Elections 2015 Dr. Magufuli ndani ya Nachingwea,Mtama na Ruangwa - Oktoba 12, 2015

Elections 2015 Dr. Magufuli ndani ya Nachingwea,Mtama na Ruangwa - Oktoba 12, 2015

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Baada ya Mapumziko ya siku mbili, mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr. Magufuli ameanza rasmi ziara kwenye mkoa wa Lindi na asubuhi hii amefanya mkutano kwenye jimbo la Nachingwea.

Leo mchana mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi , Dr. Magufuli amefanya mikutano mikubwa miwili mpaka sasa baada ya ule wa asubuhi jimbo la Nachingwea.

Mikutano yote imekuwa na idadi ya nyomi ya kutosha hivyo ikawa rahisi kuinadi ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Kuondoa mtaala unaofanana nchi nzima. Mfano Kusini kuna gesi; mtaala VETA Kusini ukidhi utaalam wa gesi.

Mimi si fisadi, wala si tapeli, na Watanzania wote mnanifahamu. Ushindi wangu Oktoba 25 ni dhahiri. Wengine wanasindikiza.


Nachingwea
1.jpg2.jpg3.jpg4.jpg5.jpg

Ruangwa


Mtama

Hakuna namna nyingine naweza kusema kuhusu Nape na alichokifanya jana viwanja vya Sokoni huku akishirikiana na Dr. Tinga Tinga Rais wa awamu ya 5 anayesubiri kuapishwa.

Kwa uchache wetu watu wa Mtama na umati uliojitokeza Siku ya jana ni zaidi ya mara 3 ya mkutano wa Lowassa uliofaonyika wiki mbili zilizopita huku kukiwa na wanachama na wapenzi wa CHADEMA, CUF, NSSR na NLD.

Ndg Nape aliwachachafya kweli kweli wapinzani.

PIGO UKAWA
-Mratibu wa kampeni za jimboni mtama wa mgombea wa CHADEMA ndg Michael jana alirudisha kadi ya CHADEMA na kuingia CCM.

Alisema "kuna mambo ambayo sio mazuri yanayoendelea hivyo kuahid kuwaambia wananchi nini kimemkimbiza" ikumbukwe kuwa huyu ndg Michael kabla Selemani Methew hajahama CCM kuna baadhi ya wanakijiji walikuwa wakimlalamikia wapewe pesa zao alizochukua Selemani Methew kupitia vikundi vya wazee na akina mama.

-Pia dereva wa mgombea Ubunge jimbo la Mtama kupitia CHADEMA naye amerudisha kadi na kuacha kazi kwa kile kinachoitwa bosi wake ambaye ni mgombea kuna mambo anayafanya sio sahihi alisema "kuna siku mgombea Ubunge alitaka kujiteka mwenyewe ili aseme kuwa Nape ndio anataka kumteka na hilo tukio lilitokea wiki nne zilizopita.


 
Sawa kwa ajili hatutaki kumchelewesha lowassa ikulu
 
Back
Top Bottom