Dr. Leaky Abdallah, Shafih Dauda, Edo kumwembe na Geofrey Leah nani mchambuzi bora wa soka?

Dr. Leaky Abdallah, Shafih Dauda, Edo kumwembe na Geofrey Leah nani mchambuzi bora wa soka?

Mkuu soka n utundu! Dk licky anaijua
Soka,acha utan may b kama umezaliwa
Nw dayz bt kwa cc watu wa zaman
Kipindi cha itv inaanza weee hakuna
Kama lick, hawa wengine ukiwauliza
Wamejifunza kwake.
 
Nilishawai msikia shaffi dauda akisema dk lick ndiye aliye mshawishi na kitamani kuwa kama yeye kwenye masuala ya soka
 
Kwa jina anaitwa dkt lick abdalah kama sijakosea jina lake,naomba kujuzwa zaidi kuhusu huyu jamaa ambaye ni mchambuzi mzuri wa soka hapa kwetu tanzania.nawasilisha wakuu

Jina halisi la Dr lick ni abdulmarick abdallah,ni mzaliwa wa kigoma na ni mtanzania pure kwa zaidi ya 100% pia kazaliwa ktk family ambayo tabu na shida mzee wao alikuwa na uwezo wa kuzitatua.moja ya biashara zake baba'ke Dr lick ni umiliki wa petrol station, jina la Dr lick alipewa na wanafunzi wenzake wakimfananisha na yule archaeologist Dr Louis Leakey aliegundua fuvu la mtu wa kale kule Olduvai gorge mwaka 1959.kuhusu soka huyu mpira upo damuni yaani anakula soka,anaongea soka yaani kila kitu ni soka hii ni kwa sbb mzee wao alifunga dish antenna kitambo sana kwahiyo ameanza kufatilia mpira tofauti na wengi wetu ambao tumeanza kufatilia mpira sanasana kuanzia labda 1998. Lastly jamaa ni bonge la match analyst,binafsi namkubali sana. Wadau mpoo...??
 
Dah kapotea huyu..enzi mechi za UEFA mtaalamu huyu alikuwa balaah!kuna fainali ya Real vs Leverkusen aliwah hudhuria na kuchek k2 live from scotland!!dah kitambo sana,
 
Jamaa anajua historia ya mpira si mpira wenyewe, anabaki kuwajua wachezaji kwa majina yao lakini si fomeshen ya mpira wenyewe
 
Jangili mwenye kibali

Jaribu kuwa na heshima wewe pimbi, Rick anamiliki kampuni ya professional hunting na analipa kodi zote za serikali na ameajili watu wanakula na kujamba kutoka kwenye kampuni. Jifunze heshima zuzu wewe.
 
Jina halisi la Dr
lick ni abdulmarick abdallah,ni mzaliwa wa kigoma na ni mtanzania pure
kwa zaidi ya 100% pia kazaliwa ktk family ambayo tabu na shida mzee wao
alikuwa na uwezo wa kuzitatua.moja ya biashara zake baba'ke Dr lick ni
umiliki wa petrol station, jina la Dr lick alipewa na wanafunzi wenzake
wakimfananisha na yule archaeologist Dr Louis Leakey aliegundua fuvu la
mtu wa kale kule Olduvai gorge mwaka 1959.kuhusu soka huyu mpira upo
damuni yaani anakula soka,anaongea soka yaani kila kitu ni soka hii ni
kwa sbb mzee wao alifunga dish antenna kitambo sana kwahiyo ameanza
kufatilia mpira tofauti na wengi wetu ambao tumeanza kufatilia mpira
sanasana kuanzia labda 1998. Lastly jamaa ni bonge la match
analyst,binafsi namkubali sana. Wadau mpoo...??
Nimekuelewa mkuu nataman jamaa ningemuona tena kwenye world cup matches
 
Huyu mshkaji me mwenyewe namkubali kuna mwaka ilichezwa finali Kati ya Liverpool na ac Milan kipind cha kwanza Liverpool ulikua imeshaluwa 3 na akaelezea jinsi Benitez atakavofanya ili Mchozo kuubadilisha na ndo yaleyale yaliotokea cjui mnakumbuka Liverpool walivorudisha magoli matatu na kuchukua kombe kwa penalti



Kipindi Hiko nlikua naomba mpira apewe kaka ninavompenda
 
kuna uzi niliandika hivi
Mkuu, Dr. Liki(Abdulmalik Abdallah) anajua sana mambo ya soka nadhani kuliko wachambuzi wote sio tu wa Tz mpaka wale waliopo katika mashirika makubwa ya habari ya nje kama supersport, skysport, bbc, espn n.k. Nakumbuka miaka ya 1990's mwishoni kuelekea 2000 dtv/itv walikuwa wanaonesha mipira ya nje kama epl, euro, world cup na afcon(kabla ya zuio la supersports), Dr. Liki alikuwa na Michuzi pamoja na Poki Fereji, alikuwa anaelezea vitu vingi sana vya mpira kama vile; historia ya mpira, kwanini england hawapendi penalty shootout, panenka chip, eusebio, historia ya santiago bernabeu (inaonekana alifika kwenye huo uwanja pia), kwanini Afrika ilipewa nafasi tano World cup, kwanini roger milla alirudi uwanjani. Mpaka sasa bado anaelezea vitu kuhusiana na mpira wa nje ambavyo si rahisi kuvipata kwenye mtandao. Vile vile sio rahisi kujua anashabikia timu gani tofauti na kina dauda na kumwembe. Mara nyingi haoneshi ushabiki kabisa, wale mabwege wa supersport wengi wao wanashindwa kuficha ushabiki wao kwa timu wazipendazo. Kama yule black mdogomdogo(nadhani anaitwa Thomas Mlambo) muda wa 2010 wc alikuwa anaonesha ushabiki usio wa lazima kwa timu ya SA ambayo ilikuwa mbovu kabisa, kama mtakumbuka akiizungumzia mechi ya pili ya group stage kati ya SA na Uruguay(gk ya SA Khune alipewa red card na uruguay walipata penalty SA walifungwa 3-0). Vilevile watangazaji wao kwenye UCL wanaonesha ushabiki mkubwa kwa sevenlona.
https://www.jamiiforums.com/sports/449899-edo-kumwembe-vs-shaffi-dauda-3.html
 
jamani,kwa vile wataalamu wa ukweli na wachambuzi halisi hawapo kwenye media,wanabaki wababaishaji,sioni mchambuzi hapo......ni watoa maoni uhana analysis ya ukweli na hakuna figure,statistics na uchambuzi wa juu juu tuuuu mchambuzi ni MMOJA TU,KIJANA DENIS sasa yuko wizara ya maji.
 
Dr leakey anajua historia ya soka ila kwenye uchambuzi eddo yuko vzur zaid ya wote hao
 
Aisee sifuatilii sana mpira ila Dr Leaky nimemvulia kofia

Wooote hao ki ukweli Dr ni namba 1 maana yeye ndie wa kwanza hao wengine woote wame copy kwake kwa kuingia xana mitandaoni na kupata taarifa lakini wakati ule Dr alikuwa anapata taarifa kwa taabu
 
Dr leakey anajua historia ya soka ila kwenye uchambuzi eddo yuko vzur zaid ya wote hao


simba walicheza na yanga...
Na mpaka half time yanga walikuwa wanaongoza 3-0...
Je unajuwa eddo aliongea utumbo gani?
 
Kuna wachambuzi wa soka na wachambuzi wa matukio ya soka.Edo ni mchambuzi wa soka walobaki ni wachambuzi wa matukio ya soka na washereheshaji wa soka!.
 
Edo Kumwembe yuko juu hata makala zake ni za kiufundi, dr.Leakey ni mtoa historia tu ana bias na timu zake kama AC Milan au Germany, sio mchambuzi huru, shafii yaleyale anaongozwa na hisia zaidi.
 
Back
Top Bottom