Mkuu, Dr. Liki(Abdulmalik Abdallah) anajua sana mambo ya soka nadhani kuliko wachambuzi wote sio tu wa Tz mpaka wale waliopo katika mashirika makubwa ya habari ya nje kama supersport, skysport, bbc, espn n.k. Nakumbuka miaka ya 1990's mwishoni kuelekea 2000 dtv/itv walikuwa wanaonesha mipira ya nje kama epl, euro, world cup na afcon(kabla ya zuio la supersports), Dr. Liki alikuwa na Michuzi pamoja na Poki Fereji, alikuwa anaelezea vitu vingi sana vya mpira kama vile; historia ya mpira, kwanini england hawapendi penalty shootout, panenka chip, eusebio, historia ya santiago bernabeu (inaonekana alifika kwenye huo uwanja pia), kwanini Afrika ilipewa nafasi tano World cup, kwanini roger milla alirudi uwanjani. Mpaka sasa bado anaelezea vitu kuhusiana na mpira wa nje ambavyo si rahisi kuvipata kwenye mtandao. Vile vile sio rahisi kujua anashabikia timu gani tofauti na kina dauda na kumwembe. Mara nyingi haoneshi ushabiki kabisa, wale mabwege wa supersport wengi wao wanashindwa kuficha ushabiki wao kwa timu wazipendazo. Kama yule black mdogomdogo(nadhani anaitwa Thomas Mlambo) muda wa 2010 wc alikuwa anaonesha ushabiki usio wa lazima kwa timu ya SA ambayo ilikuwa mbovu kabisa, kama mtakumbuka akiizungumzia mechi ya pili ya group stage kati ya SA na Uruguay(gk ya SA Khune alipewa red card na uruguay walipata penalty SA walifungwa 3-0). Vilevile watangazaji wao kwenye UCL wanaonesha ushabiki mkubwa kwa sevenlona.