Uchaguzi 2020 Dr. Kalemani pumzika tu, Ukweli Jimbo la Chato hujafanya chochote

Ungeeleweka kama ungemtaka mtangulizi wake awapishe kwa kutofanya lolote miaka 20 akiwa Mbunge na Waziri na miaka 5 akiwa Rais akizunguka na mabulungutu ya fedha akigawa kama njugu kwa watu wasio wa nyumbani. Mpeni huyo miaka mingine 5 atawafanyia maajabu ikiwa ni pamoja na flyover kama Ulaya mkimtupilia mbali mtangulizi wake aliyeahidi kuwatua ndoo ya maji wanawake kumbe ana maana ndoo tupu.
 
ila naweza kusema watanzania hawariziki,,imagine mwananchi wa chato nae analalamika hawajafanyiwa maendeleo jimboni kwao,,,,
Aisee na mimi nimestuka sana, hawa watu wa chato ndo watu wamepata neema kuliko majimbo yoote hapa Tanzania kwa hawamu hii, suala la umeme wamesambaziwa hadi kwenye vibanda vya nguruwe, mbuzi, ng'ombe na kuku huku majimbo mengine tukiendelea kusalia kwenye giza, sasa huyu naona anakufuru maana kumbe wamejengewa na hospital, Veta nk
 
ACHA ujinga mdudu wewe, umeme hauvuki 10,000. kwa mita moja kwa mwezi iwe Mjini au vijijini
unakumbuka majenereta yalivyounguruma mijini? je yale yaliyokamatwa na JPM
ulichangia nini Tanesco au maisha yako yote wakati Herbiner Sigh na Ruge waliimaliza Tanesco?
wako waliochota mabilioni Benki ya Standard kwa canter kw nini hayakujenga kwenu hiyo REA hizo awamu nyingine
Tunazungumzia Dr Kalemani, anaitumikia Tanzania sio Chato, kamuulize Prof Muhongo na wenzake km waliiweza Wizara hiyo
 
yaani kuna mijitu mijinga sana YANAPINGA KILA KITU mpaka wanataka kuondoa neema Jimboni kwao
wamepewa mpaka Traffic Light, magari hakuna wamepewa Mabenki hawaweki pesa humo, barabara za taa, uwanja wa ndege, Kiwanja cha mpira kikubwa kuliko vyote.
Eti Mbunge Dr Kalimani hafanyi kazi hatuna maji, aache kuzunguka Tanzania
Wakaangalie Majimbo km Hai, Vunjo, Rombo hata taa za barabarani hawana, traffic light hakuna vichochoro vya lami, kiwanja tu cha mpira wanatumia cha Chuo cha Ushirika Mkoa hauna
Leo mnamsumbua Dr Kalemani
 
Na hatorudi hapo chato jinga Sana kashindwa kumtumia Magufuli kuleta maendeleo jimboni kwake,, naona watu wanaing'ong'a chato na wakazi wake Ni wivu tu endeleeni kuumia na kupata vidonda vya tumbo
 
Hongera Dr Kalemani kwa ushindi wa kura za maoni ulioupata.
To be honest, binafsi sikupendi kabisa ila tu nakuunga mkono kwa maslahi ya Chama, Chama kwanza mtu badae.

Ushauri wangu hakikisha unatatua changamoto za jimbo letu hasa hasa suala la maji japo kuna watu wanasema eti Chato tuna maji ila ukweli tunaujua sisi wana Chato hasa tulio pembezoni mwa you wilaya yetu. Shida ya maji ni kubwa sana hakikisha unaitatua.

TUPO PAMOJA KWA MASLAHI YA CHAMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…