Tetesi: Dr. Meneja wa Makampuni: Tatizo la elimu ya Tanzania sio kukariri bali ni ugumu wa lugha inayotumika bila kuwekewa msingi mzuri katika lugha hiyo

Tetesi: Dr. Meneja wa Makampuni: Tatizo la elimu ya Tanzania sio kukariri bali ni ugumu wa lugha inayotumika bila kuwekewa msingi mzuri katika lugha hiyo

"Repetion is a mother of learning and a father action." Tuache vingizio, elimu ya nchi hii imevurugwa na mikono ya wanasiasa, ni siyo suala lugha. Mwafrika anao uwezo mkubwa sana wa kujifunza kwa lugha yoyote ile, bila tatizo. Elimu yetu ya GPA za hongo ndiyo kansa inayotutafuna taratibu.
 
"Tatizo sio madawati Kama wasemavyo wanasiasa, tatizo sio vitabu Kama wasevyo wa-Dodoma tatizo elimu mbovu kama mfumo wa TFF"Bonta maarifa
 
"Repetion is a mother of learning and a father action." Tuache vingizio, elimu ya nchi hii imevurugwa na mikono ya wanasiasa, ni siyo suala lugha. Mwafrika anao uwezo mkubwa sana wa kujifunza kwa lugha yoyote ile, bila tatizo. Elimu yetu ya GPA za hongo ndiyo kansa inayotutafuna taratibu.
Mkuu umeelezea vitu vidogo sana, umesahau kuwaelezea wale wenye uwezo lakini bado hawawezi kufanya vumbuzi wala tafiti zozote.
 
"Tatizo sio madawati Kama wasemavyo wanasiasa, tatizo sio vitabu Kama wasevyo wa-Dodoma tatizo elimu mbovu kama mfumo wa TFF"Bonta maarifa
😁😁😁😁😁😁🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌madawati sio tatizo mkuu, watu wazamani walisoma bila madawati.
 
Mkuu umeelezea vitu vidogo sana, umesahau kuwaelezea wale wenye uwezo lakini bado hawawezi kufanya vumbuzi wala tafiti zozote.
Wamefanya mengi ila mikono yao hao wanasiasa, imeyaweka kapuni hautokaa uyaone, Afrika ni zaidi ya uidhanivyo katika, ulingo wa kisiasa, katika siasa za kutembeza bakuli la kuomba misaada ugenini, wakati mali tunazo tumezikalia hapa nyumbani, tukilala wanachukua, wanawapelekea, asante kwa kupewa mikopo ya mashangingi yao ya kutembelea.
 
Hadi Sasa Kuna watu wanaamini kiingereza ndio huleta Maendeleo kazi ipo
 
naamini zaidi ya 70% ya watanzania waliosoma hawakuelewa walichosomea walipokuwa shuleni baadala yake wamekuja kuelewa wakiwa kazini....

Mfumo wa elimu kwa maana ya Lugha nakubaliana hapa ni TATIZO na tuna option mbili either kiswahili la kwanza mpaka chuo kikuu au kingereza lakwanza mpaka Chuo kikuu TUACHE JANJA JANJA....

Lingine la msingi, HII NCHI HAINA MFUMO WA MAISHA UNAOELEWEKA KWA WATU, WATU HAWAJUI UELEKEO NI WAPI NA KWA LENGO LIPI baadala yake kila mtu anaenda anakojua yeye matokeo yake ni shaghala baghala kila mahala....
 
Mkuu umeelezea vitu vidogo sana, umesahau kuwaelezea wale wenye uwezo lakini bado hawawezi kufanya vumbuzi wala tafiti zozote.
Vumbuzi na tafiti zinaenda sambamba na funding, serikali imetenga bajeti kiasi gani kwa ajili ya hawa wasomi wetu kufanya tafiti ? Ni kawaida sana kumkuta PhD holder kwenye field ya Telcom au Mechanical engineering etc. anakimbizana kwenye mabanda ya nguruwe ili apate additional income.

Kwa wenzetu unakuta maprofesa wana funding za kufa mtu na anauwezo wa kumchukua mwanafunzi yoyote afanye kazi chini yake ili wakamilishe tafiti...huku kwetu mwanafunzi wa PhD unakuta anahangaika na stipend ya 200,000 kwa mwezi bado ana watoto, mjomba, shangazi wanamtegemea unafikiri atafanya tafiti gani ya maana ?
 
ukiachana na lugha na mambo ya kukariri, vingi tuvisomavyo hasa kuanzia level ya tertiary kwenda juu, havisadifu kabisa makazini (field) huko

mathalan: uhandisi umeme, nimekomaa miaka minne na ujinga ujinga wa 'integrals na differentials' , nikija uku 'kazini' kila siku ni kujaza 'repoti buk' , na ujinga ujinga mwengine na kuondoka, mwisho wa mwezi napokea 'salary' ,

unajiuliza miaka yote minne huko chuoni ni utopolo tupu, kujaziana mavyeti tu kabatini
 
Tatizo la elimu ya Tanzania sio kukariri bali ni ugumu wa lugha inayotumika bila kuwekewa msingi mzuri katika lugha hiyo.

Kila kitu huja kwa kukariri lol. Bila kukariri huwezi kuelewa. Bila kukariri huwezi kujua kusoma na kuandika, bila kukariri huwezi kushika verbs, bila kukariri huwezi kuhesabu, bila kukariri huwezi kushika table ya kuzidisha. Bila kukariri huwezi kushika kanuni za kufanyia hesabu.
Hata calculator imekaririshwa kanuni.
Hata computer imekaririswa kanuni.
Hata roboti linakaririshwa kanuni.
Hata sofwares, programes zinazakaririshwa kanuni na definition.
Hata translator zanakaririshwa pia maana za maneno.
Ni hivyo tu. Tatizo la elimu yetu ni lugha tu.

Haya anazungumza Dr. Meneja wa makampuni.

Elimu ya Tanzania inajengwa kwa msingi wa lugha ya Kiswahili baadaye inachanganywa na lugha ya kiingereza.

Nirudie tena, elimu yetu inajengwa kwa msingi wa lugha ya Kiswahili baadaye inachanganywa na lugha ya kiingereza.

Wakuu naomba tusaidiane, hii sentensi inamaana gani? Yaani nikiwa naama kwamba wewe umeilewaje?

Kama tunapenda maendeleo ya kiuchumi kupitia elimu yetu tunapaswa kufanya jambo katika elimu yetu.

Pamekua na minong'ong'ono mingi kwamba elimu yetu ni ya vyeti tu ikiwa naama kwamba watu wanakariri tu na wala hawaelewi.

Maswali
Je, ni kwanini elimu yetu ni ya vyeti?
Je, ni kwanini wanafunzi hawaelewi?
Je, ni kwanini wanafunzi wanakariri?
Je, Wanakariri ili waweze kukuhifadhi kichwani walichofundishwa?
Je, Wanakariri ili waweze kuelezea wakipewa maswali kasababu tu hawawezi kuelezea kwa maneno yao wenyewe kwa kutumia lugha wanayotumia?
Je, ukiwambia waeleze kwa lugha ya kiswahili wataweza?
Tufanye nini katika elimu yetu, tutumie lugha ipi, tuanze kuitumia wapi ili kuweka msingi imara kwenye lugha ya kujifunzia.

Karibuni
Hivi wewe ni mwlimu wa kiswahili nini,usilazimisge wenzio wasiotaka upumbavu
 
Mada nzuri na mada hii inajadiliwa kila siku. Nilichogundua ni kwamba kuna pande mbili, moja inaafiki kuwa Kiingerea kiwe lugha ya kufundishia na upande wa pili wanakataa. Maoni yangu ni kuwapa wote. Tuwe na mifumo miwili ya elimu inayofanana kwa lugha mbili tofauti. Sasa hivi Kiingereza kinatumika kutoka sekondari mpaka Phd. Basi kuwe na mfumo mwingine wa Kiswahili hivyo hivyo. Kwa mfano mwanafunzi anachagua kutumia Kiswahili kuanzia sekondari, anafaulu anakwenda Chuo cha Kilimo Sokoine na anajifunza kwa Kiswahili na kwa bahati anaajiriwa na serikali kama Afisa Ugani kule Tunduru. Mchukue huyu aliyesoma kwa Kiingeza masomo hayo hayo kwa Kiingereza na huyu wa Kiswahili, ni yupi maelekezo yake yataeleweka kwa wakulima? Huyu nesi aliyejifunza kwa Kiswahili na huyu aliyejifunza kwa Kiingereza ni yupi atafanya kazi kwa ufanisi? Hawa hawa wape mitihani inayofanana kwa kila kitu kwa kutumia lugha aliyojifunzia nina uhakika hawa watakaojifunza kwa Kiswahili watafaulu zaidi. Na watakuwa wabunifu kazini.

Sasa hivi makampuni mengi ya madawa, pembejeo na bidhaa nyingine wajitahidi kutafsiri vipeperushi na maganda ya bidhaa zao kwa Kiswahili, wanajua wazi wateja wao ni Waswahili.

Chukulia hawa wanafunzi wakati wa masomo wanakwenda Field na kufanya research huku kwa wananchi, mambo yote wanayafanya kwa Kiswahili. Kwa mfano, Questionnaires wanaziandaa kwa Kiingereza lakini wakifika field wanawauliza au wanafafanua kwa Kiswahili huyu mhojiwaji akirudi chuoni anatakiwa kuandika taarifa yake kwa Kiingereza. Huyu mwanafunzi angepata nafasi ya kuandika taarifa yake kwa Kiswahili angeandika vizuri zaidi kwa Kiswahili kuliko kwa lugha ya Kiingereza.

Fursa tunazo, majirani zetu wameamua kuongeza juhudi kujifunza kiswahili na ni kwa sababu wameona ndio lugha itakayo waunganisha wote na kuondokana na ukabila. Ikumbukwe ukabila ndio unaowafanya watumie Kiingereza zaidi, watakapofaulu na kuamua Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia katika elimu ya juu, ndipo tutakaposhituka. Sisi tutaendelea kubaki oooh kiswahili chimbuko lake ni Tanzania, ooh ni Zanzibari na wakati huo ndio wao watakaokwenda kuwa walimu katika nchi nyingine kama ilivyo sasa.

Ziko tafsiri za vitabu mbali mbali zinazoweza kutumika katika mashule. Hii kazi ilishafanyika na iko kwenye mashelf. Muda wa mijadala kwa sasa umekwisha, tuanze kutekeleza kwa awamu. Maana yangu ni vigumu kubadili mitaala yote kwa Kiswahili kwa wakati mmoja, hebu tuende kwa awamu kama tulivyofaulu kuibadili katika shule za msingi.
 
Mbona Kenya na Uganda wanatumia Kingereza hicho hicho elimu zao ni bora zaidi ya kwetu?

Wao wana tofauti gani na sisi?

Nchi zao ni kama sisi,tunafanana fanana....inakuaje wao wafanikiwe zaidi yetu?

Una hoja ya hili?

Usilete matusi lakini
Wao wana ukabila, na kinachowaunganisha wakiwa nje ya vijiji vyao ni lugha ya Kiingereza sisi ni Kiswahili. Kwa maana hiyo wao wanapokwenda vyuoni wanafahamu zaidi Kiingeza na maeneo yote wanatumia Kiingereza, vinginevyo hawataelewana. Tofauti na sisi ambapo mwanafunzi akitoka shuleni au chuoni Kiingereza anakiacha huko huko zaidi ya zile familia zenye uzungu uzungu. Ziko familia zenye uwezo wanapeleka watoto wao katika English medium schools, lakini wazazi wenyewe hawajui Kiingereza, unadhani pale nyumbani itatumika lugha gani?
 
Back
Top Bottom