Hili la kumkamata nafikiri ndiyo Mwakyembe alikuwa analiomba kwa udi na uvumba, kwani kumkamata tu haitoshi jibu ni je wataweza kumhoji?, akikataa kuongea watakaa naye kwa muda gani?, watamfunga nyaya za umeme mpaka aongee?. Hii sasa ni starting point nzuri sana kwa wapiga vita ufisadi. Nadhani wakimkamata huyu bwana watakuwa wamefungua njia ya kumkamata EL, RA, Hosea et al. Otherwise watakuwa wamemtengeneza Mwakyembe kuwa Mandela wa Bongo.
Ni jambo zuri kudhihirisha u msafi.Ishu ni kwamba na wenyewe wanaotaka kuwahoji wenzao ku-prove usafi wao nao je ni wasafi? kazi ipoNami nimeona katika star tv magazeti. Pccb katika hili la kumkamata wamechemsha. Kwanza wabunge tuna kinga katika tunayosema si tu ndani ya ukumbi bali pia katika viunga vya bunge. Takukuru hawana mamlaka ya kumkamata mbunge kwa matamshi aliyoyatoa kwenye press conf iliyofanyika kwenye viunga vya Bunge. Wanajimwambafy tu, hawana uwezo huo. Jambo la msingi ni wao kuhakikisha wito wao unaitikiwa na wabunge na kupata maelezo yao. Ni muhimu wabunge kuonyesha jamii kuwa hatuna mawaa katika mienendo yetu. Kuhojiwa na kutoa ushirikiano ni hatua mojawapo ya kuithibitishia jamii kuwa tu wasafi.
Currently Active Users Viewing This Thread: 52 (16 members and 36 guests)
Susuviri, Arnold, Buchanan, Edson, herikujua, Hofstede, Hujale, Jmpambije, JS, Kibunango, Limbani, Mfunyukuzi, Pilato2006, Shishye, Watu, Zitto
Time: 11.00 AM - Thursday
Namwona Mh yupo humu ndani... hivi mheshimiwa uko bungeni au? Maana naona you are surfing the internet saa za kazi.... tehehehe...hiyo nayo siyo kosa?
But seriously, kuna misdemeanor na makosa mengine ambayo yanaweza kushughulikiwa within the structure of the parlament, lakini ni uwendawazimu kuishikilia bango TAKUKURU kuhoji na kumkamata Mwakyembe kwa kosa la kupokea posho mara mbili.
.Kwa maoni yangu, Mwakiembe hakamatiki kwa ajili ya matamshi yake ya Dodoma, unless PCCB walimtaarifu spika kwa maandishi kuwa wanamuhitaji Mwakiembe kwa mahojiano, huku Mwakiembe mwenyewe amepelekewa samansi ya PCCB kuitwa kwa mahojiano,akakaidi, ni kweli anakamatika.
mimi ambacho kinanishangaza, si hoja ya kukamatwa Mwakyembe. ila ni vile gazeti la Mtazania lilivyogeuka kuwa jukwaa na PCCB , kutolea taarifa, ni kwanini habari hizi zinafika kwanza Mtanzania kisha kusambaa kwa magazeti mengine, ? ooh sorry kumbe hili gazeti linamilikiwa na watuhumiwa wa Ufisadi, kwa hiyo ipo mikakati kati ya Hosea, RA, NA mzee wa Monduli.
mimi ambacho kinanishangaza, si hoja ya kukamatwa Mwakyembe. ila ni vile gazeti la Mtazania lilivyogeuka kuwa jukwaa na PCCB , kutolea taarifa, ni kwanini habari hizi zinafika kwanza Mtanzania kisha kusambaa kwa magazeti mengine, ? ooh sorry kumbe hili gazeti linamilikiwa na watuhumiwa wa Ufisadi, kwa hiyo ipo mikakati kati ya Hosea, RA, NA mzee wa Monduli.
Vipi na zile taarifa zinazoyafikia haraka sana yale magazeti ya yule fisadi nyangumi(mengi)?.Utasikia ohoo mwakyembe aliatakuchomwa kisu,mwakyembe ni mti mkavu hauchimbwi dawa?. hiyo yote nini bwana.wewe chapa kazi wananchi watakurudisha jimboni na sio media.
pccb bana,yaani wanaamka tu bila kupiga mswaki!!!!
kwani kuna tatizo gani kwenda kuwasikiliza, hofu ya nini?
jamani hawa wanasiasa wanatuchanganya sana ni wala rushwa sana , hakuna cha wapambanaji wa ufisadi hapa ni wote mafisadi kwa ujumla wao
ningewaelewa hapo bungeni kama wangekomaa na hata kujiuzulu kama alivyofanya mrema , serikali chafu na wabunge hatuna kabisa , nadhani hawafiki watano wenye moyo wa dhati kutetea umma wa tanzania
Akawasikilize kina nani? Kwani wao PCCB rushwa wanazopokea nani huwa anawahoji? The point ni kuwa yeye Hosea,uchafu wake kausafisha lini,na kama kupokea posho mara mbili ni rushwa,vipi wao PCCB wanapojaza Imprest za uongo na wanajidai kwenda kukamata watuhumiwa wa rushwa,kisha wanaishia kwenye mabaa kubwia maji ya Ilala (beer) nani huwa anawahoji? Tunaishi nao,na tunawafahamu vizuri sana.
Masikini Tanzania....na huyu naye atakuja hapa kukaripia ufisadi....kweli ufisadi ni kansa ya akili iliyosambaa kila pande ya nchi yetu
omarilyas