulivyopima.
wacha tu niishie hapa kwa leo ila ni mengi sana bado hujayafanya.
TUPISHE TU MHESHIMIWA.