RESILIENT KATO
JF-Expert Member
- Aug 21, 2024
- 4,504
- 8,842
Matakwa ya mkapa ya mwintongo!!Kwa mfuatiliaji mzuri sana wa mambo ya siasa na Taifa ili tuna watu watatu ambao ni wa kuangalia kwa makini,
1.Makongoro Nyerere, Mzanaki
2. Muzamir kalokola - Mhaya
3. John Magufuli- Mzinza(Mchanganyiko muhaya na wasukuma au wasuubi wa biharamulo)
Ukabila mnaukataa lakin hawa viongozi wana utumia ili mambo yao yaende vema kwenye utawala, hii ni kutokana na kuwa na watu kwenye mifumo wanaoitajika
Mkapa aliwatetea sana wachaga na kuwapa sekta nyingi huko bandarini , kwenye ma bank na TRA,
Kikwete akawakumbatia wahaya Nshomile maana alijua kabila lake haliwezi kumsaport ndo maana akawaweka sana kwenye ngazi mbali mbali za siasa,
Suala linakuja hapa kuna muhaya Muzamiri anaibuka kuchukua form japo akili zake hakizo sawa saana, pamoja na kikwete kusapot wahaya lakin anaweza akaachana na kina Membe akaangalia mtu anayetokea kanda ya ziwa karibu na wahaya, hapo sioni Mwingine ni Magufuli, atakuwa katimiza matakwa ya Mkapa ya Mwitongo waliosema ama Makongoro au Magufuli mmoja awe rais, ni Mkristuuu, ni wa Kanda pendwa, pia hawa wote wawili rushwa kwao mwiko, japo naye akiendekeza ukabila anaweza kuwajaza wasukuma ambao kajinasibisha nao mpaka tukalia hahaha, ila wasukuma watamfelisha kwasababu kichwani hazimo sana
Ndo maana nasema Kikwete anamsapoti Muhaya muzamiri lakin CV yake ikiwa siyo tuna opt Magufuli, achana na wana maigizo wanaoenda kwenye makaburi eti kuomba baraka za mwalimu(Membe) au kina lowassa wanaonunua watu kujaza mikutano, huu ni muda wa wazee hawa kustaafu, tunataka damu changa,
Ndo maana wagombea wamekuwa wengi sana kupitia CCM ili tukimkata Bilali makamu wa rais, tukamkata Sitta Spika mstaafu, Sumaye waziri mkuu mstaafu, tukamkata Pinda waziri mkuu iwe rahisi kumkata Lowassa mwenye tamaa, ijenge mazingira kwamba kumbe mawaziri wakuu wastaafu na waliopo wamekatwa
Nasikia na Mwingine Wassira naye eti alitangaza nia, huyo atulie alivyo mlevi wa madaraka ukute akikatwa NEC ataenda kugombea ubunge tena nao anaweza kuukosa maana vijana wamebase sana kwa maendeleo si watu,
Nimevuta picha walivyokaa wakipendekeza majina!!
Hivi ni kwanini makongoro alikatwa hata Tano Bora hakuwepo!!?
Kuna chuki yoyote kati yake na mkubwa mmoja!!?