Dr Levy: Ali Kiba ni dozi ya kutwa mara tatu

Kutoka kwa Dr levy amendika hiv

ALI KIBA NI DOZI YA KUTWA MARA TATU...
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Ukimfunika kukata mauno atakushinda kutunga. Ukimfunika umaarufu atakutesa kwa sauti. Ukimsumbua kuhonga media yeye atakuumiza kwa kutojisumbua na hizo media.
Ni kama kumpenda mwanamke ambaye hajui kama unampenda. Na mbaya zaidi hata hisia juu yako hana. Utaumia sana.
Ndo Kiba. Hata mashabiki wake wanampenda kuliko yeye anavyowapenda. Anachofanya ni kuwapa kile alichopewa na Mungu. Sauti. Watu wanadata naye.
Wakati watu wengi sana wakimsifia kwa sauti ambayo anayo yeye tu ktk dunia hii. Kuna kitu wanakisahau. Ana tofauti sana katika tungo zake. Sikiliza Mapenzi yana Run Dunia.
Anamuimbia mapenzi mwanaume mwenzake. Ngumu sana mwenye akili ya kisoda kuelewa ule wimbo.
Mchizi anamuimbia mchizi wake ngoma la mapenzi afu lina bamba mbaya. Hata R Kelly na wenzake akili hii waliikosa.
Dem kaenda kwa Kiba kumshitakia ujinga wa bwanaake. Of coz watoto wa kike wanapenda faraja. Kiba akampa faraja.
Mchizi kugundua kaamua kumtosa mtoto. Mtoto kaamua kutangulia mbele ya haki. Alimpenda mchizi wake ila Kiba alimpa faraja tu baada ya ushauri. Hata mimi ningemfariji kwa namna hiyo mtoto mzuri.
Kasikilize hilo ngoma ukiwa na akili timamu usichanganye na mawazo ya hali ya Wema Sepetu kwa sasa. Hutaelewa alichoandika Kiba.
Kiba siyo wa nchi hii. Kinachofanywa na computer yeye anakitoa kwenye koromeo lake.
Kuna sauti kutoka kooni kwake ni ya pekee kuliko upekee wenyewe. Hawezi kusema ila Diamond na wenzake hicho kitu kinawaumiza sana.
Kiba hajui kujitangaza. Ndo maana hata gari anayotumia haijulikani. Kiba hajui kiki. Ndo maana huwezi kumsikia akiongelea issue zake na madem zake. Hajui kujiongeza ndo maana husikii ana nyumba au shilingi ngapi kwenye account. Na ni ngumu kumkuta news room za udaku. Vyote hivyo hana lakini bado anawaumiza kichwa kundi kubwa la watu. Katikati ya magwiji wa hizi kazi. Fella, Tale na wenzao. Sallam muweke kando hajui fitna za game hili.
Pamoja na lundo la hao watu Kiba bado anasimama nao katika mstari mmoja. Ogopa sana. Heshimu. Hana anachowaweza zaidi ya lile koo lake na akili ya kuandika kinachotakiwa kuandikwa.
Hapa siyo suala la team flan. Ukweli uko wazi kuwa kuna upinzani wa wazi na wa siri kati ya Kiba peke yake na Diamond na watu wake. Huwezi kusikia management ya Kiba ikimuongelea Diamond. Ila ni rahisi zaidi kusikia management ya Diamond ikiongea jambo la Kiba. Ndo ukweli.
Watu wanaomzunguka Diamond huwezi kushindana nao hata kwa nusu saa. Game la muziki liko vyumbani mwao. Linawatii kuliko askari wa Dar mbele ya Makonda. Lakini Kiba kaendelea kuwepo kwenye kilele bila kutumia nguvu. Alichonacho Kiba kwenye koo angekuwa nacho Diamond dunia ingesimama. Ni kama Ronaldo angekuwa na kile alichonacho Messi katika miguu yake.
Mashabiki wanatumia nguvu nyingi sana kupambana na Diamond mitandaoni, wakati Kiba anawauliza wadogo zake vilipo viatu vyake vya michezo akacheze bondeni pale Jangwani. Diamond anajituma sana na muziki wake. Kiba anatufanya tuamini kuwa muziki ni burudani na ufanywe kiburudani.
Wakati soko la muziki likilazimishwa liwe na muziki unaochezeka. Kiba alikuja na ngoma kama Mac Muga ambao hauchezeki na siyo wa mapenzi. ukakamata vibaya sana. Kasikilize Karim. Utagundua kuwa Kiba ni zaidi ya biti na promo.
 
Haya bwana umesikika team Kiba ngoja na hizo team zingine ziingie.

Ila kwa vocal tu Kiba anayo ya asili hilo halina ubishi.
 
Dk. Levy pimbi tu. Nakumbuka kipindi cha uchaguzi akajifanya kumdis Maria Sesai kule Twitter. Ndio hapo nikaona umuhimu wa elimu maana dada alimmaliza kwa point bila jazba akabaki kujing'ata tu. Kwahiyo hizi ndio level zake kuandika ujinga.
 
Ngoja kukuche vizuri...
Andaa maji ya kutosha kuwafuta watu mapovu!!.
 
Yani hii makala fupi nimeisoma nikitabasamu mwanzo mwisho...naam huyo ndiye Ali Kiba,mfalme wa muziki wa kizazi kipya Tanzania
Najisikia fahari sana kuwa shabiki wake,na daima nitabaki shabiki wake namba moja.

Kuna mwenye tatizo huko?Asante Dr. Levy
Hahahah and I love it.
 
Mie huwa nasikiliza nyimbo hizi habari za timu ngoja niwachie mzaramo,nifah na hans mtanashati
Karibu kwenye timu ya muziki mzuri mkuu,sisi hatuna mbwembwe wala hatutumii nguvu nyingi sababu Kiba anaturahisishia kazi. [emoji4]

Unaanzaje kuumiza akili kumpamba mtu ambaye huitaji kuurudia mara mbili wimbo wake wowote ili uupende?
Ni Ali Kiba pekee nchi hii,hakuna mwingine tena kama yeye.
 
Ali hana tattoo,hasuki nywele wala havai vipini, wenye akili na wanaojielewa tu ndo humwelewa Ali
Jana nilikuwa sehemu fulani na marafiki zangu likaja hili suala ktk mada zetu.
Rafiki mmoja alisema kama ulivyosema wewe [emoji122] [emoji122] [emoji122]
Huyo ndiye Ali Kiba.
 
Yataandikwa mengi lakini hawezi kuitwa AFCON!...2017 ndio mwisho wa kiba kutumia nyota ya diamond
 
Ile ndio my best hit of all Ally's.
Mimi nilianza nae kwenye Cinderella,akaja kunibamba na Hadithi...kilichofuatia hadi leo na kesho ni historia.
Acha tu niendelee kuwa shabiki wa Ali Kiba,bila yeye siwezi kusikiliza nyimbo za wasanii wengine wa bongo hii.
 
Sasa akili hapo in ipi ukiwa na kipaji tumia kikulipe co unasema unakipaji uku unakufaa njaa shituka brother we umeanza mziki mikaa sits b4 yy lakn anakizid akili za kutafta pesaa da wabongo bhana nyie mjazen maneno ivo ivo lkn show za diamond mnaenda za kina hamuendi huo ndo ushabiki ufala shabiki unatakiwa kuwa assert not liability nyambafuuuuu
 
Kiba anaekwenda Dodoma na shabiby line,likaharibika,akalisubiri litengenezwe,kaingia dodoma saa 7 za usiku,kwenda kwenye shoo akataka kuuwawa na mashabiki wenye hasira au kiba yupo huyo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naam mkuu.

We umetuelewa vzuri kabisa...hiyo ndiyo tofauti ya Ali na Nasibu.

Ali haumizi kichwa kumpita Nasibu kibiashara maana kwenye akili yake Muziki ni burudani kama anavyocheza mpira kiburudani...
Asa kama anafanya mziki burudani mbona unamfananisha na anafanya mziki biashara au sizitaki mbivu izi......mnalilia adi tunzo..!!
Wanavodai anafanya mziki for fun so nashangaa Sijui kinawauma nn domo anapofanya music as business
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…