Hii PhD sio feki! Labda tunaweza kusema haina credibility lakini kuiita feki sio sahihi. Obviously Mahanga ameapply somewhere kuipata hiyo Phd, na amefanye kitu fulani ili kuipata e.g ameandika essay ya maneno 100 labda.
Unless kama kuna mtu anadai Mahanga hajaipata hiyo Phd kutoka hicho chuo, sidhani kama kuna mtu anadai hilo.
Ni wajibu wa employer kuangalia kama kuwepo kwa hiyo Phd kwenye CV ya mtu ni kitu kizuri au kibaya, Mahanga hajadanganya kokote, ni kweli anayo hiyo Phd na ndo maana ameiweka kwenye CV yake.
Mimi kama ningekuwa ni mwajiri, ningeangalia ile CV, nitagoogle ile Uni, nitakapoona reputation ya hiyo uni ndo nitanfanya maamuzi ya kumwajiri huyo mtu. Siwezi nikasema kuwa Mahanga ni mwongo, ni kweli amepata hiyo Phd, ila mimi nimeichukulia kama worthless, na kwa kuiweka hiyo Phd kwenye CV yake Mahanga naye nimemwona worthless.
Asante mkuu, tuna hasira sana kiasi kwenda kuamini kila neno letu liko sahihi,
Nimefurahia sana hayo maneno hapo chini, hata mimi kwa uelewa wangu wa PhD naona hizi za akina Mahanga ni worthless;, sijui anaifanyia nini au kwa nini aliichukua.
Kama unafananisha PhD na toys, basi Mahanga ana PhD toy , ila anayo! kama hili toy ni bastola, basi PhD ya Mahanga ni bastola toy kainunua kariakoo kwenye maduka ya watoto na siyo bastola real kama ya Jerry Muro aliyonunua duka la Mzinga! Ila anayo
I think our cry is the quality of his PhD. Kwa position yake kuwa na aina ile ya PhD hailijengi taifa , kiongozi ana inspiration kwa jamii na kuna vijana wataiga huu mtindo wa kutokuumiza kichwa na kupata PhD isiyo na input yeyote zaidi ya satus tu.
Mahakamani Mahanga atapeleka toy lake, na majaji wataliona na kusema yes you have it! lakini bado kesi hii haitaweza kubadili huu ufisadi wa elimu, tusipoangalia unaweza kuongeza kwa kasi kubwa sana kama Mahanga akishinda.
Lakini kama alivyosema Kang; nani wanawaajiri hawa watu?????????? na nani anataka wawe na hizo PhD, tukilifumbua hili swala tutagundua mengi nyuma ya pazia
Msemakweli ninachoona kavaa bomu kajilipua, kapiga adui walio kwenye target yake, ila most likely naye akauawa kwenye hii mission ya ushujaa wa style ya Hezbola! However, what ever that will happen in this case, TCU will wake up!
still Msemakweli anahitaji sifa,
ila sifa tu kwa wale waliotayari kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio kuwa serikali haijali wala haisikilizi which is the worse katika society.Leo hatuwezi kuwanyooshea vidole wanaowaua watu kwa kuwashuku uchawi, wala wanaowachoma moto washukiwa wa wizi...... if we can not correlate these issues na kuona zinafanana sana then we are not living by our own principles. Nikifika hapo naogopa kuwa sisi hatujajipanga bado, kanuni zetu za maisha zimetawaliwa na emotions ambazo huwa zinabadilika kutokana na nani anasemwa na wakati gani( in short double standards). Imefikia muda wa kutoona viongozi ni watu ila mawe. kama kuna mtu atanihukumu kwa hili naomba kuubeba msalaba huu kwa gharama yeyote ile
Nilichoona kwenye whole drama ni kuwa ''wezi' hawa wa PhD wamepigwa mawe tumeshangilia na tumesema wasulubiwe, kesho tukiona kibaka anachomwa moto, tutawalaumu waliowachoma moto!!
We dont have alternatives ya kutatua matatizo kwa akili zaidi ila tunaona imefikia muda wa kuchukua sheria mkononi kwa kivuli cha kuwa 'hawa ni viongozi' hii ni dalili ya kushindwa mapambano, ni kama zile ngumi za utotoni ukishindwa unauma au unakimbilia mawe! huku kuna wa kushangilia pembeni, ukifikiria haya yote naona yanaturudia sisi wenyewe!
Haya sasa Mahanga akishinda kesi ndo watu watazinunua hizi PhD toys kama njugu, tutakuwa tumefanya nini? Msemakweli akishinda kesi basi tunafungulia wimbi la watu kuiga style yake!