Dr. Leakey Abdallah yupo TV 1

Dr. Leakey Abdallah yupo TV 1

Wengine hawakuwa na luninga enzi hizo mkuu,wengi wameanza kumiliki luninga na visimbusi dtv ishapotea.walokuwa na tv miaka ya 90 mpaka early 2000 walikuwa wakuhesabika mtaani,hasa huku uswahilini

Mkuu utakuwa unazikumbuka zike show za "Football made in Germany"
Football made in Italy
 
Liki Abdallah yupo vizuri kihistoria ila kwa upande wangu kwa kizazi chetu cha sasa EDO Kumwembe na Jef Leah wapo vizuri
Toa Huyo Jeff..hana uwezo wa kuchambua mechi zaidi ya kuzungumzia Man u..na kupenda kuongea Yy tu wakati unakuta wanaochambua mechi hiyo wapo wengi.
 
Kashasha mzee wa acceleration,ball control,accuracy
 
Mkuu utakuwa unazikumbuka zike show za "Football made in Germany"
Football made in Italy

Kipindi hicho tunamuangalia okocha akicheza ujerumani abeid pele akikipiga Torino ya Italy na captain Dunga akicheza Stuttgart ya ujerumani..yaani ilikua kama tunacheki gem live kumbe recorded 3 month's back..kweli tumetoka mbali
 
Binafsi Tanzania hakuna mchambuzi bora kama Mwalimu Kashasha (RIP) na Dr. Leaky wengine wote ni wachambuzi wa janjajanja.
Itakuwa Dr. umeanza kumsikia juzi juzi tu, ungefstilia euro96 na WC98 ungemjua huyu bwana vizuri, alikuwa anakwambia kipindi cha pili inabidi aingie fulani ndio atabadili tokeo na kweli inakuwa hivyo, Abdallah ana uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo
 
Dr Liki ni habari nyingine. Peleka mbali huo upuuzi wa kina Edo
Dr ana style yake unajuwa ni kama umekaa na babu halafu anakupa story una enjoy kusikiliza anajuwa mambo ya soka japo sio kwamba lazima anajuwa kuchambua mechi inayochezwa ila anajuwa anaongea nini ni style yake iko tofauti anapenda kuongelea mambo ya nyuma na kuna watu wanapenda. Sasa hawa wachambuzi waleo wanapenda ku copy yaliyoko kwenye mitandao halafu wana report tu inachukiza mpaka misemo ya kizungu utasikia press ya juu na maneno mengi ya kizungu ili kuonesha wanajuwa lakini wewe unaongea na watu tofauti sasa kuna shida gani ukaongea kiswahili ukaeleweka. Usiongelee jambo hata mimi mtazamaji nikiangalia game najuwa mapungufu yako wapi na nadhani naelewa maana nimejitest team yangu ya liver wakicheza kuna wakati nasema hapa fulani atoke aingie fulani na kweli kocha anafanya kama mawazo yangu, kwa hawa wachambuzi ili uitwe mchambuzi kuna wakati unatakiwa kuliona jambo labda sio kila mtu ana upeo wa kuliona ukaliongelea sio umekazania tu pale hakuna press pale Highline defence halafu usiongelee una maanisha nini lakini lengo lako wasikuelewe ili wakuone uko smart.
 
Mchambuzi mkongwe wa mpira.Kwa sasa yupo TV1.

Mzee anajua sana historia na matukio makubwa kwenye ulimwengu wa mpira.

Mtaani kuna tetesi kuwa yeye ni mmoja wa waanzilishi wa betting.he kuna ukweli?

Tujuzane Historia,kama aliwahi kucheza soka tujuzane tafadhali.

Huyu ni hazina kwa taifa.Tusisubiri mpaka aage dunia ndo tupate kumfahamu.
TV1 inapatikana wapi?
 
Back
Top Bottom