Dr.Milton Mahanga afungua kesi dhidi ya Msemakweli


Unaposema kawadhalilisha, you have already taken sides kuwa wewe unawatetea hawa mafisadi wa elimu kuwa hawana hatia; yaani Kainerugaba msemakweli kawaonea!! Tuiache mahakama iamue kama hayo aliyoandika Msemakweli ni kweli au sio. Let us not prejudice the case by insinuating innocence.
 

Balantanda, heshima mbele mkuu. Kainerugaba Msemakweli kwenye maandishi yake hajasema kua Mahanga sio msomi mzuri la hasha, yeye anasema hiyo shahada ya uzamifu yaani PH.D ambayo Mahanga anaitembeza ni feki kwasababu Washington International University ni chuo kisichotambulika katika medani za kitaaluma duniani!! Hata huko marekani anakosema ndiko alikoipata wanathibitisha kuwa chuo hicho ni feki!!Tafadhali soma # 34 kwenye thread hii.
 
(sawa na CPA)??? yale yaleee

Usikurupuke bana...Nimekwambia Mahanga ana CPA...Pia ana Certificate nyingine katika materials Management ambayo ni sawa na CPA...Nazungumzia CIPS/CSP(De novo atanisahihisha hapa)
 
Usikurupuke bana...Nimekwambia Mahanga ana CPA...Pia ana Certificate nyingine katika materials Management ambayo ni sawa na CPA...Nazungumzia CIPS/CSP(De novo atanisahihisha hapa)

nadhani wote tuko pamoja ila ni lugha au translation, Makongoro ni one of the highly regarded and qualified professional when it come to supply chain management [which is wider that purchasing and supplies or materials management].... CIPS inatoka Chertered Institute of Purchasing and Supplies UK na unapata baada ya michujo yote kama ilivyo ACCA; CSP inatolewa Tanzania

Tatizo la Mahanga ni ile Dr. ile PhD yake feki jamani, aiondoe tu kwenye wasifu wake hatapungukiwa na kitu, usomi si lazima PhD
 

Nimekusoma mkuu,sipipingani na Msemakweli hata kidogo bali kuna mtu nimemquote hapo juu(angalia bandiko langu) ambaye amediriki kusema kwamba Mahanga hana elimu...Angalia post ya huyo jamaa hapa chini


samvande2002
samvande2002 has no status.
Senior Member



Join Date: Fri Mar 2009
Location: pretoria, R.S.A
Posts: 75
Thanks: 5
Thanked 9 Times in 8 Posts
Rep Power: 21

re: Dr.Milton Mahanga afungua kesi dhidi ya mtunzi K.Msemakweli.
huyu jamaa mbona huwa hajiamini hata akiwa anahojiwa tu, hana elimu huyu..hawezi hata ku make points kwenye public, kwanza jimbo lake la ukonga limemshinda..hajafanya lolote jimboni kwake..sasa hivi ndio anajifanya kukwangua kwangua barabara za huko ukonga mazizini ili aonekane anafaa..hapiti safari hii!
 
Mkuu, huu ni ugonjwa wetu watanzania, kukurupuka!! i am sure samvande2002 amekurupuka tu
 

Niko na wewe katika hili mkuu Field Marshall ES.

Lakini ni muhimu kuelezea zaidi kidogo kwa ajili ya kuelezea na wengine waelewe kwa nini Mahanga ameenda mahakamani na sio TCU.

Mwenye kitabu chake amesema Mahanga ameghusi shahada yake ya udaktari wa falsafa.... kwa maana nyingine amesema Mahanga amefanya kosa la JINAI.

Kitu ambacho kingemfanya Mahanga kwenda TCU ni kama mwenye kitabu chake angesema Mahanga ana shahada ya udaktari ambayo haitambuliki hama nchini (un-acredited PHD in Tanzania)....

Kwa hiyo ni muhimu muelewe kwamba hii kesi ni rahisi sana, na kwa sheria za nchi mwenye wajibu wa kuthibitisha ni anayetuhumu sio mtuhumiwa... sasa mwenye kitabu chake ndiye akipenda aenda TCU na kukote kule... lakini sio Mahanga.

Na Mahanga akipata tu barua kutoka chuo chake kwamba naam amesoma chuo hiki xyz na ni mhitimu wao shahada ya udakari wa falsafa, kesi itakuwa imeisha.

Haya ndio madhara ya ku-think locally and ku-act locally!
 
kama kweli hii kesi itasikilizwa na sheria itachukua mkondo wake, Mahanga anaweza kushinda hii kesi kwa maana moja, kama hicho chuo alichosoma kilisema wanatoa PHD kwa miezi sita na kweli wakampa basi atakuwa na Phd kwa viwango vya hicho chuo na hiyo haiwezi kuwa ni feki katika sheria, kwani atakuwa kaipata kihalali kwa kuisomea miezi sita.

lakini tukija kwenye maswala ya Taaluma, hapo ndipo u-fake wa hiyo Phd utakapoonekana, kwani TCU wao wana criteria za kujua hii ni ndio na hii ni sio
 
1. Hivi nikirudi TZ na PhD yangu ni lazima niende TCU? Mimi nilidhani TCU inahusika na registration and accreditation of local Universities. PhD yangu inawahusu nini?
2. Back to Makongoro. Huyu mbunge amesoma CPA muda mrefu kuliko hiyo PhD, ukiangalia cv yake amepata CPA katika miaka 5, wakati PhD amepata in 2 years!! PhD gani unapata in 2 years? Ingekuwa ameipata katika chuo cha maana labda ningeweza kuwa'convinced, ila PhD at Washington International University, a dubious college.
 

Kuhusiana na kesi za defamation,hii ya Mahanga v. Msema kweli et al ni libel....Kwa marekani Mahanga angetakiwa aprove kuwa kina Msema kweli wame commit actual malice,lakini kwa Tanzania nadhani tutakuwa tunatumia common law malice ambayo ni tofauti na actual malice ya USA ambayo waliibadilisha mara baada ya kesi ya kina Sullivan ya mwaka 1964, common law malice imeweka emphasis but not limited to; spite, ill-will, bad faith or indirect motive...Yote hayo yanaweza yakawa yamemuongezea Mahanga msukumo wa kufungua kesi,hata hivyo still burden ya kuprove malice ni kubwa sana kwa paintiff na si rahisi kama unavyoelekea kupendekeza.
 

Sijui kama ni lazima uende TCU ama la,isipokuwa nachofahamu kuna international recognized association or organization ambazo zina deal na accredition kwa mfano IAO,jambo ambalo ni shughuli ya mwajiri kulifuatilia.
 
- Hizi PhD za kina Mahanga na wengine wengi tatizo lake ni moja tu hazitambuliwi na International Academic Community, lakini ni PhD ila ni worthless ndio maana Mahanga atashinda hii kesi kwa sababu aliyonayo ni PhD hiyo ni fact, my opinion ni kwamba hizo PhD ni kihiyo at best.

Respect.


FMEs!
 

Asante sana mkubwa naendelea kupata supu maana nimeamka na hangover kidogo
 

Mkuu Field Marshall ES,

Walahi nashindwa kuelewa mbona somo lako rahisi sana (no-brainer) halieleweki na vijana wa kisasa kwa nini?
 

Kama haitambuliwi na ukaiwakilisha kama ina tambuliwa,then inaweza ku constitute fakeness,kesi hii pia inategemea na serikali yenyewe,kama sijakosea,serikali pia inaweza ikaprovide accredition,na kwahivyo hiyo ni mojawapo ya namna ambayo serikali inaweza kutumika kumbana Msemakweli....Kwahiyo hapo tunarudi kwenye kuangalia ni utaratibu upi unatumika na serikali yetu kuhusiana na issue nzima ya accredition kwasababu shutuma zilizotolewa zimetolewa kutokana na public office anayo ihold ndugu Mahanga.

Kwa kifupi kuwa na Phd isiyotoka kwenye an accredited instituion na ukaiwakilisha kama vile ni accredited basi Phd hiyo ni feki chini ya taratibu hizo,ni kwamba haikubaliki....lack of authencity.

Ni matarajio yetu kuwa serikali ina utaratibu huo,lakini inavyonyesha ni kwamba haina utaratibu wa kufuata accredition kutokana na ukweli kwamba si Mahanga peke yake aliyekumbwa na tuhuma hizo,ni wimbi la viongozi wengi tu,na hilo linampa nguvu za ziada defendant.....

Pia utofauti wa kesi utakuwa mkubwa zaidi endapo ni kweli kuwa Phd yake ameipata from an accredited institution,yani kama angekuwa kwenye ile nafasi ya Daudi Mathayo basi angekuwa na nguvu zaidi za kupiga kelele,na kama ni kweli kuwa Phd yake kaipata kutoka kwenye unaccredited institution,then anapoteza muda tu.....Kwasababu kama public office anayo ihold inahitaji Phd ambayo siyo worthless kama unavyodai,halafu yeye akaileta kama ni worthy,basi inaitwa fake na si wothrless tena,yes it was unworthy but presented as worthy hence fake.
 

Jmushi1

Naomba kuweka rekodi sawa.... hili ni tatizo kwa watu wengi wa kada mbalimbali kutoka umma na binafsi, academia na proffesionals ....sio la wanasiasa/viongozi tu!
 
Jmushi1

Naomba kuweka rekodi sawa.... hili ni tatizo kwa watu wengi wa kada mbalimbali kutoka umma na binafsi, academia na proffesionals ....sio la wanasiasa/viongozi tu!

Ndiyo hivyo,chini ya civil case hii, hili ni tatizo la public figures wenye kuhold public offices,na Msema kweli anaweza kusema tu he walked like a duck and talked like a duck...Hell yeah he should've thought it was a duck kwanza given the fact our Govt incompetency maybe even on Mahanga's field,kama kuna matukio yaliyotokea ya udhaifu wa kiutendaji wa serikali kwa ujumla,ama hata pengine kutoka kwenye wizara anayoiongoza,then ntolee,na pia kama kuna wimbi hilo la Phd feki basi hakuna kesi kwasababu uwezekano wa kuprove malice unazidi kupungua.
 
Hivi mie naomba niulize kumbe Tanzania unaweza kusema mie nina degree fulani wala usifanywe kitu chochote ikachukuliwa kama kitu cha kawaida tu. Amakweli nakubaliana na mdau mmoja hebu tuzitofautishe hizi PhD maana tunakolekea tunaweza kuzalisha taaluma mbovu kabisa.

Mfano nyie mmezoea kumuita Dr Salim Ahmed Salim. Yule jamaa ana honoraria doctorates tu hana PhD. Zamani nilikuw nabishana sana na watu kuhusu hilo mwishoe nikaja kubahatika kuona CV nikaa kimya. Sasa hatari ya mtu kama huyu ni vp akija akaingia darasani afundishe wanafunzi kuna hatari akawa anazungumza vitu pasina kuwa na theory yake chini kusupport matokeo yake anaishia kutolea mifano ya sehemu alizokwenda na watu aliowaona. Hii inakuja baadae kuleta hatari kwa vijana wanaosoma kwake wanakuja kuargue hawana base yeyote ya argument zake matokeo tunazalisha wataalamu bomu nchini.

The same apply to the bogus PhD zinaweza kuja kuwaletea hatari ya kuzalisha watu wasiofaa katika jamii na matokeo ikawa hasara kwa taifa ni hilo naendelea na supu yangu na chapati!!
 

Angalizo tu ... kumbuka alipewa nafasi ile (unaibu waziri) kwa sababu qualification ya nafasi yake ni kuwa mbunge... na qualification ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika. kwa hiyo kuwepo kwake na un-accredited PHD has nothing to do na kazi aliyopewa pamoja na kwamba ni puplic post.

Goodmorning Americans, Goodevening... East africanas... and Good night and Asians!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…