Dr. Leaky Abdallah, Shafih Dauda, Edo kumwembe na Geofrey Leah nani mchambuzi bora wa soka?

Dr. Leaky Abdallah, Shafih Dauda, Edo kumwembe na Geofrey Leah nani mchambuzi bora wa soka?

Edo anaungansha story ya man u anaipeleka kwao tunduru,anaongezea na nondo alizosoma kwenye riwaya za mtobwa anatia chumvi na maneno ya mtaani! Unapata kitu kmetulia unarudia kusoma tena na tena. Wapi mwanaspoti ya leo! Edo ni nyoko eti!

Huo ni ubunifu,na ndio kitu kinachotakiwa katika kazi yoyote ile!
 
Edo ndio kila kitu kaka, shafih ana mambo mengi sometimes anasahau kutaja hadi muda wa mechi

At least Edo anajitahidi kuchambua hasa technical analysis wengine wote kina leaky sijui shafii hamna kitu wenyewe wamekariri historia na matukio ya wachezaji na mechi ndo maana ukiwasikiliza wanapoulizwa kwa mfano jinsi goli lilivyopatikana hawawezi kusema kitu zaidi ya kusema hili goli linanikumbusha mwaka 1974 flani alifunga hivihivi lakini Edo anaweza kuelezea mazingira na namna goli lilivyofungwa kiutalam
 
Wote makanjanja tu!

Wivu wa KIKE huo. Mwenzako akikuzidi mpe sifa zake.

Kwangu mimi Leaky Abdalah hafananishwi na wote hao. Kwanza ni mkongwe ametoka mbali. Pili hahitaji kujiandaa maana hapo kwa hapo anakushia nondo kali sana. Wote hawa wameiga kuyoka kwake.
 
Dr.Leack ndio Mwalimu wao.....ila Eddo ndio wa kuvaa viatu vyake....

....hawa wengine huwa sijisumbui hata kusoma makala au kusikiliza uchambuzi wao naona ni wapiga soga tu.!!
 
wote hawajui kuchambua mpira na kuelza kwa nini hiki au kile kimetokea katika dakika tisini. kuna msemo wa kiingereza " blessed is he who understands the causes of things" sasa tatizo lao wao hawaelezi nii haswa kinatokea katika zile dakika 90 na KWA NINI...yule ambaye anaweza kueleza kwa nini ndio mchambuzi lakini sijaona lolote.
 
Leaky Abdalah yupo mbali sana hupaswi kumuweka katika kundi lao hao jamaa.
Ukiwachukua hao watatu waliobaki Edo, Shaffih na Leah ukweli una baki kuwa Edo Kumwembe yupo juu yao halaf hao wengine wawili wapambanishe mwenyewe muanzisha Uzi.
 
Eddo kiasi. wengine wamekalia kutaja takwimu tu as if wao ni aechives au maktaba. COPY & PASTE
 
dr leakey ni mzuri kwa historia ya michezo lakini kwa technical issues za uwanjani sio mzuri sana labda edo ndo anaziweza na jeff.dr leakey sio kihivyo kawaida
 
Kwa jina anaitwa dkt lick abdalah kama sijakosea jina lake,naomba kujuzwa zaidi kuhusu huyu jamaa ambaye ni mchambuzi mzuri wa soka hapa kwetu tanzania.nawasilisha wakuu
 
Mimi najua kwamba Dk. Licky Abdallah anamiliki kampuni ya uwindaji wa wanyama pori
 
Kama kumbu kumbu zangu ni sahihi huyu jamaa jamaa sio Dr wa phd wala medicine..

Ni wenyeji Wa Kakonko Kigoma. Kuna kipindi alikuwa anafanya biashara ya watalii.

Hana taaluma ya soccer ila anatumia utundu binafsi
 
Back
Top Bottom